Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

𝐁𝐨𝐫𝐚 𝐓𝐚𝐬𝐤 𝐟𝐨𝐫𝐜𝐞 𝐰𝐚𝐨𝐧𝐝𝐨𝐥𝐞𝐰𝐞 𝐧𝐢 𝐯𝐢𝐥𝐚𝐳𝐚
 
𝐊𝐚𝐳𝐢 𝐲𝐚 𝐣𝐞𝐬𝐡𝐢 𝐥𝐚 𝐩𝐨𝐥𝐢𝐬𝐢 𝐬𝐢𝐨 𝐤𝐮𝐤𝐮𝐬𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐤𝐨𝐝𝐢 𝐛𝐚𝐥𝐢 𝐧𝐢 𝐤𝐮𝐥𝐢𝐧𝐝𝐚 𝐫𝐚𝐢𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐥𝐢 𝐳𝐚𝐤𝐞
 
Wafanyabiashara wamewachana live Waziri wa Fedha Dr Mwigulu na Waziri wa Biashara Dr Kijaji kwamba udaktari wao hauna faida yoyote kwa Wafanyabiashara

Wamedai Mawaziri hao siyo Wasikivu na wanawadharau Wabunge wao

Source: Channel ten
Kwanza Kijaji anashangaa hata huyo Waziri Mkuu kwenda huko Kariakoo wakati yeye kama Qaziri mhusika alishatoa msimamo kuwa Kariakoo hakuna mgomo wala tatizo isipokia wafanyabiashara wanatumia haki yao ya kufungua au kutofungua Maduka.

Zaidi anawashangaa hao waliompa Ulaji kupitia nafasi ya Uwaziri.
 
Hakuna Rais aliyekuwa anawasikiliza watanzania kama Magufuli ni manyumbu wachache mmeaminishwa hivyo
Hapo juu nimetoka kuelezea namna wananchi walivyopigwa kwa kunyanyua mabango ambayo yalikuwa yanaelezea kero zao.

Hapo ilikuwa ni hotuba ya Magufuli mwenyewe na kuthibitisha hilo sio kama hakuona kinachofanywa na wale TISS.

Kipindi ambacho wanapigwa aisema kabisa kuwa "hata mkilia siwasikii"
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, leo Mei 17, 2023.



Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo wametoa malalamiko mbele ya Waziri Mkuu ambapo wameilaimu TRA kwa kutokufuata taratibu sahihi za utozaji kodi wakishirikiana na Jeshi la Polisi.

Mfanyabiashara mmoja akitoa malalamiko yake amesema kampuni yake imewahi kusumbuliwa na Askari wa Kituo cha Kamata akidaiwa kutokuwa na risiti halali za mizigo yake, jambo ambalo sio la kweli. Pia, amemtaja kwa jina moja Askari anayehusika na kashfa nyingi za hapo kuwa ni "Mpemba"

"Kuna Askari anaitwa Mpemba hapo Kamata amenipelekesha sana, pia kuna mwingine mweusi yuko hapohapo wanatupelekesha sana. Inashangaza sana Askari wanakusumbua kama vile TRA hadi unajiuliza kazi ya TRA inafanywa na Askari"

Ameendelea, "Kwa kuwa umesema tufunguke, niseme Nchi hii hadi Polisi ni wezi mno, hakuna wakati mgumu kufanya biashara kama wakati huu, tunaiwezesha Nchi lakini wanatukatisha tamaa

Ameongeza, "Tufanye mabadiliko makubwa ili twende mbele, mengine siwezi kusema hapa, nikiyasema watanikamata, nawajua hawa"

Aidha, mfanyabiashara mwingine aliyesimama kwa niaba ya wafanyabiashara wa Vitenge amemhoji Waziri Mkuu kama Serikali haitaki wanawake nchini wapendeze maana wamekuwa wanachukuliwa kama wanauza madawa ya kulevya.

Wamewalamumu pia watu wanaohusika na uzoaji wa taka kuwa wanadai pesa zisizotakiwa, kwani huenda hadi kwenye stoo zao. Pia, watu wa TRA wamekuwa wanawafata hadi majumbani wakitaka pesa. Mama huyo amehoji, "Kwa hiyo tukadange?, hapa sio mahali sahihi kwa kuongea, nitahatarisha maisha yangu. Nipe namba nije chemba tuzungumze"

Kuhusu sababu ya kufunga maduka, mfanyabiashara mmoja amesema walifanya hivyo kutokana na;
  1. Uwepo wa utitiri wa kodi usioendana na uhalisia, "Double Taxation"
  2. Kuhamia kwa maduka barabarani kwa jina maarufu la machinga, watu ambao wamekuwa wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa hivyo kubana biashara zao (wafanyabiashara waliosajiliwa). Duniani kote hakuna machinga kwenye vituo halisi vya kibiashara
  3. Adhabu za makosa ya kutolipa kodi zisizolipika sababu ya ukali wake hivyo kuweka mianya ya rushwa
Kero nyingine iliyotajwa ni maafisa wa TRA kuwa na mamlaka makubwa ya kukadiria faini za malipo pindi wanapowakatama wafanyabiashara kwa makosa mbalimbali, ambayo mengi ni ya kusingiziwa. Jambo hili huleta mianya ya rushwa kwa sababu TRA huwaalika kwa mazungumzo ya pembeni kinyume cha taratibu.

Mfanyabiashara huyo amesema, "TRA wanatufuata mpaka nyumbani jamani, tunaomba namba wakija ili tuwatumie picha, wanatutishia wanazuia Biashara zetu, kwanini watufuate nyumbani? Waziri Mkuu siwezi kukwambia kila kitu, hapa sio sehemu salama nipe namba nikufuate chemba, la sivyo nitahatarisha Maisha yangu

Ameendelea, "Kuna kodi mpya ya Stoo ambayo inaelekeza ukikutwa na kosa unapigwa faini ya Tsh. Milioni 4. Kodi hiyo inatengeneza mazingira ya Rushwa na hatujui kama ipo kihalali au la.

Ameongeza, "Mfanyabiashara hauwezi kukamatwa kwa Mwezi mara tatu, inabidi mzungumze pembeni"

Pia, urasimu kwenye mamlaka za serikali hasa utoaji wa leseni, kupandishwa kila mwaka kwa makadirio ya kodi kwa lugha maarufu ya "Maelekezo kutoka juu", kodi kubwa ya stoo za bidhaa, mfumo mbovu wa kodi ya forodha bandarini pamoja na kamatakamata za aina mbalimbali zinazofanyika sokoni hapo.

Hoja nyingine iliyoibuliwa ni Matamshi ya Waziri Mwigulu Nchemba kudharau wabunge wengine ambao ni wawakilishi wa wananchi, amekuwa na kauli chafu zinazokatisha tamaa wafanyabiashara, mfano ni ile ya kuwa yeye ni daktari wa uchumi, hawezi kubishana na waganga wa kienyeji.

Mfanyabiashara huyo amesema jeuri yote ya TRA inasababishwa na Waziri wa fedha ambae ni bosi wao mwenye jeuri, hashauriki, haambiliki. Wamewahi kuzungumza nae mara kadhaa lakini hajawahi kutekeleza hoja za mazungumzo hayo. Pia, mfanyabiashara huyo amesema Waziri Nchemba hafai kuwepo kwenye nafasi yake.

Waziri wa Biashara amelaumiwa pia kwa kutosimama na wafanyabiashara hasa kwa kauli yake ya Bungeni kuwa hakukuwa na mgomo Kariakoo. Wafanyabiashara hao wamesema kuwa haijawahi kutokea hata mara moja Waziri huyo akasimama na wafanyabiashara.

Urasimu mkubwa wa mizigo inayotoka Zanzibar umetajwa kuwepo tofauti na wafanyabiashara wanaotoa mizigo nchi zingine kama Dubai n.k. Pia, kumekuwepo na watu wengine wanaotoza kodi baada ya kutoa mzigo bandarini, watu hao wanapaswa kuwepo bandarini ili kurahisisha uliopaji wa kodi na kuokoa muda.

Mfanyabiashara mwingine amesema TRA wamepewa mamlaka ya kuomba rushwa kisheria, kwa kuwa wanalindwa na Sheria mbovu, wanataka rushwa kwa nguvu. "Rushwa ni mfumo, na sheria inawalinda. Wanatumia loophole ya elimu ndogo ya wafanyabiashara kudai rushwa....."

Mfanyabiashara wa vitenge (Mama Bonge) ametoa dukuduku lake la kudaiwa kodi zaidi ya bilioni 30, kisha baadae kutakiwa kulipia bilioni 10.3 ambazo hajalipa hadi leo.

Baada ya kushindwa kulipa alitakiwa kupelekwa mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi kisha kutakiwa walau moja ya tatu ya gharama zote (3.4 bilioni) wakati hajafanya kazi kwa zaidi ya miezi 8 na kontena zake 10 za vitenge zimekamatwa na TRA Ubungo.

===

UPDATE:
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Anazungumza

Amesema Serikali ya Samia Suluhu Hassan inayo dhamira ya dhati ya kuwasaidia wafanyabiashara wa Nchii kwa kuwasikiliza na kutatua matatizo yao.

Waziri Majaliwa amesema kikao hiki sio cha mwisho, bali vikao zaidi vitaendelea kufanyika ili kutatua kero na kuinua Sekta hii muhimu kwa uchumi wa Nchi.

Hoja zote zimechukuliwa na Serikali na zinaendelea kufanyiwa kazi kwa mfumo Shirikishi baina ya Serikali na wafanyabiashara wenyewe ikiwemo kuunda tume ya pamoja kati ya Serikali na wafanyabiashara. Timu hiyo itakuwa na watu 14, itapaswa kupitia na kuchukua yote yanayotekelezeka ili yafanyiwe kazi haraka, yanayohusu sheria yatapaswa kushughulikiwa bungeni haraka.

Amewataka Polisi kulinda usalama wa Raia na sio kujihusisha na kazi za TRA na task force hiyo imeondolewa.

Nasubiri mgomo wa waagizaji na wauzaji wa magari niwaunge mkono
 
Ni Kwa namna gani katiba mpya itakusaidia?Kwa Sababu utakuwa katiba IPO na wanasiasa Wanavunja Tu kama kawaida.

..Katiba iliyopo inalinda wale wanaoivunja na kuadhibu wanaoitetea.

..Kwa mfano kuna vipengele vibaya vinavyosema Raisi hatashtakiwi kwa lolote atakalofanya akiwa madarakani.

..Kwa hiyo Katiba inamlinda Raisi ktk kuivunja Katiba.

..Katiba iliyopo inasema masuala yanayohusiana na fedha au kodi ni lazima yapate ridhaa ya Raisi kabla hayajajadiliwa bungeni.

..Katiba mpya iweke kipengele kinachoruhusu mbunge yeyote kuwasilisha hoja binafsi kuhusu masuala ya fedha, kodi, na tozo.

..Pia katiba mpya iweke utaratibu sahihi na wa haki wa matumizi ya kodi ktk eneo kodi inapokusanywa. Kwa mfano, eneo lenye makusanyo makubwa ya kodi lipewe mgao wa haki wa kodi yao, na kiasi kingine kiende kusaidia maeneo yenye uhitaji.

..Katiba ya sasa hivi inaruhusu serikali kukusanya kodi maeneo mbalimbali na kuielekeza ktk matumizi ya anasa mfano manunuzi ya ma-V8, ujenzi wa mji mkuu mpya, etc bila kuzingatia mahitaji ya wananchi maeneo ilipokusanywa kodi.
 
Nimegundua JF imejaa kuku wa kizungu....wapambanaji wachache sana humu ndani
𝐰𝐞𝐤𝐚 𝐡𝐨𝐣𝐚 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐰𝐚𝐳𝐢 𝐢𝐥𝐢 𝐭𝐮𝐣𝐮𝐞 𝐡𝐮𝐨 𝐮𝐤𝐮𝐤𝐮 𝐮𝐤𝐨𝐣𝐞 𝐦𝐤𝐮𝐮 𝐬𝐢𝐨 𝐤𝐮𝐭𝐮𝐦𝐢𝐚 𝐦𝐚𝐧𝐞𝐧𝐨 𝐭𝐮.....𝐭𝐰𝐞𝐧𝐝𝐞 𝐤𝐰𝐚 𝐡𝐨𝐣𝐚
 
Asietoza VAT kwenye mauzo, na yeye awezi dai VAT ya kununulia.

Anaetoza VAT kwenye mauzo, na yeye anatakiwa adai kurudishiwa VAT aliyonunulia.

VAT sio kodi ya mfanyabiashara
Na ndo tatizo lingine. Kuna watu wana mzigo mkubwa hawana risiti za manunuzi inabidi awape machinga. Akiuza yeye kwa Tin yake hawezi claim VAT.

Halafu kuna wale sasa ambao input zao hazina VAT mfano hoteli ananunua nyanya, hoho, nyama kwa watu wasio VAT ila Output keshafika M100 anatakiwa kuwa VAT. Anaclaim vipi? Anajikuta anakwepa kutoa risiti.
 
Hapo juu nimetoka kuelezea namna wananchi walivyopigwa kwa kunyanyua mabango ambayo yalikuwa yanaelezea kero zao.

Hapo ilikuwa ni hotuba ya Magufuli mwenyewe na kuthibitisha hilo sio kama hakuona kinachofanywa na wale TISS.

Kipindi ambacho wanapigwa aisema kabisa kuwa "hata mkilia siwasikii"
𝐓𝐈𝐒𝐒 𝐬𝐚𝐦𝐚𝐡𝐚𝐧𝐢 𝐧𝐢 𝐮𝐬𝐚𝐥𝐚𝐦𝐚 𝐰𝐚 𝐓𝐚𝐢𝐟𝐚 𝐤𝐢𝐫𝐞𝐟𝐮 𝐜𝐡𝐚𝐤𝐞 𝐦𝐤𝐮𝐮 𝐬𝐚𝐦𝐚𝐡𝐚𝐧𝐢
 
Back
Top Bottom