Mfanyabiashara aliekuwa anakataa elfu tisini kuuza jezi mpya ya Yanga sasa anatafuta watu wa kununua jezi kwa elfu 55 na Raia wamemgomea

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Nimewahi kuandika hapa kwamba mbantu hawezi kufanya biashara kwa sababu huwa anashindwa kujitofautisha yeye na biashara yake. He think he is his business.

Kwa mfano akiwa anauza bidhaa fulani halafu watu wakawa wanaigombania sana yeye atadhani kwamba hao wateja wana mshobokea yeye na sio kwamba wanahitaji bidhaa anayouza.

Mfano mzuri tazama makonda wa daladala muda ambao hakuna abiria wengi wanaita wateja hadi huruma ila ufike muda wa jioni sasa wanaanza kudengua kama watoto wa kike yani wanahisi kama abiria wanawashobokea wao vile.

Back 2 topic, jezi mpya ya Yanga ilivyo toka, Yanga wenyewe walikuwa wanauza 50 kwa jezi na walikuwa wanauza jangwani tu.

Walanguzi kama kawaida wakawa wazinunua then wanauza kuanzia 70 hadi laki moja hasa ile ya rangi ya dhahabu.

Kitaani kwetu kuna jamaa ana duka alikuwa anauza jezi ya rangi ya dhahabu laki moja . Hizi nyingine anauza mwisho 70 hapunguzi.

Hiyo ya rangi ya dhahabu watu wameenda mpaka na tisini eti hataki anataka laki moja.

Haya sasa mechi ya jana Yanga kapigwa kifala Raia wamekasirika jezi wamechana na kuchoma moto na sidhani kama watakuwa wanaenda tena uwanjani.

Leo jamaa wa duka kashusha anauza elfu hamsini na 5 jezi na watu hawanunui wala nini wanasema hata bure hawawezi kuvaa jezi..

Wafanyabiashara muwe mnasoma alama za nyakati.
 
Nimecheka sana aisee
 
Wewe unashinda hapo dukani ujue anauza laki, rangi nyingine mwisho 70, then ujue kuna mtu alienda na tisini jamaa akamkazia!
Leo tena umeshajua ameshusha bei anauza 55 na wateja wamesusa hawanunui tena na hawatonunua !

Kama sio mlozi basi utakuwa mtume au nabii
Nilienda na tisini akakakataa namshukuru kwa sababu hata ningenunua ningechoma jezi moto.

Leo kaweka bango la sales
 
Biashara hutoa shule kwa vitendo, Huyo amepata somo zuri, kadri anavyopata somo ndivyo anavyopaswa kujirekebisha na ndivyo utajiri unavyomnyemelea.
 
Nimewahi kuandika hapa kwamba mbantu hawezi kufanya biashara kwa sababu huwa anashindwa kujitofautisha yeye na biashara yake. He think he is his business.

Kwa mfano akiwa anauza bidhaa fulani halafu watu wakawa wanaigombania sana yeye atadhani kwamba hao wateja wana mshobokea yeye na sio kwamba wanahitaji bidhaa anayouza.

Mfano mzuri tazama makonda wa daladala muda ambao hakuna abiria wengi wanaita wateja hadi huruma ila ufike muda wa jioni sasa wanaanza kudengua kama watoto wa kike yani wanahisi kama abiria wanawashobokea wao vile.

Back 2 topic, jezi mpya ya Yanga ilivyo toka, Yanga wenyewe walikuwa wanauza 50 kwa jezi na walikuwa wanauza jangwani tu.

Walanguzi kama kawaida wakawa wazinunua then wanauza kuanzia 70 hadi laki moja hasa ile ya rangi ya dhahabu.

Kitaani kwetu kuna jamaa ana duka alikuwa anauza jezi ya rangi ya dhahabu laki moja . Hizi nyingine anauza mwisho 70 hapunguzi.

Hiyo ya rangi ya dhahabu watu wameenda mpaka na tisini eti hataki anataka laki moja.

Haya sasa mechi ya jana Yanga kapigwa kifala Raia wamekasirika jezi wamechana na kuchoma moto na sidhani kama watakuwa wanaenda tena uwanjani.

Leo jamaa wa duka kashusha anauza elfu hamsini na 5 jezi na watu hawanunui wala nini wanasema hata bure hawawezi kuvaa jezi..

Wafanyabiashara muwe mnasoma alama za nyakati.

Mfanyabiashara apewe maua yake. Kukaa na stock na kuiangalia tu ni level ya juu kabisa ya kufanya biashara
 
Back
Top Bottom