Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

..Ccm haiwasikilizi wananchi au wapigakura kwasababu hawategemei kura, bali hushinda uchaguzi kwa mbinu na mabavu.

..Serikali, wabunge, wakiwa wanapatikana kutokana na kura na uchaguzi wa haki basi utaona viongozi wanawasikiliza na kuwashirikisha wananchi ktk maamuzi mbalimbali.

..Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, wananchi wanaojielewa na kutambua haki zao, ndio suluhisho.
Ni Kwa namna gani katiba mpya itakusaidia?Kwa Sababu utakuwa katiba IPO na wanasiasa Wanavunja Tu kama kawaida.
 
kwa uzoefu wangu mdogo kwenye biashara.. Kodi huwa ni zile zile, ila biashara faida na hasara pamoja na mzunguko huwa haupo vile vile.. TRA kuna nafasi ya kukaa nao chini na hata kufanya makubalinao ( na ndio hapa wanafungua mwanya wa kukunyoosha sasa ).
Mkuu umemsikia Vunja Bei Jamaa anaongea madini Kama wewe.
 
Wangegomaje wakati bado raisi ni mpya na hivyo kuna hatua za kufanya kabla ya kufikia mgomo?

Unafikiri mgomo unaanza tu kwasababu ya matakwa ya watu?

Mgomo kuufikia ni baada ya kufanya taratibu zote za kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kuwaita viongozi kuwaomba watunge sheria mpya ambayo itakuwa fair.

Na hilo wamelisema kuwa waliwafikishia viongozi malalamiko yao ila baada ya kuona hakuna utekelezaji wakaamua wagome

Sasa utawala wa Magufuli nani angethubutu kugoma eti kwakua viongozi wamepuuza maombi yao?
Kwa hiyo wameishi kwa maumivu kwa miaka yote 2?

Basi wasingemlaumu Mwigulu namna hiyo bali wangemlaumu sana Mpango
 
Wanawarekodi kwa TV ili wawafuatilie na kuwabinya chini chini hii nchi mnaijua vizuri kweli au mnaisikia.Baada ya hapo hutasikia mgomo tena,Wataanza kutishwa waliowapangisha frames hao wafanya biashara hawa mapaka watawatoa mikataba ikiisha.
 
Hakuna mwanasiasa anayeweza kuwazuia wafanyabiasha wakigoma Kwa Sababu ya unyeti wao na matatizo mengi ya Kodi na tozo yametokea ndani ya serikali hii.
Kwa kiongozi yeyote anayefuata demokrasia hilo linawezekana

Dikteta hiyo nafasi hakupi
 
Mama amemkumbatia mwingilu kwa gharama na maumivu makubwa sana! Huyu jamaa kala matusi yakutosha kabisa hadharani, mbali na madudu yake hapo nyuma likiwamo la ndege yeye kama muhusika

Ifike mahala hata yeye alie bebwa ajitathimini na aone aibu, " ukibebwa tulia, sasa yeye anamtekenya alie mbeba kwa kiasi ambacho naona hata alie mbeba hawezi vumilia " amuachie tu aende asimkumbatie tena

Tumuonee huruma Raisi pia tuoneane huruma watanzania hii cake ya wote
img_5_1684079206955.jpg
 
Mkuu umemsikia Vunja Bei Jamaa anaongea madini Kama wewe.
Sijafanikiwa msikiliza mkuu, nipo hapa nafatilia comment.

TRA bado wanafanya kazi zaidi katika theory na sio practical, ingawa kuna baadhi ya maafisa wao ( wachache walio waadilifu) wanaelewa na hata mkikaa mezani mapata solution nzuri, ila ukikutana na vimeo unaweza funga biashara. Binafsi nilitelekeza Company kwa ajiri ya ubabe wao usio na tija na kubaki nafanya kazi kama consultancy tu, nipe changu nisepe basi. Mfumo wa company nilishapiga chini
 
Hakuna utofauti wowote wa faida. VAT unalipa wewe?

Unajua kweli hiyo VAT kiongozi wangu?
Kwanini mnunuzi akanunue kwenye VAT iwapo bidhaa hiyo hiyo inauzwa na asiye na VAT jirani hapo? Watu wanaogopa kufika M100 hawatoi risiti sababu ya hichi kitu ukiachilia mbali gharama za kutunza mahesabu.
 
Back
Top Bottom