Mfalme ‘akiuawa’ huwa inachukua muda mrefu sana Taifa kupona

Mfalme ‘akiuawa’ huwa inachukua muda mrefu sana Taifa kupona

Mwaka 235 A.D kule Roma aliuwawa Kaisari aitwaye Severus Alexander. Aliuwawa kwa hila za majasusi wake waitwao The Praetorian Guard ambao walikuwa ndiyo kikosi cha ulinzi na ujasusi cha watawala wa Roma. Mtu ulikuwa huwezi kutawala Roma bila kutumia hichi kikosi.

Makaisari wa Roma walikuwa wanaheshimika kama miungu (Demi-gods), na hata kuwagusa ilikuwa ni sawa na kupingana na amri ya miungu. Utulivu na mafanikio ya dola la Roma, ulitegemea sana uimara wa kiti cha Kaisari. Makaisari wengi wa Roma kabla ya mwaka 235 A.D walikuwa ni lazima watokwe kwenye familia kubwa Roma (Roman Aristocracy) ambapo walifundishwa mambo ya utawala na siasa tangu wadogo.

Severus Alexander alivyoingia kwenye kiti alianza kufanya mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi, kisheria na kisiasa ambayo yaliifanikisha mno Roma ndani ya muda mfupi. Japo alikuwa na udhaifu mwingine mkubwa kwamba, alikuwa ni mtoto wa mama (Mama's Boy) ambaye hakuwa na uzoefu wowote wa vita. Hivyo alisoma mambo ya vita bila kwenda uwanja wa vita kama ilivyokuwa lazima kwa vijana wote wa Roma.

Hili tatizo ndilo lilimletea changamoto kwasababu alishindwa kusimamia nidhamu ya jeshi lake. Wanajeshi walikuwa wanafanya vitu vya hovyo lakini yeye kwakutokuwa na uelewa akawa anafanya nao mijadala tu. Watawala kabla yake walikuwa wanafahamu siasa za jeshi na waliweza kulidhibiti. Severus Alexander akiwa kijana mdogo alizidiwa na jeshi, kisha yeye na mama yake wakauwawa.

Baada ya kuuwawa, jeshi likamuweka madarakani askari mwenzao Maximius Thrax kama Kaisari mpya. Huyu hakuwa ametokea familia za watawala, na alikuwa hana elimu ambayo ingemsaidia kutawala. Katika utawala wake Roma ikaanza kuporomoka na ambapo kwa miaka 50 nchi haikuwa na mfalme anayeweza kumaliza muda bila kuuwawa na wanajeshi au majasusi. Hiki kipindi wanahistoria wanakiita The Third Century Crisis.

==================================================================
Kila nchi huwa na utaratibu wake wa kiutawala. Huo utaratibu ukivunjwa lazima madhara makubwa yawepo. Kwenye The Third Century Crisis walikuwepo watu zaidi ya 50 waliouwawa kwa kutaka kukalia kiti cha Kaisari ndani ya kipindi cha miaka 50. Kiufupi Roma ilikuwa imejaa vurugu kama utekaji, mauaji ya kutisha, vita, rushwa na dola kugawanyika.

==================================================================
IKO HIVI: Tokea mwaka 1961-2021, Tanzania imekuwa ikishikiliwa na kiti cha Uraisi. Raisi ni Baba, Raisi ni Mfalme, Raisi ni mungu-mtu, Raisi ni Jalala la lawama, Raisi ni alama ya umoja wa kitaifa na Raisi ni nguzo ya matumaini. Hii ndiyo Tanzania aliyoijenga Mzee Nyerere. Raisi anaweza akawa na madhaifu lakini tunamsitiri na kumstahi tukiwa na matumaini kwamba atamaliza muda wake halafu atakuja mwingine kurekebisha.

Ukweli mchungu ni kwamba miaka ya 1960's-1980's bara la Afrika liligubikwa na mapinduzi na muaji ya Maraisi. Mzee Nyerere alipona mara nyingi. Siyo kwamba alikuwa na nguvu, lakini watu wa ndani ya vyombo vya dola walikuwa wanamchukulia kama BABA YAO MZAZI. Wengi walijiuliza kwamba Mzee Nyerere akitoka nini kitafuata ???

Hata alipokuja Mzee Mwinyi ambaye Mzee Nyerere na kina Imran Kombe walimfanyia vimbwanga vingi kwasababu walikuwa hawamkubali, ukweli mchungu ulikuwa ni kwamba lazima amalize muda wake. Hili lilikuwa siyo suala la majadiliano bali mustakabali wa nchi.

Tatizo likaja mwaka 2005 alipoingia kaingia Cheki-Bobu Ikulu. Alivurunda mno nchi ikafika hadi kipindi wakafanya jaribio la kumleta Dikteta kurekebisha. Cheki-Bobu na udhaifu wake wote alivumiliwa na muda wake ukaisha. Mwaka 2015, aliingia Dikteta kwelikweli. Alifanya makubwa ndani ya muda mfupi huku akiacha vilio na maumivu mengi pia.

==================================================================
Bahati mbaya sana, wengi hawakumpenda na hawakumvumilia ambapo ilitakiwa mwaka 2025 awe anaondoka madarakani. Mbaya zaidi Tanzania kuna utamaduni wa pande mbili kupokezana miaka 10/10. Hivyo ni lazima Raisi amalize muda wake, mpende au msipende. Utamaduni huu ndiyo umeleta utulivu na amani kwa kipindi kirefu nchini.

Anaweza akaingia mvaa kobasi akasemwa sana, lakini hawezi kutolewa kwasababu lazima Raisi amalize muda wake. Kama hamumpendi msingepitisha jina lake kule NEC. Hivyo hata Wagalatia watasema na kutoa matamko, lakini hawafanyi jambo la kijinga kwasababu wanafahamu zamu yao itakuja.

Huu utaratibu unaweza kuonekana ni una ufedhuli mwingi lakini ndiyo ambao unafanya kazi kwa taifa changa kama letu (The Only Practical Method to Ensure Political Stability). Ni lazima mzani uwiane (Balance of Power), usipowiana ni lazima mtapata matatizo.

==================================================================
SHIDA INAANZA HAPA: Watu walio karibu na Raisi masaa 24/7/365 ni Majasusi na Wanajeshi. Hawa ndiyo humsaidia Raisi kutawala. Hapa Tanzania hili kundi tokea mwaka 1964 hadi 2021 lilijengwa kwa dhana kwamba Raisi hagusiki, hata iweje. Raisi ni mungu-mtu. Raisi ni Nchi. Raisi ni Baba. Hivyo kama kumdhuru subirini amalize muda wake ndiyo mtamgusa lakini mkimgusa akiwa madarakani mtayumbisha nchi nzima. Hili hata wale wenye falsafa tofauti ndani ya mfumo walikuwa wanakubaliana.

Baada ya mwaka 2021 utaratibu ulibadilika vibaya mno. MKUU WA NCHI aliguswa, kukawa na minong'ono, huku mahasimu wake wakajisifu hadharani kwamba "Sasa Bahari Iko Shwari" na kutamba kwa kejeli nyingi. Hakuna aliyewakeme. Miaka michache baadaye tunasikia minong'ono kwamba MKUU WA NCHI kweli alihujumiwa.

Ndiyo alikuwa Dikteta, Ndiyo alikosea mambo mengi tu. Lakini kwanini mlimpitisha mkifahamu tabia zake fika. Kwanini hamkusubiri amalize muda wake kama ambavyo mlimvumilia CHEKI-BOBU aliyekuwa anafanya mambo ya ajabu Ikulu yenye madhara makubwa kwa nchi ???

=================================================================
Tokea mwaka 2021 yametokea muaji makubwa ya kutisha kuwahi kutokea hapa Tanzania. Hayatakuwa mwisho kwasababu mzani wa madaraka haujakaa sawa. Mbaya zaidi imefahamika kwamba MKUU WA NCHI naye anagusika vizuri na haliwezi kutokea jambo lolote lile kubwa. Historia inaonesha kwamba mara nyingi mapinduzi makubwa, huzaa mapinduzi mengine. Nchi huchukua muda mrefu mno mpaka ije kutulia:

​
  • Mwaka 1651 waingereza walipindua mfalme wao na kumnyonga ila nchi ilikuja kutulia mwaka 1688 baada ya kuanzisha utaribu mpya wa kiutawala.​
  • Mwaka 1789 wafaransa walipindu mfalme wao na miaka zaidi ya 30 nchi ilijaa damu na vita, ikaja kutulia mwaka 1814.​
  • Mwaka 1776 makoloni 13 ya Marekani yaliasi dhidi ya Mfalme, na nchi ilikuja kutulia mwaka 1815 baada ya kumaliza ugomvi na Muingereza.​
==================================================================
Hata hapa Afrika mchezo ni uleule tu:

RWANDA: walimfukuza Mfalme Kigeri ila mpaka leo kila utawala mpya umeingia kwa kumwaga damu. General Kayibanda, General Habyarimana na General Kagame, wote wameingia kwa bunduki. Ila makosa yalianza kule kwa Mfalme Kigeri.

UGANDA: walianza na kumtoa Mutesa. Akaja Obote akatolewa. Akaja Amini akatolewa. Akarudi Obote akatolewa. Sasa yuko Museveni naye akiondoka haijulikani Uganda itakuwa kwenye hali gani. Hakuna anayeweza kuvaa viatu vya Museveni.

ZIMBABWE: nako ni hivyo-hivyo tu. Mubage alitolewa akaingia Munangagwa.

NIGERIA: walau kipindi hiki wametulia na wanapokezana kimakabila na kidino

==================================================================
Tanzania na Kenya, MUNGU alitupendelea mno. Jinsi tulivyokuwa tunayaangalia madaraka (Approach Towards Leadership) mbali na madhaifu yetu mengi imakuwa ni kuvumiliana mno (Tolerance). Siyo kwamba sisi tuna kitu cha ziada kuliko wenzetu lakini tuna kiwango kikubwa cha kuvumiliana.

GHANA, South-Africa na Botswana ni mataifa ambayo yameanza kukomaa hapa Afrika linapokuja suala zima la kuvumiliana kisiasa. Sisi hapa Tanzania tunarudi miaka ya 60's kuishi maisha ambayo hatukuyaishi. Maisha ya machafuko (Political Instability). Kitakachotokea Tanzania kipindi hiki ni kwamba kiti cha Uraisi kitatingishwa mno kwa miaka mingi, hata huyu wa sasa akitoka.

Tumeshatengeneza BAD PRECEDENT, na kutulia mpaka pande zote ziumie na kupata hasara kubwa ndiyo tutarudi kuwa kawaida. Ila kwasababu NOBODY IS SAFE. Kiufupi hata uweke wanajeshi barabarani, muda wako utafika tu. Mlichokianzisha mwaka 2021 lazima mkinywee, tena mtakinywea vibaya sana.

Siasa ndivyo ilivyo, historia imejaa ushahidi wa hichi nachokisema kuanzia Rome, The Rashidun Caliphate, Mongol Empire, Tang Dynasty n.k Kumuua mfalme (Mzuri au Mbaya) na machafuko yasitokee huwa ni nadra mno.

====================================================​
Kaisairi hakikuwa cheo ni jina kingereza ceasar.... Rome walikuwa na emporer mtawala .. Rome iliwapata emporers wenye majina ya ceasar kama wawili hivi kama sijakosea... hope nimekusaidia next time usitumie neno kaisari kama cheo...
 
CCM inavuna matatizo iliyoyapanda kuanzia miaka ya 60's. Maamuzi mengi ya wazee wetu hayakuwa sahihi. Kupindisha Demokrasia na kuhujumu mabadiliko kwa kutumia taasisi za kijasusi, kipolisi na kijeshi hakukuwa sahihi. Mwaka 1995 baada ya Mzee Nyerere kutumia mabavu kukanyaga Demokrasia akidhani anaokoa nchi, madhara ndiyo tunayavuna leo hii. Taasisi zetu za usalama zilionjeshwa damu za watanzania ili kupata madaraka na ukajengeka utamaduni mbaya mpaka leo.

Kila napoanzisha mada kusema madhaifu ya Mzee Nyerere wajamaa huwa wanakuja kunibagaza. Lakini ukweli ni kwamba ili kuitoa nchi hapa ilipo ni lazima tupitia milango ambayo tuliingilia. Kuanzia muungano mwaka 1964, katiba mwaka 1977, vyama vingi 1995. Pamoja na kupitia sera nyingi ambazo zinatengeneza sheria ambazo zimezalisha taasisi za kiutawala ambazo zinatuongoza hii leo.

Bila kukubali kujitazama kwenye kioo na kutambua matatizo yetu yaanza tokea awamu ya kwanza hatuwezi kufika popote kama nchi.

​
Kwa uelewa/taarifa ulizonazo Mkuu MALCOM LUMUMBA 1995 Lyatonga hakumgaragaza Mkapa?
 
Na vilevile ikawa kwa JPM kwamba asingeweza kuinyanyua nchi kiuchumi kwa kipindi chake (ingawa WB na IMF walisema tupo uchumi wa kati) wakati alieharibu hapo kabla kwa miaka 10 yupo na aona.
Ndio maana hotuba yake kwenye msiba wa mkapa alitoa pongezi kwa kufika uchumi wakati , alieleza alivyo fanya yeye mpaka alipoishia akaja magufuli ni kama alikuja kumalizia tu.
Kwenye hotuba hio alitoa kama kejeli fulani kuhusu vipi magufuli angefikisha lengo la dira ya taifa 2025 aliyo asisi mkapa.
Kama ulimsikia vizuri alisemea vizuri nafasi yake toka akiwa waziri kwa serikali ya mkapa hadi urais kwamba yeye ndie chanzo kikuu cha kufika kwenye uchumi wakati na magufuli hakuwa amefanya pakubwa , kama kuingiza mpira goli likiwa wazi.
 
1765596260412.png
 
Mwaka 235 A.D kule Roma aliuwawa Kaisari aitwaye Severus Alexander. Aliuwawa kwa hila za majasusi wake waitwao The Praetorian Guard ambao walikuwa ndiyo kikosi cha ulinzi na ujasusi cha watawala wa Roma. Mtu ulikuwa huwezi kutawala Roma bila kutumia hichi kikosi.

Makaisari wa Roma walikuwa wanaheshimika kama miungu (Demi-gods), na hata kuwagusa ilikuwa ni sawa na kupingana na amri ya miungu. Utulivu na mafanikio ya dola la Roma, ulitegemea sana uimara wa kiti cha Kaisari. Makaisari wengi wa Roma kabla ya mwaka 235 A.D walikuwa ni lazima watokwe kwenye familia kubwa Roma (Roman Aristocracy) ambapo walifundishwa mambo ya utawala na siasa tangu wadogo.

Severus Alexander alivyoingia kwenye kiti alianza kufanya mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi, kisheria na kisiasa ambayo yaliifanikisha mno Roma ndani ya muda mfupi. Japo alikuwa na udhaifu mwingine mkubwa kwamba, alikuwa ni mtoto wa mama (Mama's Boy) ambaye hakuwa na uzoefu wowote wa vita. Hivyo alisoma mambo ya vita bila kwenda uwanja wa vita kama ilivyokuwa lazima kwa vijana wote wa Roma.

Hili tatizo ndilo lilimletea changamoto kwasababu alishindwa kusimamia nidhamu ya jeshi lake. Wanajeshi walikuwa wanafanya vitu vya hovyo lakini yeye kwakutokuwa na uelewa akawa anafanya nao mijadala tu. Watawala kabla yake walikuwa wanafahamu siasa za jeshi na waliweza kulidhibiti. Severus Alexander akiwa kijana mdogo alizidiwa na jeshi, kisha yeye na mama yake wakauwawa.

Baada ya kuuwawa, jeshi likamuweka madarakani askari mwenzao Maximius Thrax kama Kaisari mpya. Huyu hakuwa ametokea familia za watawala, na alikuwa hana elimu ambayo ingemsaidia kutawala. Katika utawala wake Roma ikaanza kuporomoka na ambapo kwa miaka 50 nchi haikuwa na mfalme anayeweza kumaliza muda bila kuuwawa na wanajeshi au majasusi. Hiki kipindi wanahistoria wanakiita The Third Century Crisis.

==================================================================
Kila nchi huwa na utaratibu wake wa kiutawala. Huo utaratibu ukivunjwa lazima madhara makubwa yawepo. Kwenye The Third Century Crisis walikuwepo watu zaidi ya 50 waliouwawa kwa kutaka kukalia kiti cha Kaisari ndani ya kipindi cha miaka 50. Kiufupi Roma ilikuwa imejaa vurugu kama utekaji, mauaji ya kutisha, vita, rushwa na dola kugawanyika.

==================================================================
IKO HIVI: Tokea mwaka 1961-2021, Tanzania imekuwa ikishikiliwa na kiti cha Uraisi. Raisi ni Baba, Raisi ni Mfalme, Raisi ni mungu-mtu, Raisi ni Jalala la lawama, Raisi ni alama ya umoja wa kitaifa na Raisi ni nguzo ya matumaini. Hii ndiyo Tanzania aliyoijenga Mzee Nyerere. Raisi anaweza akawa na madhaifu lakini tunamsitiri na kumstahi tukiwa na matumaini kwamba atamaliza muda wake halafu atakuja mwingine kurekebisha.

Ukweli mchungu ni kwamba miaka ya 1960's-1980's bara la Afrika liligubikwa na mapinduzi na muaji ya Maraisi. Mzee Nyerere alipona mara nyingi. Siyo kwamba alikuwa na nguvu, lakini watu wa ndani ya vyombo vya dola walikuwa wanamchukulia kama BABA YAO MZAZI. Wengi walijiuliza kwamba Mzee Nyerere akitoka nini kitafuata ???

Hata alipokuja Mzee Mwinyi ambaye Mzee Nyerere na kina Imran Kombe walimfanyia vimbwanga vingi kwasababu walikuwa hawamkubali, ukweli mchungu ulikuwa ni kwamba lazima amalize muda wake. Hili lilikuwa siyo suala la majadiliano bali mustakabali wa nchi.

Tatizo likaja mwaka 2005 alipoingia kaingia Cheki-Bobu Ikulu. Alivurunda mno nchi ikafika hadi kipindi wakafanya jaribio la kumleta Dikteta kurekebisha. Cheki-Bobu na udhaifu wake wote alivumiliwa na muda wake ukaisha. Mwaka 2015, aliingia Dikteta kwelikweli. Alifanya makubwa ndani ya muda mfupi huku akiacha vilio na maumivu mengi pia.

==================================================================
Bahati mbaya sana, wengi hawakumpenda na hawakumvumilia ambapo ilitakiwa mwaka 2025 awe anaondoka madarakani. Mbaya zaidi Tanzania kuna utamaduni wa pande mbili kupokezana miaka 10/10. Hivyo ni lazima Raisi amalize muda wake, mpende au msipende. Utamaduni huu ndiyo umeleta utulivu na amani kwa kipindi kirefu nchini.

Anaweza akaingia mvaa kobasi akasemwa sana, lakini hawezi kutolewa kwasababu lazima Raisi amalize muda wake. Kama hamumpendi msingepitisha jina lake kule NEC. Hivyo hata Wagalatia watasema na kutoa matamko, lakini hawafanyi jambo la kijinga kwasababu wanafahamu zamu yao itakuja.

Huu utaratibu unaweza kuonekana ni una ufedhuli mwingi lakini ndiyo ambao unafanya kazi kwa taifa changa kama letu (The Only Practical Method to Ensure Political Stability). Ni lazima mzani uwiane (Balance of Power), usipowiana ni lazima mtapata matatizo.

==================================================================
SHIDA INAANZA HAPA: Watu walio karibu na Raisi masaa 24/7/365 ni Majasusi na Wanajeshi. Hawa ndiyo humsaidia Raisi kutawala. Hapa Tanzania hili kundi tokea mwaka 1964 hadi 2021 lilijengwa kwa dhana kwamba Raisi hagusiki, hata iweje. Raisi ni mungu-mtu. Raisi ni Nchi. Raisi ni Baba. Hivyo kama kumdhuru subirini amalize muda wake ndiyo mtamgusa lakini mkimgusa akiwa madarakani mtayumbisha nchi nzima. Hili hata wale wenye falsafa tofauti ndani ya mfumo walikuwa wanakubaliana.

Baada ya mwaka 2021 utaratibu ulibadilika vibaya mno. MKUU WA NCHI aliguswa, kukawa na minong'ono, huku mahasimu wake wakajisifu hadharani kwamba "Sasa Bahari Iko Shwari" na kutamba kwa kejeli nyingi. Hakuna aliyewakeme. Miaka michache baadaye tunasikia minong'ono kwamba MKUU WA NCHI kweli alihujumiwa.

Ndiyo alikuwa Dikteta, Ndiyo alikosea mambo mengi tu. Lakini kwanini mlimpitisha mkifahamu tabia zake fika. Kwanini hamkusubiri amalize muda wake kama ambavyo mlimvumilia CHEKI-BOBU aliyekuwa anafanya mambo ya ajabu Ikulu yenye madhara makubwa kwa nchi ???

=================================================================
Tokea mwaka 2021 yametokea muaji makubwa ya kutisha kuwahi kutokea hapa Tanzania. Hayatakuwa mwisho kwasababu mzani wa madaraka haujakaa sawa. Mbaya zaidi imefahamika kwamba MKUU WA NCHI naye anagusika vizuri na haliwezi kutokea jambo lolote lile kubwa. Historia inaonesha kwamba mara nyingi mapinduzi makubwa, huzaa mapinduzi mengine. Nchi huchukua muda mrefu mno mpaka ije kutulia:

​
  • Mwaka 1651 waingereza walipindua mfalme wao na kumnyonga ila nchi ilikuja kutulia mwaka 1688 baada ya kuanzisha utaribu mpya wa kiutawala.​
  • Mwaka 1789 wafaransa walipindu mfalme wao na miaka zaidi ya 30 nchi ilijaa damu na vita, ikaja kutulia mwaka 1814.​
  • Mwaka 1776 makoloni 13 ya Marekani yaliasi dhidi ya Mfalme, na nchi ilikuja kutulia mwaka 1815 baada ya kumaliza ugomvi na Muingereza.​
==================================================================
Hata hapa Afrika mchezo ni uleule tu:

RWANDA: walimfukuza Mfalme Kigeri ila mpaka leo kila utawala mpya umeingia kwa kumwaga damu. General Kayibanda, General Habyarimana na General Kagame, wote wameingia kwa bunduki. Ila makosa yalianza kule kwa Mfalme Kigeri.

UGANDA: walianza na kumtoa Mutesa. Akaja Obote akatolewa. Akaja Amini akatolewa. Akarudi Obote akatolewa. Sasa yuko Museveni naye akiondoka haijulikani Uganda itakuwa kwenye hali gani. Hakuna anayeweza kuvaa viatu vya Museveni.

ZIMBABWE: nako ni hivyo-hivyo tu. Mubage alitolewa akaingia Munangagwa.

NIGERIA: walau kipindi hiki wametulia na wanapokezana kimakabila na kidino

==================================================================
Tanzania na Kenya, MUNGU alitupendelea mno. Jinsi tulivyokuwa tunayaangalia madaraka (Approach Towards Leadership) mbali na madhaifu yetu mengi imakuwa ni kuvumiliana mno (Tolerance). Siyo kwamba sisi tuna kitu cha ziada kuliko wenzetu lakini tuna kiwango kikubwa cha kuvumiliana.

GHANA, South-Africa na Botswana ni mataifa ambayo yameanza kukomaa hapa Afrika linapokuja suala zima la kuvumiliana kisiasa. Sisi hapa Tanzania tunarudi miaka ya 60's kuishi maisha ambayo hatukuyaishi. Maisha ya machafuko (Political Instability). Kitakachotokea Tanzania kipindi hiki ni kwamba kiti cha Uraisi kitatingishwa mno kwa miaka mingi, hata huyu wa sasa akitoka.

Tumeshatengeneza BAD PRECEDENT, na kutulia mpaka pande zote ziumie na kupata hasara kubwa ndiyo tutarudi kuwa kawaida. Ila kwasababu NOBODY IS SAFE. Kiufupi hata uweke wanajeshi barabarani, muda wako utafika tu. Mlichokianzisha mwaka 2021 lazima mkinywee, tena mtakinywea vibaya sana.

Siasa ndivyo ilivyo, historia imejaa ushahidi wa hichi nachokisema kuanzia Rome, The Rashidun Caliphate, Mongol Empire, Tang Dynasty n.k Kumuua mfalme (Mzuri au Mbaya) na machafuko yasitokee huwa ni nadra mno.

====================================================​
HAkika hili ni andiko Bora kabisa kulisoma hapa JF tangia nilipojiunga hapa. Naamini watawala wetu kutia ndani Cheki Bob watalisoma, kulielewa na kulifanyia kazi.
 
Kaisairi hakikuwa cheo ni jina kingereza ceasar.... Rome walikuwa na emporer mtawala .. Rome iliwapata emporers wenye majina ya ceasar kama wawili hivi kama sijakosea... hope nimekusaidia next time usitumie neno kaisari kama cheo...
Upo sahihi kuwa Kaisari ni jina na siyo cheo na MALCOM LUMUMBA yupo sahihi pia kuwa Kaisari ni cheo.

Kama vile Kingunge ni cheo na ni jina pia. "Boycott " ni jina la mtu na pia ni neno linalotumika kuonesha kitendo cha kugoma.

Lugha huzaliwa hukua na Kisha hufa. Leo hii mtu akimwambia mwenzie kuwa ni "kihiyo" inaeleweka anamaanisna nini. Lakini kihiyo lilitokana na jina la Ramadhani kihiyo aliyekuwa mbunge wa Temeke.
 
Ni kweli kabisa..

Na sijui watu kama Nguruvi3, Mag3, Mzee Mwanakijiji, Doctor Mama Amon wako wapi. Hata wakija huja kwa kubipu sana wakati taifa liko kwenye hali tete. Hata kule kwenye jukwaa la Great Thinkers hawaposti chochote kwa siku nyingi sana. Mzee Nguruvi3 uko wapi rafiki? Mada zako kule GT zimetulia kwa miezi mingi bila mwendelezo

Nyie wazee waheshimiwa njooni tu hukuhuku kwenye Jukwaa la Siasa - jukwaa la vurugu mechi lililo na mchanganyiko wa kila aina ya watu wajinga, wapumbavu, wapuuzi, walevi, wanafiki na wapiga propaganda tu wa kutetea pande zao bila facts, machawa nk

Nyie njooni tu. Shusheni nondo. Kwa uzoefu wangu, machawa mara nyingi huwa irrelevant kwenye mada nyingi zilizoenda shule kama hii kwa sababu wanakuwa hawana cha kuchangia. Hata wakiweka tusi, basi linakuwa irrelevant kwa kuwa linakuwa linaelea hewani tu kupingana na ukweli halisi...!!

Asante sana ndugu MALCOM LUMUMBA kwa elimu nzuri katika makala nzuri iliyochambuliwa

1765699973902.png


Comrade Palm Beach,
Salama?

Asante kunikumbuka. Ukiona kimya jua mambo ni mengi. Lakini yote ya msingi nimekwishayasema.

Uzuri huwa sibakizi kitu kichwani. Hata wale watu wasiojulikana wakija kuniteka hawatakuta chochote kipya kichwani mwangu!

Kwa ufupi hoja yangu mpaka sasa iko hivi:

Mvutano kati ya serikali ya Rais Samia na Wakosoaji wake umefikia hatua ya "intractibility". Mgogoro uko katika hali ya mtanziko sugu, kiasi kwamba maridhiano hayawezekani tena.

Hakuna ZOPA (Zone of Possible Agreement) kabisa. Badala yake, sasa kila upande unajielekeza kwenye BATNA (Best Alternative to a Negotiated Agreement) yake.

GenZ Team wako bize na kuandaa maandamano ya kufa na kupona yasiyokoma wakati Samia Team wako bize na kutekeleza “NEW DECIDED MOPPERS policy framework.” Nitaeleza kwa ufupi.

Matukio ya tangu Machi 2021 mpaka Desemba 2025, chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan, yametufundisha mambo mengi.

Kubwa ni kwamba Samia Team wameigeuza Ikulu kuwa pango la walanguzi. Kwa ajili ya kufanikisha mradi wao huu, sasa BATNA yao ni “NEW DECIDED MOPPERS policy framework” ambapo maneno “NEW DECIDED MOPPERS" yanawakilisha sera zifuatazo:
  • Nepotic autocracy in state administration;
  • Elevation of Shariah Law over the Natural Moral Law;
  • War on Indigenous Africans in favor of Foreign Direct Investors;

  • Detentive abductions, tortures and enforced dissappearances;
  • Extrajudicial killings and extralegal operations in the name of presidential constitutional immunity against criminal charges;

  • Court capture and dramas;
  • Inquiry commissions dramas;
  • Deregistration of critical associations;
  • Election rigging in the name of INEC's constitutional immunity against criminal charges;
  • Disinformation, media adoption and mind capture;

  • Military politicization, capture and intimidation;
  • Organized violence against republican principles;
  • Parliamentary capture and dramas;
  • Police and paramilitary forces brutality;
  • Embezzlement of financial and natural resources;
  • Religious oppressions; and
  • Security forces outsourcing for domestic oppressions.
Kwa maneno mengine, Samia Team wanawatisha GenZ Team kwa kuwambia kwamba ama mnakuja kwenye maridhiano au mnakaa kimya au mkileta fyoko tunawaua. Yaani, WATNA (worst alternative to negotiated agreement) ya GenZ Team ni adhabu ya kifo.

Samia Team wanao ujasiri wa kutekeleza "New Decided Moppers policy framework" chini ya ibara ya 46 ya Katiba (1977) inayowapa leseni kufanya uhalifu wowote unaofahamuka dunia hii, ikiwemo kuua watu wasio na hatia, bila hofu ya kushitakiwa katika mahakama yoyote.

Kiburi hiki kinapanuka zaidi kwa sababu ya leseni ya kuiba uchaguzi wa Rais inayopatikana kwenye ibara ya 41(7) ya Katiba ya Tanzania (1977).

Chini ya ibara hii, hata kama Rais kapata 98% ya kura zote zilizopigwa, wakati wapiga kura ni 10% ya watu wote walioandikishwa, halafu Tume ikaamua kumtangaza yeye kwamba ndiye mshindi, tangazo hilo haliwezi kuhojiwa na mahakama yoyote nchini Tanzania.

Kwa hakika hiki ndicho kilichotokea katika uchaguzi wa mwaka huu na miaka yote iliyopita. Tuna Katiba ya hovyo sana.

Na sasa, kwa kuwa tunaye Rais anayekataa waziwazi Sheria ya Maadili Asilia, kwa sababu tu inahubiriwa zaidi na TEC, na badala yake kukumbatia maudhui ya Azimio la Kairo kuhusu Haki za Binadamu katika Uislamu, kama lilivyoazinduliwa mjini Kairo mwaka 1990, hali imekuwa mbaya zaidi.

Naongelea tamko liitwalo "The Cairo Declaration on Human Rights in Islam (1990)," linalomomonyoa haki za binadamu kwa kutumnia "Islamic shariah" likiwa linasema, kati ya mambo mengine, kwamba:

"2(a) It is the duty of individuals, societies and states to safeguard this right [to life] against any violation, and it is prohibited to take away life except for a shariah prescribed reason... 2(d) Safety from bodily harm is a guaranteed right. It is the duty of the state to safeguard it, and it is prohibited to breach it without a Shariah-prescribed reason... 12. Every man shall have the right, within the framework of the Shari'ah, to free movement... 19(d) There shall be no crime or punishment except as provided for in the Shari'ah... 22 (a) Everyone shall have the right to express his opinion freely in such manner as would not be contrary to the principles of the Shari'ah. (b) Everyone shall have the right to advocate what is right, and propagate what is good, and warn against what is wrong and evil according to the norms of Islamic Shari'ah. 23(b) Everyone shall have the right to ... assume public office in accordance with the provisions of Shari'ah. 24. All the rights and freedoms stipulated in this Declaration are subject to the Islamic Shari'ah. 25. [Islamic principles under] the Islamic Shariah is the only source of reference for the explanation or clarification of any of the articles of this Declaration."​

Azimio la Cairo kuhusu Haki za Binadamu katika Uislamu liliboreshwa na kurekebishwa mwaka wa 2020, na kusababisha Azimio jipya la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) kuhusu Haki za Binadamu. Yaani, "The Cairo Declaration of the Organization of Islamic Cooperation on Human Rights (2020)"

Azimio hili liliondoa neno "Sharia Law" kama misingi wake wa kimaadili, likilenga kuoanishwa kwa karibu na matamko ya kimataifa ya haki za binadamu, lakini likaendelea kuakisi kanuni za Kiislamu katika ibara ya 25(a).

Katika ibara hii tunasoma kuwa, "everyone has the right to exercise and enjoy the rights and freedoms set out in the present declaration, without prejudice to the principles of Islam and national legislation."

Hivyo, kwa sehemu kubwa, Tangazo la Kairo na marekebisho yake ya mwaka 2020 bado vinabatilisha, Tangazo la Dunia ya Watu Wote Kuhusu Haki za Watu Wote, kama lilivyoazinduliwa mjini Paris, mwaka 1948.

Na hapa, naongelea tamko liitwalo "The Universal Declaration on Human Rights (1948)," linalotetea haki ya kuishi kwa kusema, kati ya mambo mengine, kwamba:

"1. All human beings are born free and equal in dignity and rights ... 2. Everyone is entitled to all the rights and freedoms set forth in this Declaration, without distinction of any kind, such as race, colour, sex, language, religion, political or other opinion, national or social origin, property, birth or other status.... 3. Everyone has the right to life, liberty and security of person."​

Katika mazingira haya, kwa maoni yangu, GenZ Team hawana uwezo wa kupimana nguvu na Team Samia, na wakashinda, isipokuwa kama mojawapo kati ya mawili litatokea.

Ama GenZ Team wa uraiani waungane na GenZ Team walioko ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama. Au Ama GenZ Team wa uraiani wapate silaha thabiti za kukabiliana kimkakati na wauaji.

Ni maoni yangu kwamba, serikali inayoendesha nchi kwa kutumia “NEW DECIDED MOPPERS policy framework” inakuwa imepoteza uhalali.

Captain Tesha alitoa wito mwafaka kuhusu mtanziko huu. Yaani, wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama "kuwavusha wananchi."

Yeye aliona kuwa ili "kuwavusha wananchi" Afande CDF anapaswa kusimamia mpango wa "kuchukua nchi".

Lakini, kwa maonio yangi sio lazima Afande CDF aendeshe mpango wa "kuchukua nchi," japo hiyo ni njia mojawapo.

Kuna njia nyingi zinazoweza kutumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama "kuwavusha wananchi".

Kwa mfano, Jeshi la Zimbwabwe lilimwondoa Rais Mugabe Madarakani bila kufanya mapinduzi.

Kuhusu "mapinduzi ya kidemokrasia" ya huko Zimbabwe mwaka 2017, Meja Jenerali Moyo alisema maneno ya busara yafuatayo wakati huo:

“To both our people and the world beyond our borders, we wish to make it abundantly clear that this is not a military takeover of government.”

1765626752958.png


Katika mazingira kama haya, swali ambalo sijui jawabu lake hadi sasa ni hili hapa:

Kwa nini vyombo vya ulinzi na usalama havioni kwamba wakati wa kuwavusha wananchi, kwa kuwasadia kupita katika bonde la uvuli wa mauti, ni sasa hivi?

Ninapoongelea vyombo vya ulinzi na usalama namaanisha: wanajeshi na maofisa wa TISS na idara zake ikiwemo PSU.

Na kuhusu neno "mwanajeshi," maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumukatika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshila Kujenga Taifa.

Chini ya ibara ya 147(2) ya Katiba ya Tanzania (1977), "Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibuwa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania."

Hivi ni vyombo vya kumsaidia Rais kutawala kwa mujibu wa katiba akiwa anafanya hivyo kwa niana na kwa faida ya wananchi, na sio vinginevyo.

Hivyo, inapofika mahali Rais anabariki mauaji ya wananchi kama mbinu ya kuwalinda wageni na mali zao anakuwa amevuka mipaka ya kikatiba, na kupoteza uhalali kwa kiwango hicho.

Hivyo, napendekeza kwamba mjadala uendelee wakati tunasoma makala ya Ozan Varol (2012) yenye jina la "The Democratic coup d'état," nakala imeambatanishwa.

Kwa mujibu wa Varol (2012), mara nyingi, neno "mapinduzi ya kijeshi" linatukumbusha mapinduzi yaliyofanywa na majenerali wenye uchu wa madaraka ambao hupindua utawala uliopo, si kwa ajili ya demokrasia, bali kujilimbikizia madaraka mikononi mwao kama madikteta.

Hivyo, mara nyingo tunadhani mapinduzi yote yanaonekana sawa, yana harufu sawa, na yanawasilisha vitisho sawa kwa demokrasia.

Hili ni wazo lenye nguvu, fupi, na linalojiimarisha kihistoria. Laiki pia sio wazo sahihi mara zote, Varol (2012) anatukumbusha.

Katika Mapinduzi ya Kidemokrasia, Varol (2012) anatoa hoja rahisi, lakini yenye utata, kwamba: Wakati mwingine, demokrasia huanzishwa kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Anaimarisha hoja yake kwa kuzungumzia matukio ya Jeshi la Wanamaji la Athene mwaka wa 411 KK dhidi ya serikali ya ndani ya kidhalimu;

Anajadili mapinduzi katika makoloni ya Marekani yaliyowaondoa magavana wa Uingereza mafisadi;

Na hatimaye anagusia mapinduzi ya karne ya ishirini yaliyowaangusha madikteta na kuanzisha demokrasia katika nchi mbalimbali kama vile Guinea-Bissau, Ureno, na Kolombia.

Katika kitabu chake, kwa kuunganisha doti za matukio haya yaliyopuuzwa an watafiti, Varol (2012) anaunda simulizi yenye usawa inayopinga kila kitu tulichofikiri tunajua kuhusu mapinduzi ya kijeshi.

Kwa ufupi, Varol (2012) anasema kuwa "sometimes, a democracy is established through a Zimbabwean-type of democratic military coup."

Tuone mfano wa mapinduzi ya kidemokrasia kutoka Zimbabwe

Mwaka 2017, jeshi la Zimbabwe liliwakamata Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 na mkewe, Grace Mugabe, na kuchukua udhibiti wa mitaa ya mji mkuu na kituo kikuu cha televisheni.

Mgogoro huo ulianza kujitokeza tarehe 6 Novemba 2017 wakati Rais Mugabe alipomfukuza kazi Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa, na kumfukuza kutoka chama tawala cha ZANU-PF ili kutengeneza mazingira laini ya kumsimika mkewe Grace kama Rais mpya.

Mnangagwa alikuwa ameungana na jeshi na Chama cha Maveterani wa Vita vya Ukombozi wa Kitaifa cha Zimbabwe, na alikuwa katika mapambano makali ya madaraka katika kinyang'anyiro cha kumrithi kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 wa nchi hiyo.

Mpinzani mkuu wa Mnangagwa alikuwa Grace Mugabe, mke wa rais, ambaye aliongoza kundi pinzani la maveterani wa ZANU-PF lililojulikana kama G40, likiongoza tawi la wanawake na Grace alikuwa maarufu miongoni mwa wanaharakati vijana wa chama.

Jeshi kisha likaingilia kati bila kusita kwa kutoa taarifa ya tarehe 13 Novemba kupitia kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Zimbabwe, Jenerali Constantino Chiwenga.

Taarifa hiyo ilitaka kukomeshwa kwa uondoaji wa wabachama walioshiriki katika vita ya miaka kumi na tano ya ukombozi wa Zimbabwe kutoka kwa utawala wa wazungu, na kuonya kwamba jeshi litaingilia kati dhidi ya tishio lolote dhidi ya uadilifu wa mapinduzi yaliyosababisha uhuru wa Zimbabwe mwaka wa 1980.

Jenerali Chiwenga alisema kwamba ikiwa Mugabe hatakua hatua zinazofaa kutakuwa na uingiliaji kati wa kijeshi ili kushughulikia tishio la usalama linaloonekana katika chama tawala na nchini kwa ujumla.

Kamanda wa ZDF, Jenerali Chiwenga, alipinga kabisa madai ya kuwepo kwa mapinduzi ya kijeshi, akiziita hatua zinazochukuliwa kama "marekebisho yasiyo na umwagaji damu".

Hasa, katika matangazo ya televisheni ya jeshi alisisitiza kwamba "tunataka kuweka wazi kabisa kwamba haya sio mapinduzi ya kijeshi ya kuchukua serikali. Kinachofanywa na Jeshi la Ulinzi la Zimbabwe ni kutuliza hali inayozorota ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika nchi yetu ambayo ikiwa haitashughulikiwa sasa hivi inaweza kusababisha migogoro ya vurugu kubwa baadaye."

"Mugabe na familia yake wako salama na usalama wao umehakikishwa. Tunawalenga tu wahalifu wanaomzunguka Mugabe, hasa wanaofanya uhalifu unaosababisha mateso ya kijamii na kiuchumi nchini, ili kuwafikisha mbele ya sheria," aliendelea.

Taarifa hiyo ilizitaka taasisi, vyombo muhimu vya serikali na vyama vya kijamii kubaki makini na watulivu.

Karibu masaa 24 baadaye, msemaji wa chama cha ZANU-PF, Balozi Moyo, alimshutumu Chiwenga kwa matamshi ya uhaini na kuvuka mipaka ya mamlaka yake.

Lakini, mnamo Novemba 15, wanajeshi walichukua udhibiti wa makao makuu ya vyombo vya habari vya serikali na majengo mengine muhimu.

Jeshi liliwasihi Wazimbabwe "kupunguza harakati zisizo za lazima" na kutoa wito wa utulivu miongoni mwa idara muhimu za serikali, mahakama, bunge, sekta ya usalama, makanisa, vikundi vya vijana, viongozi wa kitamaduni na watendaji wengine wa kisiasa.

Magari ya kijeshi yalikuwa yameegeshwa mitaani, lakini hii haikuwakatisha tamaa Wazimbabwe kuendelea na maisha yao kama kawaida, wakionekana kutembea sambamba na vifaru barabarani.

1765890973964.png

Raia wa Zimbabwe wakivisindikiza vifaru mitaa mjini Hararae mwaka 2017 (CNN)​

Siku nne baada ya jeshi kuchukua hatua maalum za kijeshi, mtu ambaye jeshi lilitaka kumng'oa madarakani bado alikuwa, angalau kwa jina, bado ni Rais.

Lakini, baadaye kidogo ZANU-PF walimwondoa Mugabe kama kiongozi wa chama na kutoa amri ya mwisho: “Ama ujiuzulu ifikapo saa sita mchana Jumatatu au ukabiliwe na mashtaka ya kung'atuliwa kupitia bungeni.”

Kwa hivyo, waandishi wa habari walipoitwa Ikulu saa chache baadaye, na Mugabe akaongea nao mbashara kupitia ZBC, matarajio yote yalikuwa kwamba Mugabe hatimaye angetoa tamko la kukubaliana na majenerali kwa kujiuzulu.

Mpaka anamaliza mkutano wake na waandishi wa habari hakutoa majibu ya wazi. Hivyo, hatua za mashtaka ya kumng'oa kupitia bunge zikaanza.

Lakini, dakika chache baada ya kusikilizwa kwa mashtaka yake katika Bunge la Zimbabwe, Spika alitangaza kwamba alikuwa amepokea barua ya kujiuzulu kwake.

Barua ilikuwa na maneno 20 tu: “Nimejiuzulu ili kuruhusu uhamisho mzuri wa madaraka. Tafadhali toa taarifa kwa umma kuhusu uamuzi wangu haraka iwezekanavyo.”

Wabunge walipiga makofi na shangwe nyingi huku Spika wa bunge akisoma barua hiyo, na hatimaye kuzima suala la mapinduzi.

Mapinduzi ya Zimbabwe ya 2017 mara nyingi huelezewa na wachambuzi wa siasa kama "ya kipekee" kwa sababu kimsingi yalitofautiana na mtiririko wa kawaida wa hatua za kuchukua madaraka ya kijeshi.

Ingawa yalikuwa na sifa zote za mapinduzi, ikiwa ni pamoja na vifaru mitaani na rais aliye chini ya kizuizi cha nyumbani, jeshi lilijitahidi sana kuyaita kama mchakato wa kisheria na wa kikatiba.

Kwa ufupi, upekee wa Mapinduzi ya Zimbabwe unaweza kuelezwa kama ifuatavyo:

Tangazo la Kukataa kwamba sio Mapinduzi: Katika hotuba iliyorushwa kwenye TV mnamo 15 Novemba 2017, Meja Jenerali Moyo alisema, "Hii sio hatua ya kuipindua serikali kijeshi." Kwa hakika, ulikuwa ni mkakati wa kuepuka vikwazo vya kisiasa kutoka AU na SADC, ambayo kwa ujumla husimamisha nchi yoyote ambapo mapinduzi yanatokea.

Kukamatwa kwa Heshima Ikulu: Tofauti na mapinduzi mengi yanayoishia kifo au kukimbilia uhamishoni kwa kiongozi mkuu, Rais Robert Mugabe aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani lakini aliendelea kuwasiliana mara kwa mara na watekaji wake.

Uidhinishwaji wa Umma na Mahakama: Mapinduzi hayo yalisherehekewa sana na umma wa Zimbabwe, ambao ulifanya mikutano mikubwa mjini Harare. Zaidi ya hayo, Mahakama Kuu ya Zimbabwe baadaye iliamua kwamba uingiliaji kati wa jeshi ulikuwa wa kikatiba, ukiwa ni uthibitisho wa nadra wa kimahakama wa utekaji wa kijeshi.

Marekebisho ya Kimfumo Bila Kumwaga Damu: Jeshi liliita operesheni hiyo "Operesheni Rejesha Urithi," likiielezea kama "marekebisho bila kumwaga damu" yenye lengo la kuwaondoa "wahalifu" waliokuwa karibu na rais badala ya kumlenga rais mwenyewe.

Sababu Kuu ya mapinduzi: Kichocheo kikuu cha mapinduzi kilikuwa mapambano ya vikundi ndani ya chama tawala cha ZANU-PF kati ya makundi mawili makuu: Timu ya Lacoste na Kizazi cha G40.

Timu ya Lacoste iliongozwa na Makamu wa Rais wa zamani Emmerson Mnangagwa, ambaye aliungwa mkono na wanajeshi na maveterani wa vita.

Kizazi cha G40 kilikuwa kundi kichanga kilichoongozwa na Mke wa Rais Mugabe, Grace, ambaye alilenga kumrithi mumewe wa miaka 93.

Jeshi liliingilia kati tu baada ya Robert Mugabe kumfukuza Mnangagwa mnamo Novemba 6, 2017, na kumfungulia njia Grace Mugabe kuchukua madaraka.

Matokeo ya Muda Mrefu: Kujiuzulu kwa Robert Mugabe mnamo 21 Novemba 2017; Kuinuka kwa Mnangagwa ili kuapishwa kama rais mnamo 24 Novemba 2017; Jeshi kujijengea heshima kama chombo mahsusi cha kulinda rasilimali na umoja wa Taifa.

Hitimisho na mapendekezo

Kwa kuzingatia mifano kutoka Zimbabwe na kwingineko, wito wangu ni huu: Tanzania tutafute mbinu za kuwashika mkono GenZ ili waweze kufanikisha haya matatu kwa faida ya watu wote:
  1. Kuwapumzisha wanamtandao wanaotekeleza "new decided moppers policies" na kusimika serikali ya mpito badala yake, lakini bila kuvunja katiba ya nchi.
  2. Kupata Katiba mpya itakayofuta ibara za 46 na 41(7) katika Katiba ya sasa na kuandika upya sura ya 12 ya Katiba ya Tanzania ili kuweka bayana majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa kama inavyoonekana kwenye sura ya 12 ya Katiba ya Uganda.
  3. Na kuandaliwa kwa uchaguzi mtakatifu, kwa maana ya uchaguzi uliotakata tangu kuandikishwa kwa wapiga kura hadi kutangazwa kwa matokeo ya kura.
Vyombo vya ulinzi na usalama vinayo nafasi kubwa sana katika mchakato huu.

Nawasilisha.
 

Attachments

View attachment 3515078
Comrade Palm Beach,
Salama?

Asante kunikumbuka. Ukiona kimya jua mambo ni mengi. Lakini yote ya msingi nimekwishayasema. Uzuri huwa sibakizi kitu kichwani. Hata wale watu wasiojulikana wakija kuniteka hawatakuta chochote kipya kichwani mwangu! Kwa ufupi hoja yangu mpaka sasa iko hivi:

Mvutano kati ya serikali ya Rais Samia na Wakosoaji wake umefikia hatua ya "intractibility". Mgogoro uko katika hali ya mtanziko sugu, kiasi kwamba maridhiano hayawezekani tena.

Hakuna ZOPA (Zone of Possible Agreement) kabisa. Badala yake, sasa kila upande unajielekeza kwenye BATNA (Best Alternative to a Negotiated Agreement) yake.

Matukio ya tangu 29 Oktoba 2025 mpaka 02 Desemba 2025 yametufundisha kwamba kwa sasa, BATNA ya Samia Team ni “DECIDED MOPPERS framework” ambapo maneno “DECIDED MOPPERS" yanawakilisha sera zifuatazo:
  • Detentive abductions;
  • Extrajudicial killings and extralegal operations;
  • Court capture and dramas;
  • Inquiry commissions dramas;
  • Deregistration of critical associations;
  • Election rigging;
  • Disinformation and mind capture;

  • Media capture and intimidation;
  • Outsourcing killers;
  • Parliamentary capture and dramas;
  • Police and paramilitary forces brutality;
  • Embezzlement of financial and natural resources;
  • Religious oppressions; and
  • Security forces outsourcing for domestic oppressions.
Kwa maneno mengine, Samia Team wanawatisha GenZ Team kwa kuwambia kwamba ama mnakuja kwenye maridhiano au mnakaa kimya au mkileta fyoko tunawaua. Yaani, WATNA (worst alternative to negotiated agreement) ya GenZ Team ni adhabu ya kifo.

Katika mazingira haya, GenZ Team hawana uwezo wa kupimana nguvu na Team Samia, isipokuwa kama GenZ Team wa uraiani wataungana na GenZ Team walioko ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Ni maoni yangu kwamba, serikali inayoendesha nchi kwa kutumia “DECIDED MOPPERS framework” inakuwa imepoteza uhalali.

Captain Tesha alitoa wito mwafaka kuhusu mtanziko huu. Yaani, wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama "kuwavusha wananchi."

Yeye aliona kuwa ili "kuwavusha wananchi" Afande CDF anapaswa kusimamia mpango wa "kuchukua nchi".

Lakini, kwa maonio yangi sio lazima Afande CDF "kuchukua nchi," japo hiyo ni njia mojawapo. Kuna njia nyingi zinazoweza kutumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama "kuwavusha wananchi".

Kwa mfano, Jeshi la Zimbwabwe lilimwondoa Rais Mugabe Madarakani bila kufanya mapinduzi.

Kuhusu "coup de grace" ya Zimbabwe, Meja Jenerali Moyo alisema maneno yafuatayo wakati huo:

“To both our people and the world beyond our borders, we wish to make it abundantly clear that this is not a military takeover of government.”

View attachment 3515109


Katika mazingira kama haya, swali ambalo sijui jawabu lake hadi sasa ni hili hapa:

Kwa nini vyombo vya ulinzi na usalama havioni kwamba wakati wa kuwavusha wananchi, kwa kuwasadia kupita katika bonde la uvuli wa mauti, ni sasa hivi?

Ninapoongelea vyombo vya ulinzi na usalama namaanisha: JWTZ, Polisi, TISS na idara zake ikiwemo PSU.

Mjadala uendelee wakati tunasoma makala ya Ozan Varol (2012) yenye jina la "The Democratic coup d'état," nakala imeambatanishwa. Varol (2012) anasema kuwa "Sometimes, a democracy is established through a Zimbabwe-type democratic military coup."
Eeh, asante sana Doctor Mama Amon

Na watu kama ninyi sijui ni kwanini mko nje ya mifumo ya kiserikali kusaidia kuokoa jahazi.....

Hata hivyo, nafikiri na ninaona kuna kila dalili kuwa something very special is going to happen and perspectively change everything...

Huyu mama hawezi na hana uwezo hata wa 5% wa kiuongozi ktk level ya Urais...

Ukichanganya na ubovu/udhaifu wa mifumo ya taasisi zetu, mambo ndiyo yameharibika kabisa kwa sbb wahuni wapiga deal walio karibu naye kama washauri wake, wameacha jukumu la umma na kuangalia maslahi ya tamaa zao tu, kwa sababu ya udhaifu wa kutoelewa wa yule aliye juu yao.

Kiufupi, CCM 2015 walituletea magarasa matupu. Hata Hayati John P. Magufuli naye alikuwa ni tatizo tu. Alibebwa na spirit ya uanaume wake tu. Na udhaifu wake ule ndo anatembea nao huyu bibie na matokeo yake ni haya...

Mimi ni mzima...

Lakini nakuhakikishia jambo moja tutavuka salama japo wengi wataumia sana na wengine kupoteza maisha kabisa....!
 
View attachment 3515078
Comrade Palm Beach,
Salama?

Asante kunikumbuka. Ukiona kimya jua mambo ni mengi. Lakini yote ya msingi nimekwishayasema. Uzuri huwa sibakizi kitu kichwani. Hata wale watu wasiojulikana wakija kuniteka hawatakuta chochote kipya kichwani mwangu! Kwa ufupi hoja yangu mpaka sasa iko hivi:

Mvutano kati ya serikali ya Rais Samia na Wakosoaji wake umefikia hatua ya "intractibility". Mgogoro uko katika hali ya mtanziko sugu, kiasi kwamba maridhiano hayawezekani tena.

Hakuna ZOPA (Zone of Possible Agreement) kabisa. Badala yake, sasa kila upande unajielekeza kwenye BATNA (Best Alternative to a Negotiated Agreement) yake.

Matukio ya tangu 29 Oktoba 2025 mpaka 02 Desemba 2025 yametufundisha kwamba kwa sasa, BATNA ya Samia Team ni “DECIDED MOPPERS framework” ambapo maneno “DECIDED MOPPERS" yanawakilisha sera zifuatazo:
  • Detentive abductions;
  • Extrajudicial killings and extralegal operations;
  • Court capture and dramas;
  • Inquiry commissions dramas;
  • Deregistration of critical associations;
  • Election rigging;
  • Disinformation and mind capture;

  • Media capture and intimidation;
  • Outsourcing killers;
  • Parliamentary capture and dramas;
  • Police and paramilitary forces brutality;
  • Embezzlement of financial and natural resources;
  • Religious oppressions; and
  • Security forces outsourcing for domestic oppressions.
Kwa maneno mengine, Samia Team wanawatisha GenZ Team kwa kuwambia kwamba ama mnakuja kwenye maridhiano au mnakaa kimya au mkileta fyoko tunawaua. Yaani, WATNA (worst alternative to negotiated agreement) ya GenZ Team ni adhabu ya kifo.

Katika mazingira haya, GenZ Team hawana uwezo wa kupimana nguvu na Team Samia, isipokuwa kama GenZ Team wa uraiani wataungana na GenZ Team walioko ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Ni maoni yangu kwamba, serikali inayoendesha nchi kwa kutumia “DECIDED MOPPERS framework” inakuwa imepoteza uhalali.

Captain Tesha alitoa wito mwafaka kuhusu mtanziko huu. Yaani, wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama "kuwavusha wananchi."

Yeye aliona kuwa ili "kuwavusha wananchi" Afande CDF anapaswa kusimamia mpango wa "kuchukua nchi".

Lakini, kwa maonio yangi sio lazima Afande CDF "kuchukua nchi," japo hiyo ni njia mojawapo. Kuna njia nyingi zinazoweza kutumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama "kuwavusha wananchi".

Kwa mfano, Jeshi la Zimbwabwe lilimwondoa Rais Mugabe Madarakani bila kufanya mapinduzi.

Kuhusu "coup de grace" ya Zimbabwe, Meja Jenerali Moyo alisema maneno yafuatayo wakati huo:

“To both our people and the world beyond our borders, we wish to make it abundantly clear that this is not a military takeover of government.”

View attachment 3515109


Katika mazingira kama haya, swali ambalo sijui jawabu lake hadi sasa ni hili hapa:

Kwa nini vyombo vya ulinzi na usalama havioni kwamba wakati wa kuwavusha wananchi, kwa kuwasadia kupita katika bonde la uvuli wa mauti, ni sasa hivi?

Ninapoongelea vyombo vya ulinzi na usalama namaanisha: JWTZ, Polisi, TISS na idara zake ikiwemo PSU.

Mjadala uendelee wakati tunasoma makala ya Ozan Varol (2012) yenye jina la "The Democratic coup d'état," nakala imeambatanishwa.

Varol (2012) anasema kuwa "Sometimes, a democracy is established through a Zimbabwe-type democratic military coup."

Kwa mujibu wa Varol (2012), mara nyingi, neno "mapinduzi ya kijeshi" linatukumbusha mapinduzi yaliyofanywa na majenerali wenye uchu wa madaraka ambao hupindua utawala uliopo, si kwa ajili ya demokrasia, bali kujilimbikizia madaraka mikononi mwao kama madikteta.

Hivyo, mara nyingo tunadhani mapinduzi yote yanaonekana sawa, yana harufu sawa, na yanawasilisha vitisho sawa kwa demokrasia.

Hili ni wazo lenye nguvu, fupi, na linalojiimarisha kihistoria. Laiki pia sio wazo sahihi mara zote, Varol (2012) anatukumbusha.

Katika Mapinduzi ya Kidemokrasia, Varol (2012) anatoa hoja rahisi, lakini yenye utata, kwamba: Wakati mwingine, demokrasia huanzishwa kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Anaimarisha hoja yake kwa kuzungumzia matukio ya Jeshi la Wanamaji la Athene mwaka wa 411 KK dhidi ya serikali ya ndani ya kidhalimu;

Anajadili mapinduzi katika makoloni ya Marekani yaliyowaondoa magavana wa Uingereza mafisadi;

Na hatimaye anagusia mapinduzi ya karne ya ishirini yaliyowaangusha madikteta na kuanzisha demokrasia katika nchi mbalimbali kama vile Guinea-Bissau, Ureno, na Kolombia.

Katika kitabu chake, kwa kuunganisha nukta kati ya matukio haya yaliyopuuzwa an watafiti, Varol (2012) anaunda simulizi yenye usawa inayopinga kila kitu tulichofikiri tunajua kuhusu mapinduzi ya kijeshi.
Duuh skuwa nakujua hadi nimeangalia profile, kumbe umejiunga wakati G-Z wanaanza kumiliki simu.

Umetema nondo balaa, sjui huyu mkongwe barafu kapotelewa wapi.
 

Nimerudia tena kusoma nikiwa nimetulia, kuna vitu umeviandika in a simple way but but but…… napata kigugumiz

Mkuu umedokeza maneno machache sana, lakin….. lakini…. lakini…….


Mwamba MALCOM LUMUMBA kwenye moja ya thread zake za hivi karibuni anasema Tanzania tuliona na kuiishi na kuizoea HAIPO TENA!
Katika mazingira haya, GenZ Team hawana uwezo wa kupimana nguvu na Team Samia, isipokuwa kama GenZ Team wa uraiani wataungana na GenZ Team walioko ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama

  • Detentive abductions;
  • Extrajudicial killings and extralegal operations;
  • Court capture and dramas;
  • Inquiry commissions dramas;
  • Deregistration of critical associations;
  • Election rigging;
  • Disinformation and mind capture;

  • Media capture and intimidation;
  • Outsourcing killers;
  • Parliamentary capture and dramas;
  • Police and paramilitary forces brutality;
  • Embezzlement of financial and natural resources;
  • Religious oppressions; and
  • Security forces outsourcing for domestic oppressions.
Niwe tu muwazi, skujua kama kuna hii framwork. And % imefit na regime iliyopo. Nimeongeza kitu kwenye ubongo but matafakuri ni mengi mno!
 
hope I'm wrong, lakini Tanzania yetu is headed for a very bigger crisis. Mbaya zaidi ni kwamba baadaya Mzee Mkapa kufariki nchi imekuwa haina BABA MLEZI ambaye anaweza kusema au kukemea kitu na watu wote wakaacha na kuogopa.
Kazi kweli kweli...
 
Kwa nini vyombo vya ulinzi na usalama havioni kwamba wakati wa kuwavusha wananchi, kwa kuwasadia kupita katika bonde la uvuli wa mauti, ni sasa hivi?

Ninapoongelea vyombo vya ulinzi na usalama namaanisha: JWTZ, Polisi, TISS na idara zake ikiwemo PSU.
Hivyo ni vyombo vya kumsaidia Rais kutawala...simple answer
 
Back
Top Bottom