Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mkuu nikubali tu leo umenifunza kitu kipya sijawahi kukisikia kabisa kuwa ugomvi wa cain na abel ulianzia kwa sketi!!! Duh you're a real great thinker ahsante kwa elimu hii adimu mkuu
Kwamba Abili na Caini waligombania papuchi?

Mbona biblia haisemi hivyo?
 
Mkuu mitale na midimu mie bado nashikilia msimamo kuwa kila inapotajwa wana wa Mungu tuisome kwa context husika sio general sababu kati ya hizo maana 3 unakuta kila mwandishi alimaanisha yake ila kuhusu mwanzo 6 hao wana wa mungu walikua ni wanadamu au Malaika nafkiri tuangalie muktadha alafu linganisha na huu mstari

Yuda 1:6
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

Je kwanni mwandishi hapa alinganishe uasherati wa sodoma na gomora kama hao MALAIKA??

Neno KAMA VILE .......KWA JINSI MOJA NA HAWA yanaleta maswali zaidi kwanni uzinzi ndio ulinganishwe na wale malaika?? Ina maana hawa malaika walikuwa wanalala na wanawake ingawa sio asili yao??? Embu tuwekane sawa mkuu

Barikiwa
Kosa walillolifanya hawa malaika ni kutaka haki za ndoa walitaka nao wafanywe kama alivyofanywa binadamu yaani Mungu alipomuumba binadamu Aliwaambia malaika wote wapige goti na kusujudu kuwa huyu ndiye Mwana Wa Mungu. Wale malaika pamoja na Shetani waliasi maana wao walikataa wakimwita adam ni udongo nao ni nari.

Bado kuna ushahidi kuwa malaika sio wana wa Mungu bali wana wa Mungu ni kile kizazi tiifu cha Adam
 
Hoja yangu sio nebukadneza nasema neno lilitomuka kwenye biblia ya kiebrania ni MOJA yaani bene elohim? Ila limeelezwa kama mwana wa Mungu kwenye mstari wa 23 na baadae ikaelezwa kama malaika kwenye 28 hoja hapa ni kwamba LINA MAANA MOJA kwa muktadha wa kitabu cha daniel na ndio maana limeelezwa kma substitute ya malaika na mwana wa Mungu

Hivyo usiangalie alichosema nebukadneza ila angalia muandishi wa kitabu ambaye alikuwa na ufaham wa dini na alijua tofauti ya mwanadamu na malaika ila bado alitumia NENO moja tu kwenye verse 23 na 28
Mkuu mitale na midimu mie bado nashikilia msimamo kuwa kila inapotajwa wana wa Mungu tuisome kwa context husika sio general sababu kati ya hizo maana 3 unakuta kila mwandishi alimaanisha yake ila kuhusu mwanzo 6 hao wana wa mungu walikua ni wanadamu au Malaika nafkiri tuangalie muktadha alafu linganisha na huu mstari

Yuda 1:6
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

Je kwanni mwandishi hapa alinganishe uasherati wa sodoma na gomora kama hao MALAIKA??

Neno KAMA VILE .......KWA JINSI MOJA NA HAWA yanaleta maswali zaidi kwanni uzinzi ndio ulinganishwe na wale malaika?? Ina maana hawa malaika walikuwa wanalala na wanawake ingawa sio asili yao??? Embu tuwekane sawa mkuu

Barikiwa
amina mkuu.
muktadha unahusika sana ktk kupata maana isiyojikanganya.
Yuda kabla hajaandika 7,kuhusu ufanano wa uzinifu wa sodoma na uzinifu unaodhaniwa kuwa wa malaika wachafu.
Mstari wa sita unaweza kuweka record sawa. "AMEWAWEKA KATIKA VIFUNGO VYA MILELE CHINI YA GIZA KWA HUKUMU YA SIKU ILE KUU"

Kama waliwekwa katika vifungo, napata tabu kuamini kama waliweza kutoroka na kuzini na wanadamu.
pia Authoritative statement ya Yesu kuwa viumbe hao hawafanyi tendo la ndo. Pia neno wana wa Mungu kuwatwaa, ni neno hilohilo lililotumika wanadamu wanapotwaana kupata watoto. nashawishika kuamini walikuwa ni wanadamu na inaleta maana zaidi ya kuwa mapepo au malaika. Pia nikiamini Yesu Alihusika ktk uumbaji (Pasipo mimi hakikufanyika kitu). anafahamu hilo kuliko sisi.

Assumption kwamba Uzinzi umelinganishwa na maraika, hata hosea alipoambiwa akamuoe Gomeri (mwanamke wa uzinzi) Mungu alifafanua Kumuacha yeye na kugeukia vitu vingine pia ni UZINZI.

lakini nakubaliana kuwa Kitabu Cha ENOCH ambacho si cha kibibilia kinaweka wazi moja kwa moja kuwa malaika wanafanya mapenzi na wanadamu. Na Imani nyingi nje ya bibilia inaamini hayo.

maoni mkuu.
 
zitto junior. Kuna vitu tumefichwa lakini ukweli ni kuwa Mungu alimuumba mwanadamu kukiwa kuna maisha ya viumbe kama binadamu tayali.
Na sijui kwanini Mungu aliamua kutupunguzia maisha wakati viumbe wake waliotutangulia ndio wametufanya tuingie katika majaribu ya kutuhadaa

Ushahidi wa viumbe waliokuwepo kwa mjibu wa Biblia

5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanzo 3 :5

Hapa Mungu anatufananisha na viumbe waliotangulia hapa kuna kitu ukitafakari unapata jibu la kuwepo maisha yaliyoendelea

3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
Mwanzo 6 :3
Kwanini Mungu atupunguzie umri ili hali yeye ndiye katuumbia vitu vya kutupotosha?

Kwanini Mungu asingetupeleka sayari nyingine tuanze maisha yetu yasiyo na mchanganyiko wowote?

Kwanini Mungu asinge tupeleka hata kwenye nyota (jua) proxima century mbali na hapa tukawa mbali na wanefili?

Maana wanefili bado wanaishi ila Mungu kawapunguzia uwezo wa nguvu lakini ndiyo jamii zenye ushawishi na nguvu kiuchumi kuindesha Dunia ndio wazungu wenye macho njano.

Kwa picha hii ni uthibitisho tosha kuwa wapo ila hawana nguvu za mwili ila wamebaki kiakili
Kuna sehemu nilisoma kuwa walikufa kwenye gharika ila roho zao hakuziua. Ili dunia ijayo ijue na ione kazi zake.
Na ndio hawa wanaotawala dunia now
 
amina mkuu.
muktadha unahusika sana ktk kupata maana isiyojikanganya.
Yuda kabla hajaandika 7,kuhusu ufanano wa uzinifu wa sodoma na uzinifu unaodhaniwa kuwa wa malaika wachafu.
Mstari wa sita unaweza kuweka record sawa. "AMEWAWEKA KATIKA VIFUNGO VYA MILELE CHINI YA GIZA KWA HUKUMU YA SIKU ILE KUU"

Kama waliwekwa katika vifungo, napata tabu kuamini kama waliweza kutoroka na kuzini na wanadamu.
pia Authoritative statement ya Yesu kuwa viumbe hao hawafanyi tendo la ndo. Pia neno wana wa Mungu kuwatwaa, ni neno hilohilo lililotumika wanadamu wanapotwaana kupata watoto. nashawishika kuamini walikuwa ni wanadamu na inaleta maana zaidi ya kuwa mapepo au malaika. Pia nikiamini Yesu Alihusika ktk uumbaji (Pasipo mimi hakikufanyika kitu). anafahamu hilo kuliko sisi.

Assumption kwamba Uzinzi umelinganishwa na maraika, hata hosea alipoambiwa akamuoe Gomeri (mwanamke wa uzinzi) Mungu alifafanua Kumuacha yeye na kugeukia vitu vingine pia ni UZINZI.

lakini nakubaliana kuwa Kitabu Cha ENOCH ambacho si cha kibibilia kinaweka wazi moja kwa moja kuwa malaika wanafanya mapenzi na wanadamu. Na Imani nyingi nje ya bibilia inaamini hayo.

maoni mkuu.
Ili hii mada iishe lazima tutaje sifa kuu za hawa viumbe watatu
1Wana wa Mungu
2Wana wa binadamu
3Malaika.

Tukijua sifa za hawa viumbe ubishi utaisha na ukweli tutaujua na Tutakuwa tumejifunza jambo la kudumu.
 
Siyo kila mzungu anajua Siri ya ulimwengu!.
Kuna kikundi cha WATU wachache!.
Also SUPER NATURAL!.
Yupo Na kusudi maalumu!
So ipo siku mtafunuliwa yale ambayo mlikuwa hamyafahamu
Heee?

Huyo supernatural ndo anatuficha ukweli mkuu?
 
Siyo kila mzungu anajua Siri ya ulimwengu!.
Kuna kikundi cha WATU wachache!.
Also SUPER NATURAL!.
Yupo Na kusudi maalumu!
So ipo siku mtafunuliwa yale ambayo mlikuwa hamyafahamu
Na tutafunuliwa lini mkuu?...mda unaenda huu!

Nasikia rocafella ile familia inaujua ukweli wote!
 
Wana wa Mungu ni uzao wa adam...seth.....na kuendelea
Wana wa wanadamu...ni uzao wa Cain ...na kuendelea
Gharika likakipoteza kizazi cha Cain chote sababu Nuhu alikuwa bloodline ya Seth(adam)
Then ikaja BUT BUT BUT why KAANANI alaaniwe badala HAM????
Vipi kuhusu wake wa watoto wa nuhu hasa wa Ham....je alikuwa na damu ya Cain ( au alikuwa tayari ana mimba ya mtu wa uzao wa cain ambaye sio Ham)??????
 
Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu, hapa kuna mkanganyiko mkubwa sana sana.
Lakini tukiangalia kihistoria tutakuja gundua vitu viwili hapa:
Mosi, hoja ya kwamba wana wa Mungu walikuwa ni wana wa Seth na Tabaka fulani lenye nguvu ni theolojia ya Ukristo wa sasa. Ina maana kwamba imekuja baada ya huu Ukristo wetu kuzaliwa na haikuwepo huko kale. Hoja ambayo ilikuwepo huko kale ni hii ya B'Nai Elohim kuwa wana wa Mungu Malaika hata wanahistoria wakubwa wa kale wa Kiyahudi kama Flavuius Josephus amendika hayo kuhusu Malaika na wanadamu kuingiliana. Huyu ni mwandishi ambaye wanathiolojia wengi wanamtumia kama Authority.

Pili, hapo kwenye lugha za Biblia lazima tutofatishe kabisa.
Agano la Kale liliandikwa kwa Kihebrania na Agano jipya Kigiriki na Baadae Kilatini. Binafsi huwa navyosoma Biblia huwa natumia King James Version yenye Strong Concordance ya Kihebrania na Kigiriki. Nimesoma nikaja kugundua kuna baadhi ya maneno yaliyosawa kwenye lugha ya Kiingereza ndani ya biblia moja ni tofauti kabisa na huleta maada tofauti katika lugha zao asili za Kigiriki na Kihebrania. Kama neno "Prayer" ni kuomba lakini kigiriki na Kihebrania yanakuwa na tofauti zake kidogo. Ndiyo maana katika usoma Biblia kuna Verse to Verse reading, Amplified Meaning and Contextual Meaning.
Lazima uzitumie zote hizi ili kuweza kupata maana halisi ya neno. Sasa siku hizi shida inakuja ni kwamba watu wengi tunasoma bila kuwa na ufahamu wa Uchambuzi na hapa tunapata sana shida...Kwasababu mbali na mistari ya Biblia ni lazima mwanatheolojia yoyote ajue ni kipindi gani ule mstari uliandikwa na kwasababu gani uliandikwa.

Yote tisa,
Hizi ni nadharia tu Mkuu, tuzisome na tuzichambue bila kuvuka mipaka na kupotosha NENO TAKATIFU LA MUNGU.
Ndiyo maana Mtume Paulo aliwahi kuwaonya Wakristo kwamba wajiepushe sana na simulizi za Wayahudi zisizo na msingi kama zile za Masadukayo kusema hakuna Kiama.
nimekupata vizuri mkuu, hasa kwenye hitimisho pametulia zaidi.
ninaking james yangu hapa yenyewe hata chakula inaita nyama (meat).
sina reference za kigiriki na kiebrania, zaidi huwa natafuta kwenye websites zinazotoa ufafanuzi wa neno kwa neno.
Taadhali ni muhimu katika kujadili huku ukiwa na backup ya ukweli. Binafsi naamini Bibilia ina ULTIMATE AUTHORITY kwenye maisha yangu ya Imani, chochote nje ni assumption kama zinaumana na bibilia naziamini kama zinapingana bibilia inabaki kama mamlaka kuu.
Natambua kuna maandishi mengi nje ya bibilia ambayo yanapewa hadhi sawa na bibilia lkn contents zinakinzana na bibilia. nimejiwekea wigo wa bibilia pekee.

Kuhusu suala la Tuiache bibilia ijitafsiri kusema wale ni malaika au sio malaika inaweza ikawa na impact ndogo katika imani. Lkn nadhalia ya wale kuwa malaika mkuu inafungulia mafuriko ya mafundisho tata kuaminika.
1: Itakutaka uamini kitabu cha Enoch &co ambacho kina contradictions kibao.
2:Bibilia inasema mwanadamu nimekuumba punde kidogo ya malaika, akiwepo nephili ambaye ni hybrid wa malaika maana yake atakuwa na intermediate ability, hivyo kama ambavyo majini na mapepo hayakufa katika mafuriko kuna uwezekano akawepo huyo mdau OGU kukwepa hiyo adhabu ya Mungu. Hii inahafifisha uwezo wa Mungu kuwa wanadamu hao wanaweza kukwepa adhabu ya Mungu kiujanjaujanja.
3:Itabidi tukubaliane na hadithi zilizopo uswahilini kuwa flani alizaa na jini.
4:Itabidi tutlie mashaka authoritative statement ya yesu kuwa Malaika hawazai, wala hawana hizo habari.
5:Itatutaka tujiulize hilo zoezi la mapenzi ya malaika na wanadamu lilikwamia wapi, maana baada ya gharika majin na malaika walikuwepo, na hao wanadamu wapo hivyo hadi kesho tunaweza kudate malaika na majini. Tutaipa mzigo bibilia kutoa majibu ambayo tayari yapo kwenye vitabu vinavyopingana na bibilia.

mtazamo kiongozi.
 
Wana wa Mungu ni uzao wa adam...seth.....na kuendelea
Wana wa wanadamu...ni uzao wa Cain ...na kuendelea
Gharika likakipoteza kizazi cha Cain chote sababu Nuhu alikuwa bloodline ya Seth(adam)
Then ikaja BUT BUT BUT why KAANANI alaaniwe badala HAM????
Vipi kuhusu wake wa watoto wa nuhu hasa wa Ham....je alikuwa na damu ya Cain ( au alikuwa tayari ana mimba ya mtu wa uzao wa cain ambaye sio Ham)??????
Huko tulishamaliza kiongozi!.
Soma books of Enoch utaelewa.
 
Mc Tilly Chizenga.
Malaika hawana maumbo wala wanefili si malaika

4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
Mwanzo 6 :4

asante mkuu,lakini hakuna sehemu nimesema wanefili ni malaika wala hakuna sehemu nimesema malaika wana maumbo!nilimhoji jamaa aliyesema wanefili ni uzao wa binadamu na malaika ndio nikamuuliza ukubwa huo wa wanefili umesababishwa na "maumbo" makubwa ya malaika ili akijibu nimbananishe kwenye engo ya kwamba malaika ni roho tu!!!
 
Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu, hapa kuna mkanganyiko mkubwa sana sana.
Lakini tukiangalia kihistoria tutakuja gundua vitu viwili hapa:
Mosi, hoja ya kwamba wana wa Mungu walikuwa ni wana wa Seth na Tabaka fulani lenye nguvu ni theolojia ya Ukristo wa sasa. Ina maana kwamba imekuja baada ya huu Ukristo wetu kuzaliwa na haikuwepo huko kale. Hoja ambayo ilikuwepo huko kale ni hii ya B'Nai Elohim kuwa wana wa Mungu Malaika hata wanahistoria wakubwa wa kale wa Kiyahudi kama Flavuius Josephus amendika hayo kuhusu Malaika na wanadamu kuingiliana. Huyu ni mwandishi ambaye wanathiolojia wengi wanamtumia kama Authority.

Pili, hapo kwenye lugha za Biblia lazima tutofatishe kabisa.
Agano la Kale liliandikwa kwa Kihebrania na Agano jipya Kigiriki na Baadae Kilatini. Binafsi huwa navyosoma Biblia huwa natumia King James Version yenye Strong Concordance ya Kihebrania na Kigiriki. Nimesoma nikaja kugundua kuna baadhi ya maneno yaliyosawa kwenye lugha ya Kiingereza ndani ya biblia moja ni tofauti kabisa na huleta maada tofauti katika lugha zao asili za Kigiriki na Kihebrania. Kama neno "Prayer" ni kuomba lakini kigiriki na Kihebrania yanakuwa na tofauti zake kidogo. Ndiyo maana katika usoma Biblia kuna Verse to Verse reading, Amplified Meaning and Contextual Meaning.
Lazima uzitumie zote hizi ili kuweza kupata maana halisi ya neno. Sasa siku hizi shida inakuja ni kwamba watu wengi tunasoma bila kuwa na ufahamu wa Uchambuzi na hapa tunapata sana shida...Kwasababu mbali na mistari ya Biblia ni lazima mwanatheolojia yoyote ajue ni kipindi gani ule mstari uliandikwa na kwasababu gani uliandikwa.

Yote tisa,
Hizi ni nadharia tu Mkuu, tuzisome na tuzichambue bila kuvuka mipaka na kupotosha NENO TAKATIFU LA MUNGU.
Ndiyo maana Mtume Paulo aliwahi kuwaonya Wakristo kwamba wajiepushe sana na simulizi za Wayahudi zisizo na msingi kama zile za Masadukayo kusema hakuna Kiama.
Mkuu Malcom you inspire me a lot dah hata sijui nikupe tuzo gani kwa kazi yako iliotukuka humu jukwaani
 
Back
Top Bottom