Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Hao wafanyabiashara wanacheza "mbago" za kisiasa....Mh.Mwigulu anaingiaje katika madai yao ?!!!

Kwamba madai yao hayo yameanza kipindi mh.Nchemba akiwa waziri wa fedha ?!!![emoji15][emoji15]
Na wewe ni chawa wa Mwigulu? huoni tatizo la huyo mtu wenu?

Mwigulu na January Makamba mama awaondowe haraka hawa wahuni kuleta taswira nzuri ya serikali yake.
 
Sina mengi Ndugu zangu.

Leo wafanyabiashara wa kariakoo wamefunguka mengi Sana kuhusu masaibu wanayopitia, haya yamenifanya walau niandike ku share nawe.

1. Wamediliki kusema nchi hii waziri wa VIWANDA Hafai kuendelea na nafasi hiyo. Amewapuuza Bungeni pale mbunge alipo omba bunge lisitishe shughuli zingine kujadili kufungwa kwa maduka kariakoo.ueue alisema maduka yamefunguliwa ila machache yamefungwa
2. Wamesema waziri WA FEDHA ndiyo chanzo cha haya yote kwasababu wao kila wakitoa mapendekezo Yao hayafanyii kazi. Anawapuuza wabunge wenzake kwa kuwaita waganga wa jadi.
3. Wamelalamika kusikia Kuna FEDHA trioni 2 zimepigwa kwa mjibu wa ripoti ya CAG, hivyo inawavunja moyo wafanyabiashara kulipa Kodi ilihali FEDHA inapigwa.

Mtazamo wangu, hii ndiyo Tanzania ninayoitaka,wananchi 🇹🇿 kufuatilia kwa makini Kauli za viongozi wao pamoja na tabia zao kuwa na ujasiri wa kuongea bila uoga mambo yanayogusa maisha Yao ...NB, tukienda hivi nchi tutaikomboa kwani , kitendo cha wana KARIAKOO kukataa kuongea na waziri mkuu kwenye ukumbi uliopendekezwa na kutaka aje mnazi MMOJA nimependa.

Aluta continua
 
Waziri mkuu kafanya jambo jema sana...watu wengi wanaosumbua wafanyabiashara ni watu wasiojua biashara ila wamesomea jinsi ya kumfuatilia na kumnyonya mfanyabiashara. Leo namuona Ndugu msomi PhD holder akiambiwa mambo makubwa ya ukweli. Itoshe kusema Mwigulu anacho kiburi na dharau sana...kushindwa kuwasikiriza watu ambao wako chini yako au idara yako ni kosa kubwa sana...Sisemi aondolewe ila afai tena hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…