Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Ndio maana toka mwanzo nikasema hii mada tusiingize mahaba ya dini tufikirie nje ya box mkuu wwe unasema kusupport uwepo wa OG ni kumpinga Mungu?? Je muandishi wa kitabu cha kumbukumbu la torati naye anampinga Mungu??

Kumbukumbu la torati 3:11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu

Haya basi tufanye tufanye huyu alidanganya je Vipi kuhusu mstari huu

Mwanzo 6 : 4
4 Wanefili walikuwa duniani siku hizo, na pia baada ya hapo......

Je anaposema wanefili walikuwepo toka enzi hizo na hata baadae alikuwa ana maana gani?? Ina maana naye kapotosha??

Anyway basi tufanye hawa wote walipotosha embu tusaidie basi wanefili mfano wa mfalme OG walirudije duniani kma wote walimalizwa kwenye gharika??? Wana wa aruba,anaki,amoni,wahivi,amori,wayebusi n.k wote walikuwa ni wanefili na joshua anawataja ina maana walirudije duniani if at all wote waliuawa kwenye gharika

Tusaidie hapo ili tujifunze zaidi
 
1. Ok mikono 15 sio kama ya sasa ina maana kwa vipimo hivo hivo mikono zaidi ya 15 ambao ndio ulikua urefu wa Mfalme ogu nao sio kama wa sasa ikimaanisha bado aliyazidi maji kma alipanda juu ya milima si ndio maana yake???

2. Sijasema wamvamie tu naongelea situation meli imezama alafu wwe unaona kuna boya kweli wote mtamuacha aliye kwenye boya hku mnakufa maji?? Lazma kwenye kutapatapa mtajikuta mnavamia boya lake ili na nyie mjiokoe ssa jiulize dunia nzima inazama alafu unaona boti kubwaaaaa inaelea tu je utakufa bila hata kijaribu kuiparamia ili kujiokoa?? Ssa pata picha lijimtu kma goliath livamie boti si wangeivunjilia mbali!!!

Anyway ni nadharia tu ila zina make sense kwa kiasi chake
 
Sahihi kabisa
Kulikuwa Na mijitu ke Na me!
Lakini kwa kuanza mkuu zitto tambua kuwa mbegu ya giants Bado ipo.
Nimesikia hizi tetesi ila sijawahi kuzikalia chini kuzidadavua..... Embu tupe mbili tatu mkuu
 
Kitu ninachokijua kwa sehemu ndogo tu kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba, Mungu akitaka kufanya jambo lake hashindwi kulifanya, huyo mnefili aliyesalia kwa kufikiri fikiri tu yaweza kuwa alikuwa mimba wakati wa gharika labda.
Kinyume na hapo yaliyobakia yote ni vigumu kukubaliana nayo kwa sababu tangu mvua kunyesha mpaka maji kuanza angalau kupungua ni zaidi ya mwaka! Sasa huyo ni kiumbe gani mwenye mwili ambaye hali wala kunywa kwa mwaka mzima kwenye dharuba nzito namna hiyo?!!!
 
Fanya hivyo mzee may be I can change my view cause a critical thinker always changes his view when presented with better argument
 
Wewe ndo unachanganya huoni amekwambia walijitwalia mabinti? Sasa unaposema Wanefili walikuwepo kabla ya binadamu una maanisha nini?
 
Nilikua nataka nisome hadi mwisho lkn umenimaliza poz yani malaika kazaa na mwanadam?? Hii haiko sawa jaman sisi tunaambiwa malaika hanaga jinsia ngoja tu niishie hapa.
 
Grahnman. Sasa mkuu hapo nimechanganya wapi?
Wana wa Mungu waliwaona wana wa binadamu ya kuwa ni wazuri je wana wa Mungu walikuwa wapi?

Rejea hapa 4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
Mwanzo 3 :4

5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanzo 3 :5

Huyu nyoka alitoka wapi?
Je jamii hii ya wanefili si unaona wamekuwa na ustaarabu kabla ya wanadamu
 
Mkuu wana wa Mungu si anamaanisha hao Malaika walioshuka kuja kulala na hao wanawake mkuu
 
Najua kufikia hapa wengi mtasema ni upotoshaji na kwamba ni stori za kijiweni ila hoja hii inapata mashiko kupitia biblia kuwa mfalme OGU alikuwa ndio mnefili pekee aliyepona gharika.
Mwanzo 7:21 Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;

mkuu source nyingine sawa, ila bibilia hapana. Vilikufa vyote. labda kama swntensi hiyo niliyoiquote ilimaanisha nini.
 

Mkuu Point yako ipo sahihi kiasi chake maana hatuna ushahidi wa moja kwa moja lakini inasemekana binadamu alikuwepo kabla ya uumbwaji wa Adamu

Nitarudi ili tusaidiane katika kulifahamu hili ningojee kidoogo
Naja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…