Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Naona wafanyabiashara wa usalama wa taifa wakiwawakilisha wafanyabiashara halisi wa kariakoo

Yaani watu wamepangwa kabisa waje kuelezea kero za wafanyabiashara vile iwapendezavyo viongozi wa serikali.
 
Wewe kweli huna akili hujasikia hapa Mwigulu anaongeza Kodi ovyoovyo bila kuongea na wafanyabiasha.wakati wa Magufuli kama kungekuwa na matatizo makubwa wafanyabiasha wangegoma Tu Kwa Sababu hakuna mwanasiasa anayeweza kuwazuia wafanyabiasha.alafu shetani ni wewe hapa unayesema uongouongo.yaani miaka 2 baada ya Magufuli kuondoka hawajagoma mpaka Leo Kwa Sababu ya Kodi za ovyoovyo zilizoongezwa na serikali yako ya ovyoovyo.

..mwenye mamlaka ya kutoza au kuongeza kodi ni RAISI.

..Waziri wa Fedha ni mtekelezaji wa maamuzi ya RAISI.
 
Eti mtu hakulipa kodi miaka 2 /3 iliyopita anatakaa asilipe kisa rais alisema,Serikali na Nchi ni kubwa kuliko Rais lipeni kodi acheni mzaha nyie nyie mkitoka hapo mnainanga serikali kuwa haifanyi kitu.
 
Kwamba wafanyabiasha wanaweza kuzuiwa na wanasiasa wasigome kweli huna akili?
Ndio mbona hili liko wazi sana nani unayemtegemea angethubutu?

Fikiria tu hiki kikao kingefanyika katika utawala wa Magufuli, ungemtegemea kumuona nani ambaye angekuwa ana point uozo wa viongozi kama Mwigulu bila hofu?

Nani angeweza?

Wakati Magufuli anakuja Chunya mkoani Mbeya kwenye ziara yake, kulikuwa kuna wananchi ambao walibeba mabango kuelezea kero ambazo zinaikumba wilaya yao lakinia TISS waliwakamata wale watu na kuwashushia vichapo, na yeye Magufuli alisema "hata mkilia mi siwaoni"

Wale watu walibebwa wakaenda kutupwa kule kona za mkoa wakiwa wamepigika

Achana na hilo

Siku ya meimosi Makonda alitoa kauli ya kuwatisha wafanyakazi kuhusu kunyanyua mabango ya kudai kuongezwa maslahi, sasa kwa uzito wa jambo hili nani angethubutu?
 
Back
Top Bottom