Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Sasa mkuu kama ni uzao wa binadamu kwa nini wao wakatenganishwa jina lao wakaitwa Nephil na wassitwe binadamu yaani mi nataka nijue asili yao hawa viumbe walitokana na nini?
"... hao ndio walikuwa watu hodari wenye sifa"
bibilia inawaita ni watu, hivyo sidhani kama hilo jina ni kikwazo au linawaondoa katika utu wao.
 
Hapana mie nakubali kuwa WANA WA MUNGU ni malaika kwenye baadhi ya mistari ya biblia lakini vilevile inamaanisha WANADAMU kwenye mistari mingine ya biblia sijui inakaa vzuri hii maana ukisoma daniel 23 na 28 biblia iko wazi kabisa inataja neno MALAIKA kwenye nafasi ya WANA WA MIUNGU hivo ikimaanisha wana wa Mungu ni malaika kuendana na kitabu cha daniel ila wakuu wengine kina mitale na midimu wanajengea hoja kupitia mistari mingine mingi tu inayoonyesha WANA WA MUNGU ni wale wanaomcha Mungu na kufanya mapenzi yake

So nikatoa conclusion kuwa kila mahala Wana wa Mungu inapotajwa tuangalie muktadha na sio JINA maana naamini kila mwandishi aliandika kwa muktadha tofauti ila all in all kwa mistari kadhaa ya biblia upo sahihi tu kuwa wana wa Mungu ni MALAIKA
mkuu, wana wa Mungu ambao wanachukua hadhi flani ya malaika angalau ni wale wa kwenye kitabu cha ayubu ambao shetani alijihudhulishaamoja nae.
lkn pia panaacha vimaswali kidogo, kwa nini malaika wajihudhulishe mbele ya Mungu wakati yuko nao kila siku huko. CC Isaya 6.

Kuhusu Nebukadneza.
Alianza kwa kusema "Naona watu wanne"
Kisha akasema " mmoja wao ni mfano wa mwana wa Miungu"
Kisha akasema " Mungu katuma malaika kuja kuwaokoa"
Nebukadneza alikuwa mpagani, mwenye uelewa finyu wa mambo ya Mungunwa waebrania.
utajiuliza alijuaje kuwa yule ni mwana wa Miungu? lakini kwa nini aone watu wa nne, badala ya watatu na malaika mmoja.
Sisi tunayemjifunza Yesu, Tunaamini huyo alikuwa ni Yesu. Na yawezekana kwa kukaa na wale madogo nebukadneza alikuwa na mwangwi wa uelewa wa uwepo wa mwana wa Mungu (Mwana katika GodHead). Ndio maana yesu aliwashangaa mafarisayo kwa nini wanasoma maandiko hayo likiwemo na hilo lakini hawaelewi?

uelewa mdogo wa nebukadneza sidhani kama ni sahihi kuutumia kama kigezo ha kuhalalisha uwana wa malaika.

maoni mkuu.
 
Mkuu mwana wa Mungu inatafsiri tofauti kwa kila kifungu inapotajwa sasa kwa muktadha wa job na zaburi na daniel wana wa Mungu ni MALAIKA

Ila kwa mwanzo kwa uelewa wangu wana wa Mungu pale ni wana wa seth sababu ndio waliokuwa wasafi ila wanadamu ni uzao wa cain (kizazi cha nyoka) ila bado kuna wanaoweza kujengea hoja kuwa wana wa Mungu wanaotajwa kwenye zaburi kuwa walishangilia pamoja na nyota ya asbuhi siku dunia inaumbwa ndio hao hao wanaotajwa na mwanzo 6:4 hivyo hii mistari bado ni mjadala unless tuseme wana wa Mungu kwa kila kitabu ina maana tofauti ila tukizifungamanisha basi ndio inazaa mjadala kma hivi kuwa ipi ni ipi nachoona muhim tuangalie muktadha wa kitabu husika na tusifungamanishe kuwa definition ya mwana wa Mungu ni moja kwa biblia nzima nafkiri hii itasaidia kupunguza mkanganyiko huo

Cc impongo Mchawi Mkuu mitale na midimu
umeandika points mkuu nakubaliana na wewe.
Yesu anaitwa Mwana wa Mungu.
Wana wa Israel pia wanaitwa wana wa Mungu. Yeremia 31:20, 1 nyakati 22:10
Mimi na wewe kama tunauamini wokovu katika Yesu tunafahamika mbinguni kama wana wa Mungu. Warumi 8:16, Yohana 1 (wote waliompokea aliwapa uwezo wa kuwa wana wa Mungu).

Binafsi wale wana wa Mungu wa mwanzo kuwa wana wa seth, inaelewaka sana na inaleta mantiki zaidi.
 
Ile kusema kuwa mwingine alitoa sadaka iliyonona mwingine akatoa Ili dhaifu kuna mtu alisema ile ilikuwa target ya watu wapiga dili kanisani lakini uhalisia ni huo. Hivi kikawaida tu fikiria eti we ubarikiwe mi nichukie hadi niwaze kukuua ili nipate nini labda??

Lakini kuhusu mke nakuua aisee ila nikuue kisa unabarikiwa ni uongo.

Njoo kwenye maisha ya kawaida mtu anayebarikiwa kwenye familia hutegemewa sana na kupendwa sana na kuombwa msaada sana. hivo navoona Abili angependwa na kuombwa msaada na ndugu zake. Lakini Niambie ukweli kutoka moyoni kaka au mdogo wako akikuingilia kwa mkeo utamfanyaje??
Ndugu wangapi wameuana kisa mapenzi wengine wameua wazazi ila sijawahi kusikia Ndugu anamuua ndugu yake kisa ndugu anabarikiwa labda atake kumuibia ila sio kwa baraka na Kain asingemaindi maana kuchunga tu hajui yeye alikuwa Shamba boy[emoji120]
mkuu hayo maneno unayatoa wapi ya hao jamaa kuwa waligombania wake.
Bibilia inazungumzia matendo ya Ibada ndio yaliwatofautisha kaini na Abeli.
ni kawaida mtu aliyefanikiwa kuonewa wivu.
lakini nakubaliana na wewe kuwa adamu alikuwa na watoto wengi, na ilibidi waoane ndugu ili kupropagate kizazi.
 
Lakini movies za Clash of the Titans Wrath of the Titans.... Zinaweza kua na majibu kidogo.
 
Nilikua nataka nisome hadi mwisho lkn umenimaliza poz yani malaika kazaa na mwanadam?? Hii haiko sawa jaman sisi tunaambiwa malaika hanaga jinsia ngoja tu niishie hapa.
Kumbe umeambiwa..! nikajua umesibitisha[emoji124] [emoji124]
 
Hatujaambiwa walikuwa jinsia gani so huenda kulikuwa na wanefili wa kiume na wakike. Ila uzao wao upo mfano huyu mfalme ogu alikuwa anatawala MAJIJI 60 kwenye himaya ya jamii yake ikimaanisha aliweza kuwa na uzao ingawa hatujaelezwa huyo mke wake alikuwa wa aina gani kma naye ni alikua mnefili ama lah ila kwa kujibu swali lako tuamini tu kuwa kulikuwa na wanawake wanefili pia hivyo walilala nao hao hao
Sasa kwa ukubwa huo wa wanefili wa kike ilikuwa lazima wajamiiane na wanefili wenzao wa kiume. Sababu mwanaume wa kawaida ungeweza kuzama na kupotelea kwenye kiungo cha uzazi cha jitu la kike. Vivyo hivyo mwanamke wa kawaida angewekewa dhakari ya jitu la kiume ingekuwa kama kabebeshwa nguzo ya umeme angekufa papo hapo.

Swali linakuja wanefili(majitu) walizaana vipu na binadamu?

Labda tujenge nadharia kwamba baba wa wanefili wa kwanza walikuwa malaika waovu ambao kwa uwezo wao walichukua maumbo madogo ya miili sawa na binadamu.
Lakini walipowapa mimba binadamu ndipo wakazaliwa watoto majitu yaani wanefili wanaume kwa wanawake. Nao wanefili wakapata kuoana wenyewe kwa wenyewe.
 
Wale waliokuwa kizazi cha Sethi walikuwa wana wa Mungu, Kizazi cha Kaini walikuwa Wanefili, Kizazi cha ndugu au madogo wa Sethi hao ndio wana wa Binadamu.
 
Narudia Tena wana wa Mungu ni kizazi cha Sethi wana wa binadamu ni kizazi cha ndugu wa Sethi na wanefili ni kizazi cha Kaini.

Wengine wanajua kabisa Adam alipata kuzaa watoto 40 mara 20 kila uzao pacha ni dume na jike.

Hata ugomvi wa kaini na Abili ilikuwa mke Abili alitaka kumuoa pacha wa kaini kaini akamwambia muoe dadako dadangu mzuri hivi, wakwako mbaya kila mtu aoe dada yake. na hapo ndio wakamwambia Adam, Adam akasema Abili uko sahihi kaini akahisi haki haijatendeka, Adam akasema basi tumuulize Mungu wakaomba wakanuia wakaweka sadaka kila mtu alitwaa katika kazi yake mfugaji aliweka mnyama na Mkulima aliweka mazao, Kwa kuwa Abili alikuwa sahihi Mungu akaitwaa sadaka Ya Abili utata ukaisha lakin kwa kuwa kaini hakuridhika na alichukia ndipo shetani akamjaza hasira na kumpa mbinu za kumuua ndugu yake kabla hajamuoa dadake, Kaini akatimiza Lengo la Shetani. Abili akafa ndipo Mungu akahamishia Baraka kwa Uzao uliofata yaan Sethi. sijui niongeze nini.
Mkuu hao wana wa mungu(kizazi cha sethi) si ndio walizaa na wana wa binadamu (kizazi cha ndugu wa sethi) ndio wakawapata hao wanefili..
Sasa hao wana wa kaini wanakuaje wanefili tena?
 
pia haikusemwa mbele za Bwana kuwa ni mbinguni au kolote kule
Hata wanao enda kwenye masinagogi makanisani misikitini huwa wanajihudhurisha mbele za Mungu nao huitwa wana wa Mungu

prove kama wana wa Mungu ndi malaika?
Neno wana wa Mungu lilitumika hapo kwenye Biblia Asilia ya kihebrania ni neno "B'nai Elohim" ambalo sehemu zote lilipotumika lilimaanisha Malaika.
 
Mkuu hao wana wa mungu(kizazi cha sethi) si ndio walizaa na wana wa binadamu (kizazi cha ndugu wa sethi) ndio wakawapata hao wanefili..
Sasa hao wana wa kaini wanakuaje wanefili tena?
Wana wa Mungu walizaa na wana wa binadamu watu hodari, kumbuka tayari wanefili walikuwepo au rudia kusoma hicho kifungu
 
Mkuu zitto junior ukitaka uyasome vizuri haya mambo watafute wasomi wa Theolojia hawa wafuatao. Dr. Kenneth Hovind, Dr. Perry Stone na Dr.Finnis Dake.

Dr. Finnis Dake wanatheolojia wenzake wanamwita a Heretic kwasabababu alifanya utafiti kuhusu uumbaji kwa miaka 30 na akaja na nadharia zake ambapo akadai kwamba kabla ya Uumbaji kulikwa na Pre-Adamites walioishi hapa duniani.
Akatoa na ushahidi wa mistari ya kibiblia ili kuweka uzito.

Akasema dunia iliumbwa mara ya kwanza kabisa lakini kwenye uumbaji anasema hakuna sehemu ambayo maji yaliumbwa hivyo akadai na kusema kwamba kulikuwa na Mafuriko ya kwanza hata kabla ya yale ya Nuhu. Kibaya zaidi ni kwamba Mafuriko ya kwanza yalikuwa yakumtoa Lucifer mbunguni baada ya vita.

Akasema kwamba Lucifer alianguka kabla ya Uumbaji na Mungu akaamua kuumba viumbe wengine (Binadamu) ili kuyhibitisha kwamba yeye huwa hakosei na ndiyo maana Lucifer akawa anawashambulia sana wanadamu. Sasa akauliza swali, kama Lucifer alianguka duniani kabla ya Uumbaji aliangukia dunia ipi hiyo ???

Amezungumzia uwepo wa Pre-Adamites ambao Mungu aliamua kuwagharikisha baada ya kuanguka kwa Lucifer kwasababu walijiunga naye kwenye Uasi dhidi ya Mbingu.

Amezungumzia vitu vingi sana kwa kupitia maandiko mbali mbali. Vitabu vyake na CD vilikuwepo nyumbani kwetu miaka ya nyuma kidogo. Kama bado zipo ntajaribu kuscan baadhi ya kurasa na kurip baadhi ya video halafu ntaviweka hapa.
 
Back
Top Bottom