Mfalme Suleiman (Solomon) alikuwa na wake 700 na michepuko 300 kweli? Kwanini?

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,377
Reaction score
3,394




Juzi nilipokwenda dukani kununua liwa kwa ajili yakurembesha uso wangu. Muuzaji alinifungia liwa hiyo kwenye kipande cha karatasi ambacho kilikuwa na habari inayomhusu Nabii Suleiman AS.

Huyu nabii anaelezwa kwamba alikuwa na utajiri mkubwa usiyo kifani, lakini pia alikuwa na busara na hekima haijapata kutokea hapa duniani. Alikuwa na nguvu sana na utajiri wake ulikuwa ni mkubwa usioweza kupimika.

Lakini pamoja na kujaaliwa neema zote hizo lakini vyote hivyo havikuwa na maana yoyote kwake.

Inasemekana alikuwa ni mwanaume shababi mwenye siha nzuri. Pamoja na kuwa na wake 700 na nyumba ndogo zipatazo 300, lakini kamwe hakuna na amani moyoni mwake.

Je ni kitu gani alikosa nabii huyu?
  1. Wake warembo alikuwa nao 700
  2. Nyumba ndogo zilizojaaliwa neema za Allah zilikuwa 300
  3. Hekalu kubwa lenye kila aina ya nakshi vikiwemo vito vya thamani
  4. Utajiri mkubwa usio na mfano ulikuwa mikononi mwake
Alikuwa ana uwezo wa kupata starehe zote alizozitaka hapa duniani zikiwepo pombe za kila aina huku akiwa amezungukwa na wanawake warembo wa kila sampuli waliojaaliwa neema za Allah……. Mh!

Unaweza kushangaa, Je ni kitu gani amekikosa mtu huyu?

Naam, hebu angalia maisha ya vijana wa kiume wa nyakati hizi.Wanahangaika sana kutafuta fedha, wanajenga mahekalu,wananunua magari ya kifahari, wanaoa wake warembo, wanakuwa na uwezo wa kula starehe sana tena za kila aina, watatafuta nyumba ndogo zisizo na hesabu,lakini bado hawatatosheka.

Pamoja na habari hiyo ya nabii Suleiman ambayo wengi wetu tunaifahamu vyema, lakini bado vijana wa kiume wameshindwa kung'amua kwamba hivi vitu vya nje, yaani Fedha, na fahari zote za dunia si chochote, na kamwe haviwezi kutuletea amani na ridhiko hata siku moja katika maisha yetu.

Kama Nabii Suleiman hakupata ridhiko kwa amali alizojaaliwa na Mwenyenzi Mungu seuze wao!

Ni kuhangaika tu kusiko na mashiko na kamwe fedha,mahekalu na wanawake wanene wanene wenye makalio makubwa na matiti yenye kututumka vifuani na sura za kuvutia si mali kitu, havitawafaa hata kwa miaka dahari.

Mtafuteni Mungu atawaongoza, acheni michepuko,tulieni na wake zetu.

Ujumbe huu uwafikie

Asprin, Mentor, KakaKiiza, Kaizer, Ntuzu, mwekundu, mayenga, ayanda, Kiranga, Nyani Ngabu
 
Ok,Na sisi tutaoa wake angalau 70 ili tutulie na pia nyumba ndogo angalau 10 ili tusihangaike na michepuko. Natania bwana
 
Peace of mind au furaha inatoka moyoni mwako kamwe usitegemee kutoka kwa mtu au vitu (hasa hasa wanawake ndo wanadhani furaha inatokana na magari,fedha ,nyumba etc)mwingine they will disappoint you
You are responsible for your own happiness,
 
Yaani hio ni karibbia na Female wote wa JF andhani, duh jamaa si mchezo nadhani alikua anatumia dawa fulani hivi
 
furaha ya maisha unaitengeneza mwenyewe hakuna binadamu atakaye kuletea furaha......
 
Peace of mind au furaha inatoka moyoni mwako kamwe usitegemee kutoka kwa mtu au vitu (hasa hasa wanawake ndo wanadhani furaha inatokana na magari,fedha ,nyumba etc)mwingine they will disappoint you
You are responsible for your own happiness,

kumbe unaakili wakati mwingine
 
Hela/fedha sio kila kitu katika kuleta furaha,nafikiri amani ndani ya moyo ndio kila kitu
 
bora tu iwe credit kwa maana unajua kingetokea nn

ivi hawa wanawke 700 alikuwa anawpa huduma kivipi..it means baada ya twoo yrs ndo anapata gegedo mwaka una siku 365........

Ushaambiwa alikuwa na siha nzuri na ni mwanaume shababi, unadhani atakuwa kama Kaizer au Asprin au Mentor ?
Hapo ilikuwa ilikuwa kumi kwa siku na wote wanapata habari yao, siyo hawa wanaume wa siku hizi wa chipsi mayai na kachumbari
 
Last edited by a moderator:
Ushaambiwa alikuwa na siha nzuri na ni mwanaume shababi, unadhani atakuwa kama Kaizer au Asprin au Mentor ?
Hapo ilikuwa ilikuwa kumi kwa siku na wote wanapata habari yao, siyo hawa wanaume wa siku hizi wa chipsi mayai na kachumbari

Chakula Chetu Cha Siku Hizi
Asubuh Chai Na Slesi Mbili Na Yai La Kisasa Moja
Mchana Chipsi Na Tu Mishkaki Na Maji Kilimanjaro
Usiku Super Gate Tambi Na Ka Safari Siku Imeisha.
NAENDA KUMGEGEDA WIFE DAKIKA YA 3 HOI NIMESHA LALA. MASKINI MKE WANGU NDIO KWANZAAA......
 
Last edited by a moderator:
Story nzuri,unaweza ukawa na mali nyingi na wake wengi wazuri bado huna amani ,amani ya moyo hailetwi na mali nyingi wala wake wengi

Inaletwa na nn hiyo Amani ya moyo mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…