Mfahamu Meja Jenerali Muhiddin Kimario. Ukisikia mzalendo ndio huyu

Uliyosema ni kweli kabisa ila wakati wa vita yeye hakuwa waziri kamili, nadhani huenda alikuwa waziri mdogo; sasa hivi sikumbuki aliongoza brigade gani ila ni kati ya wale mabrigedia na majenerali wapatao 12 walioingia na kuiteka Uganda yote.
 
Kabisa.. nyerere naye alikua mwoga sana..
Kuna kisa kingine cha kusikitisha cha jamaa mmoja alikua Captain wa Jeshi akiitwa Mohamed Martin Tamimu(Comandoo). Huyu aliuzwa vibaya sana kwa kupelekwa nje ya nchi kufanya kazi ambayo yeye akiamini ni yakulitumikia taifa.

Yalitokea mambo kadhaa. Waliomtuma wakamgeuka na kumruka, akawa adui wa huko alipotumwa na adui wa nchi iliyo mtuma! Akajikuta analazimika kuingia kwenye uasi/uhaini na aliuwawa pale Kinondoni Mkwajuni kwa kufyatuliwa risasi na mwanasiasa maarufu sana hapa nchini ambaye habari zake za mwisho alikua upinzani
 
Kumbe huo ujinga wa kupeana vyeo kijinga jinga ilianziaga zaman. Wanafichiama aibu ndo maana ata kizazi cha sasa kipo hvyo hvyo
 


Huu nao ni uwongo mwingi sana. Ni kweli Tamimu aliuwawa Kinondoni kutokana na uhusika wake katika njama za kupindua serikali mwaka 1982; hakuuzwa bali alijiunga na akina Zakaria Hanspope, Uncle Tom, Badru Kajaja na wengineo katika njama za kutaka kuipindua serikali kutokana na maisha magumu yaliyofuatia baada ya vita.

Tanzania ya leo tumelogwa nini kuamini hizi conspiracy theories kupita kiasi?
 
Wazalendo wa sasa mpaka Mzee meko awatangaze
 
Hizi habari ziko nyingi. Mimi ninae jamaa yangu alishiriki vita hivyo, alipotea Uganda kwa muda na alipatikana baada ya kuokotwa pembeni ya MTO hajitambui, wazee wake walishafanya hitma wakiamini alifariki. Huyu mzee alipata tb. Akikusimulia alivyoponea chupu chupu na majeshi ya Amini huwezi kuamini. Alipopotezana na wenzake hakuwa na chakula. Ilifika wakati ikawa anakunywa maji ya MTO yaliyokuwa yakinuka na kuelea maiti. Alikuwa anaumwa na tb kwa kipindi kirefu kutokana na athari za vita. Aliishia kupewa asante. Kwa kweli wako wengi. Na wakimsema vibaya sana Mwl Nyerere.
 
Dah! Pole zake ndio nchi zetu za kiafrica zilivyo
 
Habari moja kumhusu Kimario ni kwamba kuna kipindi kulikuwa na stalement kwenye mapigano na jeshi la Amin: askari wa Tanzania walikuwa wakiwasukuma askari wa Amin; na Amin anajibu mapigo kwa kuwasukuma askari wa Tanzania. Hii sukuma nikusukume ilidumu kwa siku kadhaa. Wakati huo waandishi wa habari wa Tanzania walikuwa wanaidadisi Serikali kuwaruhusu waende kujionea wenyewe mambo yalivyo ili waandike wanachoona na si kuambiwa tu na Serikali kama ilivyokuwa ikifanyika mpaka hapo. Serikali ikakubali kuwapeleka kundi la waandishi wa habari, akiwemo Ben Kiko ambaye wengi watakumbuka habari alizokuwa akiripoti kwenye Radio Tanzania kwa ustadi mkubwa. Ndege iliyowachukua waandishi hao wa habari iliondoka Dar na kutua Zanzibar. Hapo hakutelemka mtu na wala hakukuwa na kujaza mafuta. Badala yake mtu mmoja tu alipanda na ndege ikaondoka. Mtu huyo alikuwa Mhidin Kimario. Waandisshi wa habari wakawa wakijiuliza hivi kweli ilikuwa lazima ndege kwenda Zanzibar kuchukua mtu mmoja tu? Jibu walijionea wenyewe baada ya kufika Uganda na Kimario kushika hatamu ya kuongoza mapigano. Jeshi la Tanzania likawafurumisha askari wa Amin moja kwa moja. Mwandishi akamaliza habari kwa kusema kwamba kushinda kwa mapigano si kwa ubora tu wa askari wako au silaha walizo nazo ila pia na uongozi uliopo mstari wa mbele.
 
Kama kitu wewe hukijui usiseme kua hakipo au hakikuwahi kuwepo. Unajua baada ya kutoka vitani Tamimu alikua wapi na alikua anafanya nini?

Vita iliisha mapema 1979 baada ya Amin kuikimbia Uganda na Majeshi ya Tanzania yakatwaa Mamlaka ya kuiongoza nchi hiyo hadi walipochaguana wenyewe. Mwl. Nyerere alianza kuwaingiza wanajeshi wa Tanzania kwenye shughuli za siasa na kazi nyingine za umma

Njama za uhaini zilipangwa mnamo 1982 na ni sahihi unaposema Tamimu alikuwepo kwenye njama hizo. Lakini unajua kabda ya hapo alikua wapi? Unazijua mission zote alizotumwa na wakubwa zake akazitimiza kwa ufanisi na uaminifu mkubwa kabda ya kuuzwa na kusalitiwa na haohao waliomtuma na akajikuta sio tu kapoteza kazi yake bali pia akiwindwa ili auwawe? Kama hujui uliza mkuu wangu, wengine hatujasimuliwa tumeyaishi haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…