mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
"... hao ndio walikuwa watu hodari wenye sifa"Sasa mkuu kama ni uzao wa binadamu kwa nini wao wakatenganishwa jina lao wakaitwa Nephil na wassitwe binadamu yaani mi nataka nijue asili yao hawa viumbe walitokana na nini?
mkuu, wana wa Mungu ambao wanachukua hadhi flani ya malaika angalau ni wale wa kwenye kitabu cha ayubu ambao shetani alijihudhulishaamoja nae.Hapana mie nakubali kuwa WANA WA MUNGU ni malaika kwenye baadhi ya mistari ya biblia lakini vilevile inamaanisha WANADAMU kwenye mistari mingine ya biblia sijui inakaa vzuri hii maana ukisoma daniel 23 na 28 biblia iko wazi kabisa inataja neno MALAIKA kwenye nafasi ya WANA WA MIUNGU hivo ikimaanisha wana wa Mungu ni malaika kuendana na kitabu cha daniel ila wakuu wengine kina mitale na midimu wanajengea hoja kupitia mistari mingine mingi tu inayoonyesha WANA WA MUNGU ni wale wanaomcha Mungu na kufanya mapenzi yake
So nikatoa conclusion kuwa kila mahala Wana wa Mungu inapotajwa tuangalie muktadha na sio JINA maana naamini kila mwandishi aliandika kwa muktadha tofauti ila all in all kwa mistari kadhaa ya biblia upo sahihi tu kuwa wana wa Mungu ni MALAIKA
umeandika points mkuu nakubaliana na wewe.Mkuu mwana wa Mungu inatafsiri tofauti kwa kila kifungu inapotajwa sasa kwa muktadha wa job na zaburi na daniel wana wa Mungu ni MALAIKA
Ila kwa mwanzo kwa uelewa wangu wana wa Mungu pale ni wana wa seth sababu ndio waliokuwa wasafi ila wanadamu ni uzao wa cain (kizazi cha nyoka) ila bado kuna wanaoweza kujengea hoja kuwa wana wa Mungu wanaotajwa kwenye zaburi kuwa walishangilia pamoja na nyota ya asbuhi siku dunia inaumbwa ndio hao hao wanaotajwa na mwanzo 6:4 hivyo hii mistari bado ni mjadala unless tuseme wana wa Mungu kwa kila kitabu ina maana tofauti ila tukizifungamanisha basi ndio inazaa mjadala kma hivi kuwa ipi ni ipi nachoona muhim tuangalie muktadha wa kitabu husika na tusifungamanishe kuwa definition ya mwana wa Mungu ni moja kwa biblia nzima nafkiri hii itasaidia kupunguza mkanganyiko huo
Cc impongo Mchawi Mkuu mitale na midimu
Hapana Ni lazima ujiongeze kidg. Ni Mara chache au hakuna anayefundisha haya kanisaniWanahistoria na wachunguzi wa mambo kwa namna ya akili tu ya kawaida[emoji23]
mkuu hayo maneno unayatoa wapi ya hao jamaa kuwa waligombania wake.Ile kusema kuwa mwingine alitoa sadaka iliyonona mwingine akatoa Ili dhaifu kuna mtu alisema ile ilikuwa target ya watu wapiga dili kanisani lakini uhalisia ni huo. Hivi kikawaida tu fikiria eti we ubarikiwe mi nichukie hadi niwaze kukuua ili nipate nini labda??
Lakini kuhusu mke nakuua aisee ila nikuue kisa unabarikiwa ni uongo.
Njoo kwenye maisha ya kawaida mtu anayebarikiwa kwenye familia hutegemewa sana na kupendwa sana na kuombwa msaada sana. hivo navoona Abili angependwa na kuombwa msaada na ndugu zake. Lakini Niambie ukweli kutoka moyoni kaka au mdogo wako akikuingilia kwa mkeo utamfanyaje??
Ndugu wangapi wameuana kisa mapenzi wengine wameua wazazi ila sijawahi kusikia Ndugu anamuua ndugu yake kisa ndugu anabarikiwa labda atake kumuibia ila sio kwa baraka na Kain asingemaindi maana kuchunga tu hajui yeye alikuwa Shamba boy[emoji120]
Kumbe umeambiwa..! nikajua umesibitisha[emoji124] [emoji124]Nilikua nataka nisome hadi mwisho lkn umenimaliza poz yani malaika kazaa na mwanadam?? Hii haiko sawa jaman sisi tunaambiwa malaika hanaga jinsia ngoja tu niishie hapa.
Sasa kwa ukubwa huo wa wanefili wa kike ilikuwa lazima wajamiiane na wanefili wenzao wa kiume. Sababu mwanaume wa kawaida ungeweza kuzama na kupotelea kwenye kiungo cha uzazi cha jitu la kike. Vivyo hivyo mwanamke wa kawaida angewekewa dhakari ya jitu la kiume ingekuwa kama kabebeshwa nguzo ya umeme angekufa papo hapo.Hatujaambiwa walikuwa jinsia gani so huenda kulikuwa na wanefili wa kiume na wakike. Ila uzao wao upo mfano huyu mfalme ogu alikuwa anatawala MAJIJI 60 kwenye himaya ya jamii yake ikimaanisha aliweza kuwa na uzao ingawa hatujaelezwa huyo mke wake alikuwa wa aina gani kma naye ni alikua mnefili ama lah ila kwa kujibu swali lako tuamini tu kuwa kulikuwa na wanawake wanefili pia hivyo walilala nao hao hao
Wana wa Mungu ni kile kizazi che Sethi na wana wa wanadamu ni kizazi cha Kaini.
Wewe kwa iman yakoSi kwamba malaika hana jinsia tu, bali hakuna kitu kinachoitwa malaika, ni hadithi za kimapokeo tu.
Mkuu hao wana wa mungu(kizazi cha sethi) si ndio walizaa na wana wa binadamu (kizazi cha ndugu wa sethi) ndio wakawapata hao wanefili..Narudia Tena wana wa Mungu ni kizazi cha Sethi wana wa binadamu ni kizazi cha ndugu wa Sethi na wanefili ni kizazi cha Kaini.
Wengine wanajua kabisa Adam alipata kuzaa watoto 40 mara 20 kila uzao pacha ni dume na jike.
Hata ugomvi wa kaini na Abili ilikuwa mke Abili alitaka kumuoa pacha wa kaini kaini akamwambia muoe dadako dadangu mzuri hivi, wakwako mbaya kila mtu aoe dada yake. na hapo ndio wakamwambia Adam, Adam akasema Abili uko sahihi kaini akahisi haki haijatendeka, Adam akasema basi tumuulize Mungu wakaomba wakanuia wakaweka sadaka kila mtu alitwaa katika kazi yake mfugaji aliweka mnyama na Mkulima aliweka mazao, Kwa kuwa Abili alikuwa sahihi Mungu akaitwaa sadaka Ya Abili utata ukaisha lakin kwa kuwa kaini hakuridhika na alichukia ndipo shetani akamjaza hasira na kumpa mbinu za kumuua ndugu yake kabla hajamuoa dadake, Kaini akatimiza Lengo la Shetani. Abili akafa ndipo Mungu akahamishia Baraka kwa Uzao uliofata yaan Sethi. sijui niongeze nini.
Neno wana wa Mungu lilitumika hapo kwenye Biblia Asilia ya kihebrania ni neno "B'nai Elohim" ambalo sehemu zote lilipotumika lilimaanisha Malaika.pia haikusemwa mbele za Bwana kuwa ni mbinguni au kolote kule
Hata wanao enda kwenye masinagogi makanisani misikitini huwa wanajihudhurisha mbele za Mungu nao huitwa wana wa Mungu
prove kama wana wa Mungu ndi malaika?
Wana wa Mungu walizaa na wana wa binadamu watu hodari, kumbuka tayari wanefili walikuwepo au rudia kusoma hicho kifunguMkuu hao wana wa mungu(kizazi cha sethi) si ndio walizaa na wana wa binadamu (kizazi cha ndugu wa sethi) ndio wakawapata hao wanefili..
Sasa hao wana wa kaini wanakuaje wanefili tena?
Mkuu hawa nephilism waliokimbia dunia wana uhusiano wowote na annunnaki?