Ninapoongelea vyombo vya ulinzi na usalama namaanisha: wanajeshi na maofisa wa TISS na idara zake ikiwemo PSU.
Na kuhusu neno "mwanajeshi," maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshila Kujenga Taifa.
Chini ya ibara ya 147(2) ya Katiba ya Tanzania (1977), "Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania."
Hivi ni vyombo vya kumsaidia Rais kutawala kwa mujibu wa katiba akiwa anafanya hivyo kwa niaba na kwa faida ya wananchi wote, na sio vinginevyo. Hivyo, inapofika mahali Rais anabariki mauaji ya wananchi kama mbinu ya kuwalinda wageni na mali zao anakuwa amevuka mipaka ya kikatiba, na kupoteza uhalali kwa kiwango hicho.