tian
JF-Expert Member
- Jul 27, 2007
- 1,770
- 538
Inaletwa na nn hiyo Amani ya moyo mkuu?
Maamuzi binafsi
Inaletwa na nn hiyo Amani ya moyo mkuu?
bora tu iwe credit kwa maana unajua kingetokea nn
ivi hawa wanawke 700 alikuwa anawpa huduma kivipi..it means baada ya twoo yrs ndo anapata gegedo mwaka una siku 365........
Yaani hio ni karibbia na Female wote wa JF andhani, duh jamaa si mchezo nadhani alikua anatumia dawa fulani hivi
Labda Mwati anaweza kumkaribia ha ha ha ha.
Juzi nilipokwenda dukani kununua liwa kwa ajili yakurembesha uso wangu. Muuzaji alinifungia liwa hiyo kwenye kipande cha karatasi ambacho kilikuwa na habari inayomhusu Nabii Suleiman AS.
Huyu nabii anaelezwa kwamba alikuwa na utajiri mkubwa usiyo kifani, lakini pia alikuwa na busara na hekima haijapata kutokea hapa duniani. Alikuwa na nguvu sana na utajiri wake ulikuwa ni mkubwa usioweza kupimika.
Lakini pamoja na kujaaliwa neema zote hizo lakini vyote hivyo havikuwa na maana yoyote kwake.
Inasemekana alikuwa ni mwanaume shababi mwenye siha nzuri. Pamoja na kuwa na wake 700 na nyumba ndogo zipatazo 300, lakini kamwe hakuna na amani moyoni mwake.
Je ni kitu gani alikosa nabii huyu?
- Wake warembo alikuwa nao 700
- Nyumba ndogo zilizojaaliwa neema za Allah zilikuwa 300
- Hekalu kubwa lenye kila aina ya nakshi vikiwemo vito vya thamani
- Utajiri mkubwa usio na mfano ulikuwa mikononi mwake
Alikuwa ana uwezo wa kupata starehe zote alizozitaka hapa duniani zikiwepo pombe za kila aina huku akiwa amezungukwa na wanawake warembo wa kila sampuli waliojaaliwa neema za Allah . Mh!
Unaweza kushangaa, Je ni kitu gani amekikosa mtu huyu?
Naam, hebu angalia maisha ya vijana wa kiume wa nyakati hizi.Wanahangaika sana kutafuta fedha, wanajenga mahekalu,wananunua magari ya kifahari, wanaoa wake warembo, wanakuwa na uwezo wa kula starehe sana tena za kila aina, watatafuta nyumba ndogo zisizo na hesabu,lakini bado hawatatosheka.
Pamoja na habari hiyo ya nabii Suleiman ambayo wengi wetu tunaifahamu vyema, lakini bado vijana wa kiume wameshindwa kungamua kwamba hivi vitu vya nje, yaani Fedha, na fahari zote za dunia si chochote, na kamwe haviwezi kutuletea amani na ridhiko hata siku moja katika maisha yetu.
Kama Nabii Suleiman hakupata ridhiko kwa amali alizojaaliwa na Mwenyenzi Mungu seuze wao!
Ni kuhangaika tu kusiko na mashiko na kamwe fedha,mahekalu na wanawake wanene wanene wenye makalio makubwa na matiti yenye kututumka vifuani na sura za kuvutia si mali kitu, havitawafaa hata kwa miaka dahari.
Mtafuteni Mungu atawaongoza, acheni michepuko,tulieni na wake zetu.
Ujumbe huu uwafikie
@Asprin Mentor, KakaKiiza, Kaizer, Ntuzu, mwekundu, mayenga, ayanda, Kiranga, Nyani Ngabu
Not how much you have but how much you enjoy,
hakika masikini ni mwenye furaha zaidi ya tajiri
Eccleciates 10:19 - A feast is made for laughter, and wine maketh merry: but money answereth all things.