baba-mwajuma
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 4,178
- 7,591
Mfano sisi Tanga, Hatujawahi toka top 10 pato la tafia na sometime tupo top 5, tuna maviwanda makubwa makubwa toka enzi na enzi mpaka leo yana lipa mamaia ya mabilioni ya kodi, ila bajeti ya manispaa hapa mjini utasikia ni 70B, hela zinazozalishwa na mkoa zinaendeleza mikoa mingine, hio barabara ya horohoro mpaka kujengwa ilikua ni mbinde na ni barabara kubwa ilikua, ukienda Pangani ndio unaweza ukalia barabara mbovu kupita maelezo sehemu ambayo unaelekea kwenye mbuga, hotel kubwa za kitalii.Ili kuwe na miundombinu lazima kuwe na sababu ya kuweka hiyo miundombinu kaka.
Hata hiyo Morogoro ambayo sasa hivi ni miongoni mwa mikoa inayokua jwa kasi hawakulimbikiziwa tu miundombinu ndio watu wakajaa kaka.
Kuna vitu vilivutia watu na ongezeko la watu likavutia uanzishwaji wa miundombinu wezeshi kwaajili ya hao watu.
Kaskazini yote Tanga ndio inaongoza kuichangia Pato la Taifa ila barabara zinazojengwa Moshi vijinini na ukicompare na Tanga ni mbingu na Ardhi.
Nchi hii kuna watu wanazalisha pato la Taifa lakini wanachozalisha hakitumiki kuwanufaisha wao,
same kwa hao Wapemba, Tunapoongelea pato kubwa la Zanzibar huwezi kuacha kuongelea karafuu, Mikarafuu mingi ipo Pemba kuliko Unguja, Mikarafuu wa Pemba unafika hadi mita 15 na ukishapanda unavuna kwa miaka hadi 50, ni cash generating machine,
Hili pato la Zanzibar kwa jumla na karafuu mauzo ya nje
Mfano hapo 2021
-Jumla ya Pato ni dola milioni 72
-Pato la karafuu ni dola milioni 46
Hapo ina maana kama asilimia 60 ya pato la Taifa mauzi ya njehutokana na karafuu ambayo kwa kiasi kikubwa hutoka Pemba, Wapemba hawaruhusiwi kuuza hii kaarufu bali serikali ya mapinduzi ndio inauza, kwa lugha nyengine serikali ya mapinduzi kwa kiasi kikubwa pato lake inatoka Pemba.
Je ni sawa Pemba kunyimwa miundombinu kwenye hili pato ambalo kwa kiasi kikubwa no wao wamelitengeneza?