Mfahamu Meja Jenerali Muhiddin Kimario. Ukisikia mzalendo ndio huyu

Mwaka 77 alijenga uwanja wa ccm kirumba kwa kuchangisha wananchi sasa inakuwaje viwanja vinakuwa vya ccm?
 
Pichani ni Marehemu Major Generali Muhiddin Kimario, ni moja kati ya mawaziri wawili tu waliowahi kudumu katika nafasi zao za wizara ya mambo ya ndani kwa muda wa miaka mitano (5) katika Historia ya Tanzania.

Mwaka 1978 alitumwa kwenda mkoani Mwanza na Mwalimu Nyerere kwenda kuwaaga Wanajeshi waliokuwa wanakwenda kupigana Vita vya Kagera kumn'goa Idd Amin Dada, wakati akitoa Hotuba yake ndani ya Viwanja vya Nyamagana ghafla aliamua kujivua uwaziri na kuamua kwenda vitani "Mkuu wa Mkoa ninaomba ufikishe taarifa hii kwa mh Rais kwamba najivua Uwaziri na ninaamua kurudi jeshini kuungana na wenzangu leo kwenda kumshikisha Adabu Amin"

 
Amefariki 2005, ila Kisa chake cha kusikitisha ndio hiki
Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mbele wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya Karuma Kwa maajabu,Mwl Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu
 
Kuna siri nyingi sana kwenye utawala wa awamu ya kwanza
 
Hakuwa anatokea lake zone labda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…