Bodhichitta
JF-Expert Member
- Jul 1, 2015
- 315
- 762
Kiongozi ukisikia ushujaa ni kujitoa,Dk. Zakir Naik ni mhubiri ambaye amealikwa kuja kufanya mijada ya kidini Tanzania, anatarajiwa kufanya mihadhara mitatu
Mihadhara hiyo itakuwa inajadili kuhusu Mtume Muhammad na Yesu
Mihadhara yake itarushwa live na Azam TV na ZBC2
Mhadhiri huyu ana asili ya India na anamiliki channel inayoitwa Peace TV
Dk. Nakir anatafutwa na mamlaka za kisheria za nchi yake ya India kwa kutoa mahubiri yanayochochea ugaidi na chuki katika ya makundi tofauti ya Dini
Pia amepigwa marufuku kuingia nchi za Malaysia, Sri Lanka, Uingereza Canada, na channel yake ya Peace Tv kupigwa marufuku kuonyeshwa na Tv yoyote kutokana na mahubiri yake kuonekana hayafai
Mojawapo ya kauli tata alizowahi kunukuliwa Dk. Zakir Naik ni pamoja na
"Kama bin Laden anapigana na maadui wa Uislamu, mimi namuunga mkono. Ikiwa anaitisha Marekani—gaidi mkubwa zaidi kuliko wote—mimi niko pamoja naye. Kila Muislamu anapaswa kuwa gaidi."
Dk.Nakir pia anatajwa kuwa mahubiri yake yalichochea shambulio la kigaidi lililotokea Sri Lanka mwaka 2019 siku ya pasaka, na mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea Dhaka mwaka Bangladesh mwaka 2016
Jitoe wewe ukamkamate na umuwasilishe sehem husika na utoe maelezo juu yakutafutwa kwake.
Jipange kiongoz uwe shujaa itakuwa ni jambo la kherii.