Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Ukija nitamalizia
Na impact zake zilikuaje!
Na jinsi ilivyokuwa mgawanyiko!
Kumbuka Hawa nephilism kuna wengine walikimbia Dunia! Wakaenda mbali!
Ndiyo baadhi tuna waita so called UFO's !
Mkuu hawa nephilism waliokimbia dunia wana uhusiano wowote na annunnaki?
 
kiongoz sasa tukienda kwa kubuni tu kuwa wana wa Mungu ndio malaika hapo tutakua tunapotosha

MAANA YA WANA WA MUNGU NA WANA WA WANADAMU
1. WANA WA MUNGU:
a. WANAOITWA WANA WA MUNGU KWA JINSI YA KIMWILI - ni wa uzao wa Adamu kupitia Sethi, walikuwa wa kwanza kuliitia Jina la BWANA. Mwanzo 4:25 Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. 26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la BWANA.
b. WANAOITWA WANA WA MUNGU KWA JINSI YA KIROHO – Ni wa uzao wa Mungu kwa kwa BWANA YESU KRISTO kupitia ya Roho Mtakatifu; yaani ni wale waliozaliwa mara ya pili kiroho. Yohana 1:9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. 10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. 11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. 12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Yohana 3:3 YESU akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 YESU akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. Warumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. 15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. 1Yohana 3:1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.

2. JE, MALAIKA NI WANA WA MUNGU?
Tunasoma hivi, katika Waebrania 1:5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana? 6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu. 7 Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto. 8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. ... 13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? 14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Hivyo hapa tunapata jibu ya kwamba: MALAIKA NI WA TUMISHI TU, ILA WATU HUWAITA WANA WA MIUNGU, kutokana na imani za kale kuhusu uwepo wa miungu mingi ya kipagani, kama ile ya Babeli au hasa ile masimulizi ya kigiriki. Kwa mfano katika Danieli 3: 23 Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. 24 Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. 25 Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.

3. WANA WA WANADAMU
a. WANA WA WANADAMU WA UZAO WA ADAMU KUPITIA KAINI. Mwanzo 4: 16 Kaini akatoka mbele za uso wa BWANA, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni. 17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe. 18 Henoko akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli akamzaa Lameki. 19 Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila. 20 Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama. 21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi. 22 Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa Naama. 23 Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;
b. WANA WA WANADAMU WA MCHANGANYIKO (Yaani, Machotara au Haibridi)- ni wa uzao wa WANA WA MUNGU AMBAO HAWAKUPANDIKIZWA NGUVU YA UZAO WA MAJITU na wa WANA WA WANADAMU WALIOPANDIKIZWA NGUVU YA UZAO WA MAJITU NDANI YAKE (Hakuna jipya chini ya mbingu! - yaani malaika waovu(mapepo?) yaliwekea baadhi wanaume wa wana wa wanadamu vinasaba (genes, engelic genes; kama wafanyavyo mafundi wa genetical engeneering-ili kuzalisha miili tu iliyo hai(pia wanefili=mijusi, ile iitwayo dinosaurs) kama WANYAMA MWENYE au MIJUSI (DINOSAURS?) YENYE UMBILE LA KIBINADAMU, ambayo kwa macho tunamuona kama ni mwanadamu/mtu-kumbe sivyo, bali NI MIILI AMBAYO HAINA ROHO YA MWANADAMU NDANI YAKE! Ilikuwa ni majitu yanayobaka(na siyo malaika toka mbinguni kama wengine wasemavyo), tena yanatafuna watu kama wanyama wafanyavyo, sehemu nyingine katika biblia yaliitwa majitu kama simba(2Sam.23:20; 1Nya.11:22); ni majitu ambayo hayawezi kamwe kuupokea wokovu wala kuwa na hamu ya kuokoka, kwani si binadamu kabisa! Ni majitu yaliyowafundisha hata wanadamu tabia za kuwaza na kukusudia mabaya tu moyoni siku zote, kiasi kwamba hata yakasababisha Mungu ajute kwa nini amemfanya binadamu, na kuamua atamfutilia mbali asiwepo tena juu ya uso wa nchi, na kupunguziwa umri wa kuishi. Ndiyo maana Mungu aliyafuta makabila na mataifa ya majitu hayo kutoka katika uso wa dunia yasiwepo tena kabisa, kwa kupitia gharika ya Nuhu na vita vya wana wa Israeli – waliambiwa wasiyaache majitu hayo kuishi! Swali, ni kuhusu-artificial insemination? test tube baby? Je, Mungu hutia roho ya mwanadamu anayetengenezwa kwa njia hiyo? Au ndiyo kutengeneza Majitu ambayo Mungu ameyakataa?
Mwanzo 6:1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mnyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 4 NAO WANEFILI WALIKUWAKO DUNIANI SIKU ZILE; tena,baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.

•••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••

JE, NI KWELI KWAMBA MALAIKA WALIZAA NA WANADAMU?
Hapana! Biblia haisemi hivyo! Ila ni mawazo na maelezo ya watu kutokana na kuitafsiri vibaya mistari katika kitabu cha Mwanzo 6:1-4.
Hapa haina maana kwamba malaika toka mbinguni walifanya tendo la ndoa(uzinzi) na mabinti za wanadamu, (BIBLIA HAISEMI KAMA MALAIKA NDIO WALIOZINI NA BINTI ZA WANADAMU, ILA INASEMA KWAMBA SIKU ZILE WALIKUWEPO WANEFILI AMBAO NI MAJITU SI WANADAMU WA KAWAIDA); bali ni kutokana na mchanganyiko wa kuoana kwa wanadamu wa uzao wa Sethi(WANA WA MUNGU AMBAO HAWAKUPANDIKIZWA NGUVU YA UZAO WA MAJITU) na uzao wa wanadamu (WANA WA WANADAMU WALIOPANDIKIZWA NGUVU YA UZAO WA MAJITU NDANI YAKE); ndipo “wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.” (AMBAO KIMAUMBILE WALIFANANA NA WANEFILI Latin siyo w

zitto junior soma kuanzia kwenye vinukta
Mkuu toka mwanzo nimeshasema mwanzo 6 ni watoto wa seth na cain hakuna mahala nimesema ni uzao wa malaika na wanadamu hiyo hoja ipo nje ya biblia sio ndani ya biblia

Ila mimi nauliza nje ya mwanzo 6 je malaika hawezi mzalisha mwanadamu?? Nmeuliza tu kma Roho mtakatifu alivyoweza kuweka roho ya Yesu kwenye tumbo la maria bila maria kulala na mwanaume je haiwezekani pia wakatunga mimba kwa wanadamu wengine hata bila ya ngono if at all hoja yako ni kuwa malaika hawana jinsia

Kama ni ngono nmeshahoji kma wale malaika waliomtembelea abraham na lotu waliweza kufanya kila kitu alichofanya mwanadamu maana walivaa mwili wakibinadam je hawawezi weza kulala na mwanamke kma wangeamua?? Na wangeweza ina maana malaika anaweza kufanya ngono si ndio maana yake??

Embu tuanzie hapo kwanza tuachane na mwanzo 6 maana nlishaeleza hapo juu kuwa WANA WA MUNGU ina maana tofauti kwenye kila kitabu hivyo tukijengea hoja hapo tutakesha humu maana zaburi daniel na Ayubu vinawataja wana wa Mungu ni viumbe vya mbinguni sio hapa
 
Fafanua annunaki kwa faida ya wengine
Hawa annunaski niliwasikia kwa mara ya kwanza kuwa walikujaga miaka mingi sana hapa duniani
huwa wanakuja na sayari yao na kuondoka kwa kila baada ya kipindi fulani.. Mara ya mwisho walikuja enzi za kina nuhu au babeli kama sijakosea
Hivi karibuni ilizushwa kuwa ile sayari ya nibiru ndio wao na wanasemekana wapo karibuni kuja tena duniani
Na ni viumbe ambao wapo advanced saana
 
Nishaelezea hapo juu kiongozi!
But ndiyo hao ambao waligawanyika!
Kumbuka kabla ya mafuriko kuna wengine walikimbia Dunia Na kuanzisha maisha yao huko mbali ya Dunia!
Waleee baadhi ya waliobaki waliangamizwa Na mafuriko!
Dunia Ina mengi ya kujifunza kiongozi!
 
Zitto junior Nakuthibitishia Malaika hawezi kuzaa na mtu na mbinu aliyoitumia Mungu kumleta Yesu Malaika haiwezi. Maana Mungu alitoa nafsi moja ambayo ndiyo yesu ili malaika afanye hivo ajiingize mwenyewe. sasa ataweza??
Ni kweli mkuu hakuna ushahidi wa malaika kuweza kuzaa na binadamu ila nlichouliza hakuna possibility?? Maana nmeshuhudia watu wakiingiliwa na maroho usiku na akiamka asbuhi anakuta katumika je ina maana hizo roho zina jinsia??

Kingine nachouliza mkuu maana nipo hapa kujifunza pia..... Je kma Nafsi moja ya Yesu ndio iliowekwa kwenye tumbo la bikira maria je kiongozi wa malaika walioasi Zammuzamim,azazel na semyaza je na huenda nao walipandikiza nafsi ya roho flani ndani ya vizazi vya wanawake kama alivyofanya Roho mtakatifu kwa bikira maria??

Embu nisaidie hapo
 
Hebu zitto sema utata wako upo wapi
Atlest tutoane tongotongo
 
Hawa wanefili ni matokeo ya malaika kuzaa na binadamu na inasemekana waliangamia na hawapo tena
Kwanini hawa malaika waliozaa na binadamu huwa hawashuki tena duniani na kuja kuzaa na mabinti wengine baada ya gharika hadi mpaka sasa?
Nini kimewazuia
Hakuna mahali wamesema Malaika walizaa na wanadamu ila wana wa Mungu walizaa na wanadamu tofautisha hapo
 
Nishaelezea hapo juu kiongozi!
But ndiyo hao ambao waligawanyika!
Kumbuka kabla ya mafuriko kuna wengine walikimbia Dunia Na kuanzisha maisha yao huko mbali ya Dunia!
Waleee baadhi ya waliobaki waliangamizwa Na mafuriko!
Dunia Ina mengi ya kujifunza kiongozi!
Leo ndio nmeamini mkuu kuna mengi sana unafahamu ila unaficha..... Unajua nmekuwa nikijiuliza hao viumbe wa nje walitoka wapi na nkilinganisha mambo makubwa yaliyofanywa wakati ule ilihali teknolojia ilikuwa hamna mfano ujenzi wa pyramid na mnara wa babeli naweza kubaliana na ww kwamba huenda baadhi ya ''kizazi cha nyoka'' walikimbilia sayari zingine kuepuka gharika na ndio hawa aliens wa leo!!!

Hata kuna michoro ya alien spaceships kwenye mapango kuanzia mexico mpaka japan hadi iraq inayoonyesha uwepo wa aliens takriban miaka 10,000 iliopita?? Je huenda nao ni wanefili mkuu??
 
Hebu zitto sema utata wako upo wapi
Atlest tutoane tongotongo
Hapana mie nakubali kuwa WANA WA MUNGU ni malaika kwenye baadhi ya mistari ya biblia lakini vilevile inamaanisha WANADAMU kwenye mistari mingine ya biblia sijui inakaa vzuri hii maana ukisoma daniel 23 na 28 biblia iko wazi kabisa inataja neno MALAIKA kwenye nafasi ya WANA WA MIUNGU hivo ikimaanisha wana wa Mungu ni malaika kuendana na kitabu cha daniel ila wakuu wengine kina mitale na midimu wanajengea hoja kupitia mistari mingine mingi tu inayoonyesha WANA WA MUNGU ni wale wanaomcha Mungu na kufanya mapenzi yake

So nikatoa conclusion kuwa kila mahala Wana wa Mungu inapotajwa tuangalie muktadha na sio JINA maana naamini kila mwandishi aliandika kwa muktadha tofauti ila all in all kwa mistari kadhaa ya biblia upo sahihi tu kuwa wana wa Mungu ni MALAIKA
 
Leo ndio nmeamini mkuu kuna mengi sana unafahamu ila unaficha..... Unajua nmekuwa nikijiuliza hao viumbe wa nje walitoka wapi na nkilinganisha mambo makubwa yaliyofanywa wakati ule ilihali teknolojia ilikuwa hamna mfano ujenzi wa pyramid na mnara wa babeli naweza kubaliana na ww kwamba huenda baadhi ya ''kizazi cha nyoka'' walikimbilia sayari zingine kuepuka gharika na ndio hawa aliens wa leo!!!

Hata kuna michoro ya alien spaceships kwenye mapango kuanzia mexico mpaka japan hadi iraq inayoonyesha uwepo wa aliens takriban miaka 10,000 iliopita?? Je huenda nao ni wanefili mkuu??
Mkuu!
Kile kizazi kilisambaa Na kikaonekana kitakuja kuwa na madhara mkubwa ndiyo maana SUPER NATURAL ikaamua kukiangamiza!.
Kama unakumbuka Mungu alisema roho yake haitashindana Na kiumbe! Ikamladhimu life span apunguze!.
Pia KUHUSU mengineyo ya Hawa viumbe!.nitakuwa naelezea kwa mafumbo.!
 
Ni kweli mkuu hakuna ushahidi wa malaika kuweza kuzaa na binadamu ila nlichouliza hakuna possibility?? Maana nmeshuhudia watu wakiingiliwa na maroho usiku na akiamka asbuhi anakuta katumika je ina maana hizo roho zina jinsia??

Kingine nachouliza mkuu maana nipo hapa kujifunza pia..... Je kma Nafsi moja ya Yesu ndio iliowekwa kwenye tumbo la bikira maria je kiongozi wa malaika walioasi Zammuzamim,azazel na semyaza je na huenda nao walipandikiza nafsi ya roho flani ndani ya vizazi vya wanawake kama alivyofanya Roho mtakatifu kwa bikira maria??

Embu nisaidie hapo
Malaika walioasi walikuwa ni theluthi moja. Sijui kinachomutatiza ni wing wao au nini. Malaika hwajawahi kuzaana yaani wangeweza hii dunia isingekalika Wanefili ni Kizazi cha Kaini na wana wa Mungu ni kile kizazi cha Sethi na ndugu zake waliomkiri na kufata maagizo ya Mungu, Kumbuka Kaini Aliasi kwa kumuoa pacha wake. fatilia hata leo mapacha wa jinsia tofauti hawachezagi kibaba baba na kimama mama, maana ni kosa tangu Mwanzo. Ukifanya hivo lazima kitokee kizazi cha ajabu aidha walemavu au wadhaifu sana kwa sasa lakini. ila kipindi hicho walipofanya hivo kilitokea kizazi cha ajabu nadhani au niseme tu ndio wanefili sasa, nao walitokea katka kizazi cha kaini wana wa binadamu walitokea kizazi cha Wadogo zake Sethi na wana wa Mungu ndiyo kizazi cha Sethi maana hawa ndio wanatajwa hadi uzao wa Nuhu.
 
Hapana mie nakubali kuwa WANA WA MUNGU ni malaika kwenye baadhi ya mistari ya biblia lakini vilevile inamaanisha WANADAMU kwenye mistari mingine ya biblia sijui inakaa vzuri hii maana ukisoma daniel 23 na 28 biblia iko wazi kabisa inataja neno MALAIKA kwenye nafasi ya WANA WA MIUNGU hivo ikimaanisha wana wa Mungu ni malaika kuendana na kitabu cha daniel ila wakuu wengine kina mitale na midimu wanajengea hoja kupitia mistari mingine mingi tu inayoonyesha WANA WA MUNGU ni wale wanaomcha Mungu na kufanya mapenzi yake

So nikatoa conclusion kuwa kila mahala Wana wa Mungu inapotajwa tuangalie muktadha na sio JINA maana naamini kila mwandishi aliandika kwa muktadha tofauti ila all in all kwa mistari kadhaa ya biblia upo sahihi tu kuwa wana wa Mungu ni MALAIKA
Sahihi
Lakin kumbuka biblia imeandikwa kwa mtindo wa mafumbo Na code maalumu!.
 
Wana wa mungu ni wa kina nani hao?
Narudia Tena wana wa Mungu ni kizazi cha Sethi wana wa binadamu ni kizazi cha ndugu wa Sethi na wanefili ni kizazi cha Kaini.

Wengine wanajua kabisa Adam alipata kuzaa watoto 40 mara 20 kila uzao pacha ni dume na jike.

Hata ugomvi wa kaini na Abili ilikuwa mke Abili alitaka kumuoa pacha wa kaini kaini akamwambia muoe dadako dadangu mzuri hivi, wakwako mbaya kila mtu aoe dada yake. na hapo ndio wakamwambia Adam, Adam akasema Abili uko sahihi kaini akahisi haki haijatendeka, Adam akasema basi tumuulize Mungu wakaomba wakanuia wakaweka sadaka kila mtu alitwaa katika kazi yake mfugaji aliweka mnyama na Mkulima aliweka mazao, Kwa kuwa Abili alikuwa sahihi Mungu akaitwaa sadaka Ya Abili utata ukaisha lakin kwa kuwa kaini hakuridhika na alichukia ndipo shetani akamjaza hasira na kumpa mbinu za kumuua ndugu yake kabla hajamuoa dadake, Kaini akatimiza Lengo la Shetani. Abili akafa ndipo Mungu akahamishia Baraka kwa Uzao uliofata yaan Sethi. sijui niongeze nini.
 
Eti Kipanga Boy Vipi mbona kila nikiandia Uzi zangu za Mahaba huwa hazionekani? Au nimetengwa kama Father Dr. Alex Malasusa na JF??
 
Back
Top Bottom