Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣🤣🤣Hii mbona imekaa kimkakati zaidi? Waziri wa Fedha gani hashauriki, yaani hao wafanyabiashara gani walimshauri?
kamachana na Ashatu Kijaji, kanifurahisha sana pedezhee Chuki ShabanMwenyekiti wa wamiliki wadogo na wa kati wa malori amenifurahisha sana ...amemchana live mwigulu mchemba
Naona na wewe umeiga kusoma kwake kwa kuandika kama yeye!!Huyu darasa la ngapi ajui ata kuxoma vixuri
Huyo mama haondolewi kwa poroja za wapumbavu. Yaan mpuuzi mmoja huko apangwe la kusema then waziri aondolewe?Ashatu Kijaji hana shughuli mpaka saizi, asante sana Chuki Shabani mzee wa Tabata.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Nchi inakusanya kodi wewe unasema hawaaminiki?Mwigulu, kijaji hawaaminiki kwemye nafasi zao ni vizuri wajiuzulu wenyewe maana wamekuwa failures kwenye wizara zao
Yeye mwenyewe si alishasema yeye ni dokta wa uchumi hataki ushauriHii mbona imekaa kimkakati zaidi? Waziri wa Fedha gani hashauriki, yaani hao wafanyabiashara gani walimshauri?
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, leo Mei 17, 2023.
Wafanyabiashara hao wametoa malalamiko mbele ya Waziri Mkuu ambapo wameilaimu TRA kwa kutokufuata taratibu sahihi za utozaji kodi wakishirikiana na Jeshi la Polisi.
Mfanyabiashara mmoja akitoa malalamiko yake amesema kampuni yake imewahi kusumbuliwa na Askari wa Kituo cha Kamata akidaiwa kutokuwa na risiti halali za mizigo yake, jambo ambalo sio la kweli. Pia, amemtaja kwa jina moja Askari anayehusika na kashfa nyingi za hapo kuwa ni "Mpemba"
Aidha, mfanyabiashara mmoja aliyesimama kwa niaba ya wafanyabiashara wa Vitenge amemhoji Waziri Mkuu kama Serikali haitaki wanawake nchini wapendeze maana wamekuwa wanachukuliwa kama wanauza madawa ya kulevya.
Wamewalamumu pia watu wanaohusika na uzoaji wa taka kuwa wanadai pesa zisizotakiwa, kwani huenda hadi kwenye stoo zao. Pia, watu wa TRA wamekuwa wanawafata hadi majumbani wakitaka pesa. Mama huyo amehoji, "Kwa hiyo tukadange?, hapa sio mahali sahihi kwa kuongea, nitahatarisha maisha yangu. Nipe namba nije chemba tuzungumze"
Kuhusu sababu ya kufunga maduka, mfanyabiashara mmoja amesema walifanya hivyo kutokana na;
Kero nyingine iliyotajwa ni maafisa wa TRA kuwa na mamlaka makubwa ya kukadiria faini za malipo pindi wanapowakatama wafanyabiashara kwa makosa mbalimbali, ambayo mengi ni ya kusingiziwa. Jambo hili huleta mianya ya rushwa kwa sababu TRA huwaalika kwa mazungumzo ya pembeni kinyume cha taratibu.
- Uwepo wa utitiri wa kodi usioendana na uhalisia, "Double Taxation"
- Kuhamia kwa maduka barabarani kwa jina maarufu la machinga, watu ambao wamekuwa wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa hivyo kubana biashara zao (wafanyabiashara waliosajiliwa). Duniani kote hakuna machinga kwenye vituo halisi vya kibiashara
- Adhabu za makosa ya kutolipa kodi zisizolipika sababu ya ukali wake hivyo kuweka mianya ya rushwa
Pia, urasimu kwenye mamlaka za serikali hasa utoaji wa leseni, kupandishwa kila mwaka kwa makadirio ya kodi kwa lugha maarufu ya "Maelekezo kutoka juu", kodi kubwa ya fremu za biashara, mfumo mbovu wa kodi ya forodha bandarini pamoja na kamatakamata za aina mbalimbali zinazofanyika sokoni hapo.
Hoja nyingine iliyoibuliwa ni Matamshi ya Waziri Mwigulu Nchemba kudharau wabunge wengine ambao ni wawakilishi wa wananchi, amekuwa na kauli chafu zinazokatisha tamaa wafanyabiashara, mfano ni ile ya kuwa yeye ni daktari wa uchumi, hawezi kubishana na waganga wa kienyeji.
Mfanyabiashara huyo amesema jeuri yote ya TRA inasababishwa na Waziri wa fedha ambae ni bosi wao mwenye jeuri, hashauriki, haambiliki. Pia, mfanyabiashara huyo amesema Waziri Nchemba hafai kuwepo kwenye nafasi yake.
Waziri wa Biashara amelaumiwa pia kwa kutosimama na wafanyabiashara hasa kwa kauli yake ya Bungeni kuwa hakukuwa na mgomo kariakoo.
Tulia wewe kama una maslahi nae jiandae ugali ushamwagwaRais hasikilizi porojo za mitaani, kuna watu wanafanya analysis, kuna wawekezaji wakubwa nk, sio muuza mifuko wa Kariakoo anaropoka tu.
Ukute hapa ASHANTU hajawahi kumuona anafananaje.
Wapumbavu hamuwezi kujificha ushujaa wake ni nini? Wakati wa shetani Mwigulu hakuwa waziri?Ni jambo jema sana tena mno!
Nafuatilia mubashara TBC kiukweli angekuwepo Shujaa Magufuli kwa haya maelezo ya Wafanyabiashara Waziri angeliwa kichwa fasta!
Haya mbwiga!Wapumbavu hamuwezi kujificha ushujaa wake ni nini? Wakati wa shetani Mwigulu hakuwa waziri?
Kumbe ndio maana alikuwa anawasaliti wenzake mnafiki huyu? CCM hawawezi kuwa fairView attachment 2625114Mwenyekiti wa wafanya biashara😁
Wewe mbuzi utamshauri nini sasa? Sio kila mtu anaweza kumshauri Waziri wa Fedha bhana.Yeye mwenyewe si alishasema yeye ni dokta wa uchumi hataki ushauri