Mfanyabiashara ahukumiwa kunyongwa Dar, alimuua mdai wake aliyempa hela amuagizie Fuso

Similar scenario imetokea huku kwetu mzee mstaafu aliagiza fuso kwa kumtumia mtoto wa rafiki yake 2018. Mzee kidogo adhulumiwe kabisa fuso imeletwa 2022 mwezi wa 8... Jamaa kamletea mzee baada ya kushinikizwa sana ase. Na fuso lenyewe kamletea namba AZ_.

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba nyumba anapoishi mzee kumetokea attempts mbili za kuichoma. Mara ya kwanza walichoma nyumba ya jirani yake ambaye ni mstaafu pia na ana gari ya mizigo pia. Hii iliungua kabisa yani kila kitu, lakini mchomaji alikosea nadhani hakuwa mwenyeji wa haya maeneo yetu.

Baada ya siku moja kupita, Attempt ya pili ilikuwa kwenye target yenyewe lakini nyumba ya mzee ilipona miraculously. Walichoma milango lakini moto haukukolea hadi ndani walijaribu kuchoma mbao za kenchi lakini ilishindikana.

Matukio yote haya yalifanywa wakati wa usiku watu wakiwa wamelala.

Inasemekana huyo jamaa alipewa hela ya kununua fuso yenye ubora lakini ndo hivyo kamletea mzee wa watu garasa na kumpa presha za kuchomewa nyumba.
 



Huyo jamaa muuuaji alipewa pesa na marehemu sh 35 millions taslim,
Jamaa amuagizie gari toka nje.

Baada ya kimya kingi, marehemu akaanza kusumbuana Kwa simu kutaka pesa zake..

Siku moja muuaji akampigia simu marehemu aje afate chake pale kwake,

Kumbe muuaji alikuwa ameshaandaa shimo hapo nyumbani alipopanga,

Marehemu bila kujua akajipeleka mwenyewe nyumbani Kwa mdeni wake,
bila kujua kaandaliwa shimo la kuchomwa na kuzikwa humo.

Inasemekana marehemu aliuawa akiwa ndani ya nyumba na baadae akachomwa moto na akazikwa uani humo, huku akiwa amezungushiwa godoro mwili mzima na kuchomwa akiwa shimoni humo, na baadae muuaji alimfukia na kusakafia sakafu na cement Ili asigundulike Kwa urahisi.


Ilipita miezi kadhaa ndiyo muuaji akahama nyumba hiyo bila hata kumaliza Kodi yake,

--Siku moja mpangaji mpya aliyehamia ktk nyumba Ile akawa anapaki gari yake pale pale jamaa alipofukiwa.
Ndy akagunduwa kwamba eneo lile Kuna sehemu panatitia,

Jamaa akapata mashaka maana Ile sehemu ilikuwa imesakafiwa vizuri sana na ni eneo lote la uani,
Iweje pale tu pavunjike? Na kunaonekana Kuna dalili za shimo.

Jamaa akaamua kwenda kutoa riporti kwa Mjumbe na baadae polisi.

Jamaa walipokuja wakavunja lile eneo lililotitia na baadae wakakuta mabaki ya mwili ambao tayari ulikuwa umeshaharibika vibaya sana.

Kilichowashangaza zaidi ni kuona maiti Ile,
Ikiwa imeunguzwa na kuteketea kabisa lakini bado Kuna mabaki ya godoro mwilini mwake huku akiwa ameungua vibaya sana hata kushindwa kutambulika kabisa.

Ndiyo hapo mwenye nyumba akakumbuka kwamba yule mpangaji aliyopita alizungumzia mambo ya kuchimba shimo na kutapisha choo.

Lakini mbona hakuna dalili za kutapisha choo?

Ikabidi jamaa aitwe na mwenye nyumba, jamaa muuaji bila kutambua chochote aliitikia wito na kukamatwa on the scene.

Jamaa muuaji baada ya kutiwa mbaroni akafunguka tukio zima.

Ukweli ni kwamba muuaji ndiye aliyekuwa anadaiwa na marehemu..
 
Rudi tena ukasome biblia umechanganya habari
 
kesi kama hii iliwatoe kanda ya kati.

Na nyingine kama hii ipo kanda ya kati tenba, tofauti ni kuwa hawa bado hawajauana. Ila tayar washazuruminiana. Ni ndugu na jamaa wa karibu kabisaaaaaaaaaaaaaaaaa.


Dunia hii iman ime kwisha, ................................
 
Ndg kirahs hivyo unasurrender, hUyo alishakuwa na roho ya kuua na alishajipanga kumpiga. Si rahis kumvungia Mtu unayemdai Chako Hasa pesa nyingi kia's hicho
 
Mara nyingi mauaji yoyote huwa lazima yaache alama ama viashiria vya kuanzia upelelezi!

Ingawa kabla ya kutekeleza mauaji hayo, watu hujidanganya kuficha tukio, lakini hawawezi kuziba mianya yote jambo hilo lisiweze kujulikana milele!
Una elimu ya upelelezi. Nafurahi kule Marekani mafaili hayafungwi.Watu hukamatwa zaidi ya miaka 50 mbele.
 
Hasa hivi ndivyo ilivyokuwa maana hata Clouds kipindi cha Gea waliifatilia sana hii habari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…