Mfalme ‘akiuawa’ huwa inachukua muda mrefu sana Taifa kupona

Mfalme ‘akiuawa’ huwa inachukua muda mrefu sana Taifa kupona

Hivyo ni vyombo vya kumsaidia Rais kutawala...simple answer

Ninapoongelea vyombo vya ulinzi na usalama namaanisha: wanajeshi na maofisa wa TISS na idara zake ikiwemo PSU.

Na kuhusu neno "mwanajeshi," maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshila Kujenga Taifa.

Chini ya ibara ya 147(2) ya Katiba ya Tanzania (1977), "Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania."

Hivi ni vyombo vya kumsaidia Rais kutawala kwa mujibu wa katiba akiwa anafanya hivyo kwa niaba na kwa faida ya wananchi wote, na sio vinginevyo. Hivyo, inapofika mahali Rais anabariki mauaji ya wananchi kama mbinu ya kuwalinda wageni na mali zao anakuwa amevuka mipaka ya kikatiba, na kupoteza uhalali kwa kiwango hicho.
 
Mkapa alimkemea Cheki-Bobu na Mtandao mwaka 2015 kuhusu kumuweka Membe unadhani angeshindwa kukemea ujinga wa SSH ??? Mkapa alisema kabisa wakate Lowassa na wakamkata na akatia mkwara kama mtu hataki atoke na wote wakakinywea. Binafsi naamini kabisa Mzee Mkapa angekuwepo hai wakati wa kifo cha JPM 2021, siasa za Tanzania zingekuwa za tofauti sana sanaa.

Ushawishi wa Mzee Mkapa ulikuwa ni mkubwa sana hapa nchini na huko nje. Kukupasha tu, hata kipindi kile Kagame na Jakaya wanaparurana, Mzee Mkapa alisafiri kwenda Kigali, Membe akalalamika kwamba lazima aambiwe wamezungumza nini, ila mambo yakatulia vizuri na uhasama ukafa. Kiufupi kifo cha Mkapa hakina tofauti na The Dismissal Chancellor Otto Von Bismarck. (If you know you know)
​
Kifo cha mkapa ndo chanzo cha matatizo yote mpaka Magufuli kuondoka mpaka October 29 chanzo ni kifo cha Mkapa huyu mzee alikua na mapungufu stil alikua na uzalendo
 
Mkapa ndo anaye takiwa kulaumiwa kwa kupindua meza 2015 mwisho wa siku akatuletea Jpm ambaye alikuwa mshamba wa siasa.
Uelekeo wa siasa za tz ulianza kubadilika baada ya magufuri kuingia madarakani.
(1)Alizima bunge lisioneshwe live.
(2)Akazuia vyama vya siasa kufanya mikutano.
(3)Akaanzisha utamaduni wa kuteka na kuuwa wakosoaji wa serikali.
(4)akanzusha utamaduni wakuhonga wanasiasa wa upinzani ili wahamie ccm.
(5)Akaanzisha utamaduni wa kupitisha wagombea wa ccm bila kupingwa huku wapinzani wakikatwa.
Yaani tuseme kiufupi jpm alikuja kuvuruga mambo mengi sana ambayo watangulizi wake waliyajenga kwa damu.
Kiufupi kila kinacho endelea sasa mzizi mkuu ni siasa za magufuri.
Na mbaya zaidi watu wenye akili walisema sana kuwa haya mambo aliyo yaasisi magufuri yataligharimu taifa kwa miaka mingi hata baada ya yeye kufa mkaishia kuwaita vyeti feki sijui mafisadi.
Magufuli kuhusu upinzani alikua sawa wapinzani walikua matapeli ulitaka afanye nini matapeli kama Mbowe?
 
Kifo cha mkapa ndo chanzo cha matatizo yote mpaka Magufuli kuondoka mpaka October 29 chanzo ni kifo cha Mkapa huyu mzee alikua na mapungufu stil alikua na uzalendo
Crisis 1.png

Crisis 2.png
Crisis 3.png

 
Tumeshatengeneza BAD PRECEDENT, na kutulia mpaka pande zote ziumie na kupata hasara kubwa ndiyo tutarudi kuwa kawaida. Ila kwasababu NOBODY IS SAFE. Kiufupi hata uweke wanajeshi barabarani, muda wako utafika tu. Mlichokianzisha mwaka 2021 lazima mkinywee, tena mtakinywea vibaya sana.
====================================================​
 
When goes around comes around walichomfanyia Magufuli na suala la October wanaosema tutasahau ni watu wapumbavu sana
Katika siasa, mifumo na watu wanaokuwa na nguvu kubwa leo, kesho wanaweza kujikuta upande wa pili wa sarafu. Historia inaonyesha kuwa pale ambapo misingi ya haki na utaratibu wa kisheria inapovunjwa au kuchezewa ili kukandamiza upande mmoja, mara nyingi mfumo huo huo unakuja kuwageuka walio uasisi pale upepo wa kisiasa unapobadilika.
 
Kwanza aliondoka Nkrumah kwa hila na vurugu.

Lakini baadaye Afrifa, Akuffo na Acheampong wakaondoka kwa pamoja kinyama!

Wao walidhani kuwa mambo yameisha hivi, lakini lbahati mbaya lilikuwa ni suala la muda tu!
​
Tz tunae Jk mwanadiplomasia na msuluishi wa migogoro ndani na nje ya nchi, hopeful hayo ya akina nkrumah hayawezi kutukuta.
 
Back
Top Bottom