Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Ni jambo jema sana tena mno!

Nafuatilia mubashara TBC kiukweli angekuwepo Shujaa Magufuli kwa haya maelezo ya Wafanyabiashara Waziri angeliwa kichwa fasta!
Malalamiko yalikuwepo hata wakati wa shujaa wako, hatukuona waziri akifukuzwa. Hivyo, acha unafiki. Kuongea kote huko ni sababu ya uhuru alioutoa mama.
 
Swala la bulk shipping au sijui consolidation ni simple serikali imchukulie muagizaji kama supplier anaewauzia mzigo retailers wa kariakoo.

Yeye ndio atoe receipt za mauzo kwa hao retailers awatoze VAT ya mzigo wao, na yeye akadai VAT aliyolipia bandarini and value chain starts for him mzigo ukishaingia Tanzania.

Shida hapo sasa itakuja baadhi ya hao waagizaji kuna makontena wanayotoa bila ya kulipia ushuru na awataki kuwa traced.
 
Ukifanya biashara utaelewa. Mfano mpo 30, mmeagiza mzigo China ili kujaza contena, mzigo unapita kwa tin moja pale bandarini. Mkishagawana mzigo unatoa wapi risiti yenye tin yako?
mbona hiyo inawezekana wanafanya prorata ya kodi ili kila mfanyabiashara awe na risiti yake ya kodi anayolipia mzigo wake.
 
Kuna watu wanapanda jukwaani sidhani kama ni wafanya biashara maana wanazomewa kabisa, ni kama wanaenda kupoteza muda na hata wanavyoongea ni kama kuwafanya wafanyabiashara waonekane hawajui wanataka nn.
Majasusi hao wabobezi- TISS..CCM ni dhiki kuu
 
mbona hiyo inawezekana wanafanya prorata ya kodi ili kila mfanyabiashara awe na risiti yake ya kodi anayolipia mzigo wake.
Umeshaagiza mzigo kupitia mtu wa tatu ukafanya hiyo prorata?
Mkuu embu tuachane na hili hatutaelewana sababu unasema jambo ambalo ni nadharia maana moja ya tatizo la mfumo ambalo hata W/mkuu kalikubali leo ni hili.

Tukubali kutokukubaliana kuwa ukiwa na mzigo bila risiti wewe ni mhujumu uchumi kama unavyosema.
 
Hongereni wafanyabiashara mmetema cheche kweri kweri, mmetuwakilisha vyema.

Na sisi wengine tugome ajenda iwe matumizi ya kodi zetu sahihi ya kodi zetu. 😝

Kodi ni msingi wa maendeleo, tulipe na tuilinde kwa wivu mkubwa sana.
Ni mara ya kwanza nashuhudia mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, soko letu pendwa (baadhi). Vilevile mkutano kama huu wakitema cheche mbele ya Serikali. Hakika, kodi ni msingi wa maendeleo.
Roving Journalist shukran kwa thread na link
 
E4A5756B-99D4-4E96-B767-22B956048B28.jpeg
 
Back
Top Bottom