Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Hiyo picha hapo jama kapiga goti mbele kuna mzungu anamuomba kazi
 
Nilivyosoma tu kichwa cha habari nikajua mleta uzi ni msabato. Hawana kazi nyingine zaidi ya kulalama na kujiona wenye haki. Kizazi cha mafarisayo. Wanatumia muda mwingi kunyooshea vidole makanisa yasiyo ya kisabato hasa ukatoliki huku wakisahau kahaba mkuu ni miili na mioyo yao na matamanio yao wenyewe. Kilicholetwa hapa hakina tofauti na anachofanya Gwajima - kuandama wenzie tu badala ya kuhubiri injili. Ni upuuzi uliopitiliza kwa mtu yeyote anayejiita Mkristo kupoteza muda kutetea na kuponda dini zilizoletwa na wanadamu. Inakusaidia nini kujua kuwa kahaba sijui mpinga Kristo ni Papa wakati hujioni wewe mwenyewe kuwa unampinga Kristo kwa kufanya mambo yasiyokuhusu tena kwa njia ambayo hata Kristo hakuwahi kuifikiria?

Kristo alisema wewe Petro umfuate. Kitakachompata Yohana hakikuhusu. Na kama unaijua sana Biblia ungekuwa umeshajua chochote kinachofanyika hapa duniani anakifanya Mungu mwenyewe - kibaya kwa mkono wa "shetani" na kizuri kwa mkono wake kwa sababu zake. Kazi yako ni kumwabudu na kumwacha afanye yake. Hangaika na roho yako ili Mungu aje kufanya makao humo uwe mtu wake naye awe Mungu wako. Ndo kuingia mbinguni huko. Hili si swala la baada ya kifo bali ni la sasa. Ufunuo hauonyeshi kama kuna mbingu zaidi ya hapa. Utake neno moja nalo ulitafute - kuutazama uzuri wa Bwana na kutafakari hekaluni mwake. Sasa badala ya kukaa moyoni na kuutazama uzuri wa Mungu unarandaranda kuzodoa taasisi za walimwengu. Mpaka utakufa hujaionja mbingu ukisubiri kwenda mbinguni baada ya kufa kutokana kwa kufikiri unachuma thawabu kwa kuzodoa wakatoliki. Mna-complicate sana mambo.
 
hapo ndipo penye Subira ya watakatifu hao wazishikao AMRI ZA MUNGU na KUWA NA USHUHUDA WA YESU
uf 12:17

SASA SIJUI NI MBINGU IPI HIYO MNAYOISUBIRI ISIYOTII AMRI ZA MUNGU

Na moja wapo ya Amri za Mungu ni SABATO
Unashika Sabato wewe ni muebrania...?
 
Pole sana, kama wewe ni msomaji biblia na ukawa unaamini sabato ni jumapili basi ulikuwa na tatizo. Sabato ipo wazi katika biblia ni jumamosi, ila pamoja na hilo haimaanishi kwamba kusali jumapili sala zako hazisikiki.

Wakatoliki wa ukweli wanajua sabato ni jumamosi, na wanaendelea kuabudu katika siku ya jumapili.

Sabato lengwa kibiblia si jumamosi wala jumapili wala jumatisa bali pumziko/amani anayopata mtu baada ya kuamua kumbebesha mizigo yake Bwana wa Sabato. Sabato ni pumziko. Sasa ukristo ni maisha ya kiroho kwa hiyo tukiongelea pumziko basi ni la kiroho. Kupumzika jumamosi au jumapili ni kupumzisha mwili kwani unachoka kwa shughuli za siku sita na kuhitaji kuhuishwa kama tulivyoagizwa hata kupumzisha mashamba kila miaka saba.

Halafu tumeonywa tusibishanie dini. Sijui nimefikaje hapa? Sirudi.
 
Sabato lengwa kibiblia si jumamosi wala jumapili wala jumatisa bali pumziko/amani anayopata mtu baada ya kuamua kumbebesha mizigo yake Bwana wa Sabato. Sabato ni pumziko. Sasa ukristo ni maisha ya kiroho kwa hiyo tukiongelea pumziko basi ni la kiroho. Kupumzika jumamosi au jumapili ni kupumzisha mwili kwani unachoka kwa shughuli za siku sita na kuhitaji kuhuishwa kama tulivyoagizwa hata kupumzisha mashamba kila miaka saba.

Halafu tumeonywa tusibishanie dini. Sijui nimefikaje hapa? Sirudi.
Wasabato siyo wakristo
 
Ukifel kidato channe Mara nyingi jamii inakuuliza ,, yaan umekoswa hata ya kwenda ualimu ? Hapa ndipo shida ilipo.
6fd9b58a43c6cef9a362c0e160aab9e5.jpg
 
Hoja dhaifu kwa mtu anayejiita padri. Wenzio wanakiri wazi kuwa papa ndiye mnyama ila wako huko kwa maslahi tu.

Haya nikirudi kwenye hoja yako ni lazima huyo mnyama Ellen G. White kama ulivyomwita kuwa ndiye namba 666 inamsema, sharti atimize maelezo yaliyoko Daniel 7:21-21 na ufunuo 13 15-18.
1. Huyo mnyama atatesa watakaktifu kwa miaka 1260. Ellen G white hata hakufika miaka 90 ya uhai wake. Hoja yako ni mfu.
2. Mnyama anayetajwa katika ufunuo 13:15-18. Atalazimisha watu wote ulimwenguni kuisujudia sanamu yake. Ellen G. White alishakufa siku nyingi hana mammlaka ya kushinikiza watu wote wamwabudu. Lakini roman catholic na papa wana mamlaka hayo kwa kuwa kila taifa linamtii papa.
3. Alama ya 666 inahusu mnyama au mamlaka kama biblia inavyosema katika Daniel 7. Wanyama ni wafalme juu ya uso wa dunia. Ellen G. White hakuwahi kuwa mtawala juu ya uso wa dunia, bali ipapa ni mamlaka iliyotoka katika ufalme wa nne juu ya uso wa dunia, yaani rumi.
5. Upapa ni taasisi hivyo kumhusisha mtu mmoja na taasisi ni kukosa hoja. Hata Nero mnayedai ndiye mnyama sio taasisi.
Mpaka hapo umeshajua kuwa njia ya mwongo ni fupi. Nakishuri acheni kudanganya watu mtakija kudaiwa hizo roho mnazozipotosha. Mungu hadhihakiwi.
Naona hamjui hata mnachokiongea mana mnazd kutuchanganya tu,uzi huu unasema kahaba wa ufunuo ni kanisa katoliki na mmeleta na baadhi ya mifano yenu kama ushahidi wa rangi za mavazi na kuwaua watakatifu na hapa unasema papa ndo mnyama na hapo hapo mnatuambia kwny huyo mnyama kutaibuka pembe ndogo katika pembe kumi ambayo itaangusha pembe nyingine tatu nayo pia mwasema ni upapa huo. Haya labda tuanze na mistari hii
1. Katika point yako mosi ya sasa umesema papa ndo mnyama, tizama ufunuo 17:16
Revelation 17:16
[16]And the ten horns which thou sawest upon the beast, these shall hate the whore, and shall make her desolate and naked, and shall eat her flesh, and burn her with fire.
Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.(kama hujui kuna wanyama wawili toka katika ufunuo 13 wa kwanza ni yule mwenye vichwa saba na pembe kumi na wa pili ni yule atakayeibuka na kutengeneza sanamu ya mnyama wa kwanza na kulazmisha watu wamuabudu mnyama wa kwanza na huyu ataleta chapa 666 ili mtu asiuze wala kununua bila chapa ndo mna verse hii inasem zile pembe 10 za mnyama wa kwanza n wafalme kumi ambao pamoja na mnyama wa pili watafanya vita na huyu kahaba na kumtokomeza kabisa..je unataka kusema mnyama huyu unayemuita ww papa atafanya vita na kahaba huyu mnayetuaminisha katika uzi huu kuwa ni ukatoliki na wataufuta au kuutokomeza kabisa ukatoliki? Na umesema mnyama atatawala siku 1260(miezi 42 kwa kadiri ya unabii wa biblia) ambaye ww wamuita papa sasa na baada ya hapo inamna hatakuwepo kabisa.je upapa haupo sasa?au hzo siku 1260 bado hazijaja na ukisema hazijaja utuambie kama zikija papa mnyama atautokomeza ukatoliki ambao mwadai ndiye kahaba.
Waweza kusema papa atakua mnyama yupi kati ya hao wawl mana nmekusaidia hapo juu,ukisema yule mwnye pembe kumi na vichwa saba nitakuuliza hzo pembe kumi ambazo biblia yasema ni wafalme kumi ni akina nani na hvo vichwa saba ni akina nani ambayo biblia yasema ni wafalme saba,watano wameshaanguka,mmoja yupo na wa saba hajaja na ukumbuke katika vichwa hivi saba ndio kuna kimoja chenye jeraha la mauti(sasa xjui kitakua kati ya hvo vitano vlivoanguka kama utasema n upapa).ukinijibu kuwa upapa ni mnyama wa pili,nitakuuliza mnyama wa kwanza ni nan sasa?
Tizama nanukuu baadhi ya mistari ya nilivovisema:
Revelation 13:11-12,14-15,17
[11]And I beheld another beast coming up out of the earth; and he had two horns like a lamb, and he spake as a dragon.
Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
[12]And he exerciseth all the power of the first beast before him, and causeth the earth and them which dwell therein to worship the first beast, whose deadly wound was healed.
Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
[14]And deceiveth them that dwell on the earth by the means of those miracles which he had power to do in the sight of the beast; saying to them that dwell on the earth, that they should make an image to the beast, which had the wound by a sword, and did live.
Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
[15]And he had power to give life unto the image of the beast, that the image of the beast should both speak, and cause that as many as would not worship the image of the beast should be killed.
Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
[17]And that no man might buy or sell, save he that had the mark, or the name of the beast, or the number of his name.
tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
Usisahau kutuambia ni lini hzo mieziu 42 zmetumika na kama bado inamaana wamaanisha badae mnyama papa atafanya vita na kahaba ukatoliki na kuutokomeza kabisa?
 
Kifungu gan ktk maandiko kimesema sabato ni ya waebrania ??
Sabato ilikuwa kwa ajili ya waebrania...Na iliwekwa mahususi kwa ajili ya kukumbuka siku walipotolewa utumwani Misri...

Sasa wewe Kenge mfuasi wa Nabii Mke, mama watoto wa Bw James white, niambie ni lini ulitolewa utumwani Misri....?

Rejea kutoka 20:1-8
 
Sabato ilikuwa kwa ajili ya waebrania...Na iliwekwa mahususi kwa ajili ya kukumbuka siku walipotolewa utumwani Misri...

Sasa wewe Kenge mfuasi wa Nabii Mke, mama watoto wa Bw James white, niambie ni lini ulitolewa utumwani Misri....?

Rejea kutoka 20:1-8
Well ,, nimeshapasoma na nmesoma tena upya ,, Hakuna mahali Mungu amesema Sabato ni ya waebrania !!.
 
Hivi nyinyi mnaosoma biblia mnazo akili kweli??? Mana nashangaa kwanini mnapotosha maana mm nikiisoma naelewa tofauti na mnavyo danganyana makanisani HUYO ANAEDAIWA KUWA KAHABA MKUU NI MWILI WA BINADAMU NA WAFALME NI NAFSI YA MWANADAMU .kuzini na huyo kahaba ni nafsi KUFUATA TAMAA ZA MWILI na kahaba kulewa kwa damu na maombi ya watakatifu ni NIKWASABABU WATAKATIFU WATAZISHINDA TAMAA ZA MWILI" kahaba" hivyo ndivyo ninavyo ielewa mm nisomapo biblia na ndiyo ukweli na najiamini nipo sahihi asilimia 100
 
Pole sana, kama wewe ni msomaji biblia na ukawa unaamini sabato ni jumapili basi ulikuwa na tatizo. Sabato ipo wazi katika biblia ni jumamosi, ila pamoja na hilo haimaanishi kwamba kusali jumapili sala zako hazisikiki.

Wakatoliki wa ukweli wanajua sabato ni jumamosi, na wanaendelea kuabudu katika siku ya jumapili.
Sasa kaeni mkubaliane. Wenzio wanasema sabato ni siku yeyote uliyoochagua. Kubalianeni kwanza huko kisha mrudi hapa.
 
Hata mimi ningefurahi mkuu Otorong'ong'o,kwani hiyo post ya Pd Amigu imeshiba kwelikweli.
Kama huyu padri ndiye mnamtegemea kwa hoja nawapa pole. Mapadri ninaowajua maparoko na mabruda nimefanya nao mazungumzo ya neno la Mungu tena nikiwa na wachungaji wa kilutheri. Wote walikiri kuwa wasemacho wasabato ni ukweli mtupu. Papa ndiye mnyama wa ufunuo 13. Ila sasa wafanyeje ilihali kula yao inaegemea kazi yao hiyo? Niliwatia moyo kuwa siku moja Mungu atawapa kazi nyingine bora zaidi ila wawe tayari kutoka babeli. Kuna mchungaji mmoja wa moravian ni rafiki yangu huwa nampa vitabu vya kanisa letu na anavitumia kufundishia.

Huyu padri wenu angekuwa mkweli angekiri kama wenzie walivyokiri. Ukimkiri Yesu atakukiri mbele za Baba na Malaika Watakatifu.
 
Juu ya hili usibishe. Wakristu wengine tofauti na wasabato tunaabudu jumapili na sababu kuu maadhimisho ya pasaka ni jumapili hivyo jmapili ni siku ya ushindi kwetu wakristo na ikatengwa hivyo.

Pasaka inaadhimishwa jumapili, na imekuwa stated kabisa katika biblia kuwa siku ya kwanza ya juma yesu alifufuka. From logic tuu utagundua kuwa jumamosi ni siku ya mwisho ya juma.

Ilaa, nimemuuliza swali kuwa, mimi ninayesali jumapili sala zangu hazisikilizwi.? Au je sala zake yeye anayesali jmosi zinasikilizwa sana zaidi ya zangu.?

Maana sioni kama ni big issue kusali jumapili kwa maana imeandikwa mungu yupo mahali popote, na wakati wote, ni wewe tuu kuomba na kusubiria majibu.

Bora wewe imelijua hilo ila kuna tahadhari kwa kutotii amri za Mungu.Mithali 28:9.
" Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo".
 
Back
Top Bottom