Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Mwigulu kama ataendelea kubaki waziri kweli nitathibitisha kuna watu wana roho pea mbili

..anayetoza kodi ni Rais Ssh.

..anayeteua Kamishna Mkuu wa Tra ni Rais Ssh.

..kwanini mnakwepa kuelekeza lawama kunakohusika?
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, leo Mei 17, 2023.



Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo wametoa malalamiko mbele ya Waziri Mkuu ambapo wameilaimu TRA kwa kutokufuata taratibu sahihi za utozaji kodi wakishirikiana na Jeshi la Polisi.

Mfanyabiashara mmoja akitoa malalamiko yake amesema kampuni yake imewahi kusumbuliwa na Askari wa Kituo cha Kamata akidaiwa kutokuwa na risiti halali za mizigo yake, jambo ambalo sio la kweli. Pia, amemtaja kwa jina moja Askari anayehusika na kashfa nyingi za hapo kuwa ni "Mpemba"

"Kuna Askari anaitwa Mpemba hapo Kamata amenipelekesha sana, pia kuna mwingine mweusi yuko hapohapo wanatupelekesha sana. Inashangaza sana Askari wanakusumbua kama vile TRA hadi unajiuliza kazi ya TRA inafanywa na Askari"

Ameendelea, "Kwa kuwa umesema tufunguke, niseme Nchi hii hadi Polisi ni wezi mno, hakuna wakati mgumu kufanya biashara kama wakati huu, tunaiwezesha Nchi lakini wanatukatisha tamaa

Ameongeza, "Tufanye mabadiliko makubwa ili twende mbele, mengine siwezi kusema hapa, nikiyasema watanikamata, nawajua hawa"

Aidha, mfanyabiashara mwingine aliyesimama kwa niaba ya wafanyabiashara wa Vitenge amemhoji Waziri Mkuu kama Serikali haitaki wanawake nchini wapendeze maana wamekuwa wanachukuliwa kama wanauza madawa ya kulevya.

Wamewalamumu pia watu wanaohusika na uzoaji wa taka kuwa wanadai pesa zisizotakiwa, kwani huenda hadi kwenye stoo zao. Pia, watu wa TRA wamekuwa wanawafata hadi majumbani wakitaka pesa. Mama huyo amehoji, "Kwa hiyo tukadange?, hapa sio mahali sahihi kwa kuongea, nitahatarisha maisha yangu. Nipe namba nije chemba tuzungumze"

Kuhusu sababu ya kufunga maduka, mfanyabiashara mmoja amesema walifanya hivyo kutokana na;
  1. Uwepo wa utitiri wa kodi usioendana na uhalisia, "Double Taxation"
  2. Kuhamia kwa maduka barabarani kwa jina maarufu la machinga, watu ambao wamekuwa wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa hivyo kubana biashara zao (wafanyabiashara waliosajiliwa). Duniani kote hakuna machinga kwenye vituo halisi vya kibiashara
  3. Adhabu za makosa ya kutolipa kodi zisizolipika sababu ya ukali wake hivyo kuweka mianya ya rushwa
Kero nyingine iliyotajwa ni maafisa wa TRA kuwa na mamlaka makubwa ya kukadiria faini za malipo pindi wanapowakatama wafanyabiashara kwa makosa mbalimbali, ambayo mengi ni ya kusingiziwa. Jambo hili huleta mianya ya rushwa kwa sababu TRA huwaalika kwa mazungumzo ya pembeni kinyume cha taratibu.

Mfanyabiashara huyo amesema, "TRA wanatufuata mpaka nyumbani jamani, tunaomba namba wakija ili tuwatumie picha, wanatutishia wanazuia Biashara zetu, kwanini watufuate nyumbani? Waziri Mkuu siwezi kukwambia kila kitu, hapa sio sehemu salama nipe namba nikufuate chemba, la sivyo nitahatarisha Maisha yangu

Ameendelea, "Kuna kodi mpya ya Stoo ambayo inaelekeza ukikutwa na kosa unapigwa faini ya Tsh. Milioni 4. Kodi hiyo inatengeneza mazingira ya Rushwa na hatujui kama ipo kihalali au la.

Ameongeza, "Mfanyabiashara hauwezi kukamatwa kwa Mwezi mara tatu, inabidi mzungumze pembeni"

Pia, urasimu kwenye mamlaka za serikali hasa utoaji wa leseni, kupandishwa kila mwaka kwa makadirio ya kodi kwa lugha maarufu ya "Maelekezo kutoka juu", kodi kubwa ya stoo za bidhaa, mfumo mbovu wa kodi ya forodha bandarini pamoja na kamatakamata za aina mbalimbali zinazofanyika sokoni hapo.

Hoja nyingine iliyoibuliwa ni Matamshi ya Waziri Mwigulu Nchemba kudharau wabunge wengine ambao ni wawakilishi wa wananchi, amekuwa na kauli chafu zinazokatisha tamaa wafanyabiashara, mfano ni ile ya kuwa yeye ni daktari wa uchumi, hawezi kubishana na waganga wa kienyeji.

Mfanyabiashara huyo amesema jeuri yote ya TRA inasababishwa na Waziri wa fedha ambae ni bosi wao mwenye jeuri, hashauriki, haambiliki. Wamewahi kuzungumza nae mara kadhaa lakini hajawahi kutekeleza hoja za mazungumzo hayo. Pia, mfanyabiashara huyo amesema Waziri Nchemba hafai kuwepo kwenye nafasi yake.

Waziri wa Biashara amelaumiwa pia kwa kutosimama na wafanyabiashara hasa kwa kauli yake ya Bungeni kuwa hakukuwa na mgomo Kariakoo. Wafanyabiashara hao wamesema kuwa haijawahi kutokea hata mara moja Waziri huyo akasimama na wafanyabiashara.

Urasimu mkubwa wa mizigo inayotoka Zanzibar umetajwa kuwepo tofauti na wafanyabiashara wanaotoa mizigo nchi zingine kama Dubai n.k. Pia, kumekuwepo na watu wengine wanaotoza kodi baada ya kutoa mzigo bandarini, watu hao wanapaswa kuwepo bandarini ili kurahisisha uliopaji wa kodi na kuokoa muda.

Mfanyabiashara mwingine amesema TRA wamepewa mamlaka ya kuomba rushwa kisheria, kwa kuwa wanalindwa na Sheria mbovu, wanataka rushwa kwa nguvu. "Rushwa ni mfumo, na sheria inawalinda. Wanatumia loophole ya elimu ndogo ya wafanyabiashara kudai rushwa....."

Mfanyabiashara wa vitenge ametoa dukuduku lake la kudaiwa kodi zaidi ya bilioni 30, kisha baadae kutakiwa kulipia bilioni 10.3 ambazo hajalipa hadi leo. Baada ya kushindwa kulipa alitakiwa kupelekwa mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi kisha kutakiwa walau moja ya tatu ya gharama zote (3.4 bilioni) wakati hajafanya kazi kwa zaidi ya miezi 8 na kontena zake 10 za vitenge zimekamatwa na TRA Ubungo.
Wafanyabiasha Wanasema matatizo yote ni Kwa Sababu viwango vya Kodi vilivyowekwa na serikali hii Chini ya Mwigulu havitekelezeki.
 
We unafikiri hii changamoto haikuwepo kipindi cha Magufuli?

Utofauti unaofanya uone haikuwepo ni kwamba kile kipindi isingewezekana kufanya mgomo kutokana na udikteta wa Magufuli
Inakuaje sasa katika awamu ya kufanya biashara kwa uhuru na uwazi bila bughudha na mama hapendi kodi za dhuruma
Inakuwaje kutokee haya?
 
KWa huu mkutano ni wa kariakoo peke yako?
Hivi hujui kuwa mwenyekiti wenu ni mtu wa system?
Ukikua utajua nisemayo.
Kuna watu wanaongea kwa hisia na wewe kwa kutokujua kwako unaona wako upande wenu, hao wanatuliza upepo tu then kupigwa kutarudi pale pale[emoji23][emoji23]
Usikariri
 
Ni jambo jema sana tena mno!

Nafuatilia mubashara TBC kiukweli angekuwepo Shujaa Magufuli kwa haya maelezo ya Wafanyabiashara Waziri angeliwa kichwa fasta!
Usiwe mwepesi kiasi hicho kichwani.

Lawama hizi siyo za mtu mmoja, Waziri, ingawaje naye ni mchangiaji wa matatizo.

Hao waliosema mambo hapo, wamesema yanayohusu upande wao, hujasikia chochote toka upande wa pili. Ingefaa na wao wakasema kitu tukawasikia.

Wafanya biashara mahali popote duniani hakuna wanaopenda kulipa kodi stahiki. Kukiwa na mwanya, ni lazima watautumia tu kutolipa kodi.

Lawama inaiangukia serikali, inayoshindwa kuweka mfumo unaozuia haya wanayolalamikia wafanya biashara.

Na kwa serikali mbovu kama hii iliyopo sasa, matatizo haya ndiyo yanazidi kuonekana wazi zaidi.
 
Kodi ipi ya hovyo iliyowekwa? Kodi za hovyo alianzisha Magufuli. Kama hujui uliza. Yule Shetani bora alivyokufa maana hata uhuru huo wa wafanyabiashara haukuwepo.
Unapata tabu sana dogo awamu ya mama inapopolewa
 
Ukifanya biashara na ukawa na EFD, tena VAT registered utaelewa
Kwani nchi zingine hakuna mamlaka za mapato? Kwa nini shida ni Tanzania tu?

EFD kila siku unafunga hesabu, na kama una kampuni unalipa return kila mwezi au unajaza nil, tatizo liko wapi?
 
Back
Top Bottom