myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 166,767
- 705,461
SafiiiiPM amefanya kitu kizuri kusikiliza kero za wafanyabiashara....Naangalia hapa TBC na Channel 10.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SafiiiiPM amefanya kitu kizuri kusikiliza kero za wafanyabiashara....Naangalia hapa TBC na Channel 10.
SawasawaMgogoro unaoendelea ni kwamba wafanyabiashara hawapendi kulipa kodi kama zile wanazolipishwa wafanyakazi kwa jina la PAYE.
Serikali kama inawasikiliza wafanyakazi basi iwasikilize wafanyakazi pia.
1. Bill of landing inaorodha ya mizigo yote ndani ya container, so unapata total ya kodi zote kama ni different products zinapigwa kodi tofauti.Ukifanya biashara utaelewa.
Mfano 1. mpo 30, mmeagiza mzigo China ili kujaza contena, mzigo unapita kwa tin moja pale bandarini. Mkishagawana mzigo unatoa wapi risiti yenye tin yako?
Mfano 2. Una hoteli ww unahitaji hoho, biringanya, nyama n.k kwa wakulima wasio na risiti.
Mfano 3. Contractors, umeshawahi kupata tenda vijijini? Sehemu ambayo hakuna hardware kubwa zenye risiti za VAT? Unabakiwa na option mbili, either usafirishe cement zako au ukubali VAT ikuumize.
Ni sahihi, lakini kodi zimezidi mno, kila kona kodi alafu unalipia kitu kimoja. Ni vyema kungekuwa na mfumo mmoja, ukilipa hapo basi. Sheria zetu pia zilekebishwe zinaleta mazingira ya Rushwa.Somo la kodi lingeanzia chini kabisa primary huko.
Kama hujasoma mambo ya uhasibu na uchumi mambo ya kodi yanakupita kushoto, matokeo yake ukiingia uraiani mambo unakuta vururu kabisa yaani tofauti na mategemeo yako.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, leo Mei 17, 2023.
Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo wametoa malalamiko mbele ya Waziri Mkuu ambapo wameilaimu TRA kwa kutokufuata taratibu sahihi za utozaji kodi wakishirikiana na Jeshi la Polisi.
Mfanyabiashara mmoja akitoa malalamiko yake amesema kampuni yake imewahi kusumbuliwa na Askari wa Kituo cha Kamata akidaiwa kutokuwa na risiti halali za mizigo yake, jambo ambalo sio la kweli. Pia, amemtaja kwa jina moja Askari anayehusika na kashfa nyingi za hapo kuwa ni "Mpemba"
"Kuna Askari anaitwa Mpemba hapo Kamata amenipelekesha sana, pia kuna mwingine mweusi yuko hapohapo wanatupelekesha sana. Inashangaza sana Askari wanakusumbua kama vile TRA hadi unajiuliza kazi ya TRA inafanywa na Askari"
Ameendelea, "Kwa kuwa umesema tufunguke, niseme Nchi hii hadi Polisi ni wezi mno, hakuna wakati mgumu kufanya biashara kama wakati huu, tunaiwezesha Nchi lakini wanatukatisha tamaa
Ameongeza, "Tufanye mabadiliko makubwa ili twende mbele, mengine siwezi kusema hapa, nikiyasema watanikamata, nawajua hawa"
Aidha, mfanyabiashara mwingine aliyesimama kwa niaba ya wafanyabiashara wa Vitenge amemhoji Waziri Mkuu kama Serikali haitaki wanawake nchini wapendeze maana wamekuwa wanachukuliwa kama wanauza madawa ya kulevya.
Wamewalamumu pia watu wanaohusika na uzoaji wa taka kuwa wanadai pesa zisizotakiwa, kwani huenda hadi kwenye stoo zao. Pia, watu wa TRA wamekuwa wanawafata hadi majumbani wakitaka pesa. Mama huyo amehoji, "Kwa hiyo tukadange?, hapa sio mahali sahihi kwa kuongea, nitahatarisha maisha yangu. Nipe namba nije chemba tuzungumze"
Kuhusu sababu ya kufunga maduka, mfanyabiashara mmoja amesema walifanya hivyo kutokana na;
Kero nyingine iliyotajwa ni maafisa wa TRA kuwa na mamlaka makubwa ya kukadiria faini za malipo pindi wanapowakatama wafanyabiashara kwa makosa mbalimbali, ambayo mengi ni ya kusingiziwa. Jambo hili huleta mianya ya rushwa kwa sababu TRA huwaalika kwa mazungumzo ya pembeni kinyume cha taratibu.
- Uwepo wa utitiri wa kodi usioendana na uhalisia, "Double Taxation"
- Kuhamia kwa maduka barabarani kwa jina maarufu la machinga, watu ambao wamekuwa wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa hivyo kubana biashara zao (wafanyabiashara waliosajiliwa). Duniani kote hakuna machinga kwenye vituo halisi vya kibiashara
- Adhabu za makosa ya kutolipa kodi zisizolipika sababu ya ukali wake hivyo kuweka mianya ya rushwa
Mfanyabiashara huyo amesema, "TRA wanatufuata mpaka nyumbani jamani, tunaomba namba wakija ili tuwatumie picha, wanatutishia wanazuia Biashara zetu, kwanini watufuate nyumbani? Waziri Mkuu siwezi kukwambia kila kitu, hapa sio sehemu salama nipe namba nikufuate chemba, la sivyo nitahatarisha Maisha yangu
Ameendelea, "Kuna kodi mpya ya Stoo ambayo inaelekeza ukikutwa na kosa unapigwa faini ya Tsh. Milioni 4. Kodi hiyo inatengeneza mazingira ya Rushwa na hatujui kama ipo kihalali au la.
Ameongeza, "Mfanyabiashara hauwezi kukamatwa kwa Mwezi mara tatu, inabidi mzungumze pembeni"
Pia, urasimu kwenye mamlaka za serikali hasa utoaji wa leseni, kupandishwa kila mwaka kwa makadirio ya kodi kwa lugha maarufu ya "Maelekezo kutoka juu", kodi kubwa ya stoo za bidhaa, mfumo mbovu wa kodi ya forodha bandarini pamoja na kamatakamata za aina mbalimbali zinazofanyika sokoni hapo.
Hoja nyingine iliyoibuliwa ni Matamshi ya Waziri Mwigulu Nchemba kudharau wabunge wengine ambao ni wawakilishi wa wananchi, amekuwa na kauli chafu zinazokatisha tamaa wafanyabiashara, mfano ni ile ya kuwa yeye ni daktari wa uchumi, hawezi kubishana na waganga wa kienyeji.
Mfanyabiashara huyo amesema jeuri yote ya TRA inasababishwa na Waziri wa fedha ambae ni bosi wao mwenye jeuri, hashauriki, haambiliki. Wamewahi kuzungumza nae mara kadhaa lakini hajawahi kutekeleza hoja za mazungumzo hayo. Pia, mfanyabiashara huyo amesema Waziri Nchemba hafai kuwepo kwenye nafasi yake.
Waziri wa Biashara amelaumiwa pia kwa kutosimama na wafanyabiashara hasa kwa kauli yake ya Bungeni kuwa hakukuwa na mgomo Kariakoo. Wafanyabiashara hao wamesema kuwa haijawahi kutokea hata mara moja Waziri huyo akasimama na wafanyabiashara.
Urasimu mkubwa wa mizigo inayotoka Zanzibar umetajwa kuwepo tofauti na wafanyabiashara wanaotoa mizigo nchi zingine kama Dubai n.k. Pia, kumekuwepo na watu wengine wanaotoza kodi baada ya kutoa mzigo bandarini, watu hao wanapaswa kuwepo bandarini ili kurahisisha uliopaji wa kodi na kuokoa muda.
Mfanyabiashara mwingine amesema TRA wamepewa mamlaka ya kuomba rushwa kisheria, kwa kuwa wanalindwa na Sheria mbovu, wanataka rushwa kwa nguvu. "Rushwa ni mfumo, na sheria inawalinda. Wanatumia loophole ya elimu ndogo ya wafanyabiashara kudai rushwa....."
Mfanyabiashara wa vitenge (Mama Bonge) ametoa dukuduku lake la kudaiwa kodi zaidi ya bilioni 30, kisha baadae kutakiwa kulipia bilioni 10.3 ambazo hajalipa hadi leo.
Baada ya kushindwa kulipa alitakiwa kupelekwa mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi kisha kutakiwa walau moja ya tatu ya gharama zote (3.4 bilioni) wakati hajafanya kazi kwa zaidi ya miezi 8 na kontena zake 10 za vitenge zimekamatwa na TRA Ubungo.
===
UPDATE:
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Anazungumza
Amesema Serikali ya Samia Suluhu Hassan inayo dhamira ya dhati ya kuwasaidia wafanyabiashara wa Nchii kwa kuwasikiliza na kutatua matatizo yao.
Waziri Majaliwa amesema kikao hiki sio cha mwisho, bali vikao zaidi vitaendelea kufanyika ili kutatua kero na kuinua Sekta hii muhimu kwa uchumi wa Nchi.
Hoja zote zimechukuliwa na Serikali na zinaendelea kufanyiwa kazi kwa mfumo Shirikishi baina ya Serikali na wafanyabiashara wenyewe ikiwemo kuunda tume ya pamoja kati ya Serikali na wafanyabiashara. Timu hiyo itakuwa na watu 14, itapaswa kupitia na kuchukua yote yanayotekelezeka ili yafanyiwe kazi haraka, yanayohusu sheria yatapaswa kushughulikiwa bungeni haraka.
Amewataka Polisi kulinda usalama wa Raia na sio kujihusisha na kazi za TRA na task force hiyo imeondolewa.
Sanaaaa kuna kipindi mwaka jana nahisi alikamatwa na kupewa kesi ya kuhujumu uchumiAaaaah....Kumbe ndivyo Auntie?
Basi nikajua ndiyo huyo wa kwa Millard...
Halafu huyo wa Vitenge Kariakoo ni maarufu sana..
Hatoki mtu hapo ni kelele za chura watu wanabebanaMwigulu anajiona yeye ndie mwenye alimu pekee hapa Tanzania
Ndiyo Auntiee....Sanaaaa kuna kipindi mwaka jana nahisi alikamatwa na kupewa kesi ya kuhujumu uchumi
kwani hapa tunaongelea tatizo au tunaongelea way forward zitakazo tatua tatizo la waagizaji wa mizigo kwa less than container?Umeshaagiza mzigo kupitia mtu wa tatu ukafanya hiyo prorata?
Mkuu embu tuachane na hili hatutaelewana sababu unasema jambo ambalo ni nadharia maana moja ya tatizo la mfumo ambalo hata W/mkuu kalikubali leo ni hili.
Tukubali kutokukubaliana kuwa ukiwa na mzigo bila risiti wewe ni mhujumu uchumi kama unavyosema.
Sio ww uliyesema kuwa ukiwa na mzigo bila risiti ni mkwepa kodi? Kama ndiye na unajua kuwa inawezekana kuwa na mzigo bila risiti sababu ya mfumo basi hukupaswa kusema hivyo.kwani hapa tunaongelea tatizo au tunaongelea way forward zitakazo tatua tatizo la waagizaji wa mizigo kwa less than container?
Kwa hiyo mkeka utoke Leo LeoMama Samia akiendelea kuwakumbatia hawa wahuni Wawili, January Makamba na Mwigulu Nchemba faida yake ataiona 2025, sisi tunamuangalia tu.
Kwa mara ya kwanza leo ndo nimejuaMmoja kaomba namba ya waziri mkuu...
Unafanya kazi TRA.Muongeaji anasema au wakadange ?sasa hawa ndo waongeaji wao??
Ukiwa na pesa kichwa kinabalance mambo mjombaHapa TANZANIA nimeani wafanyabiashara ndo watu smart upstairs yaani Fred vunja Bei kaongea point mpaka nimeshangaa madini tupu.
Kwani Kenya hakuna viwanda?Hii nchi ya ajabu sana. Yaani Kenya soda bei rahisi kuliko Tanzania
TuacheMwigulu ni arrogant sana.Vile alianzisha betting company,alifuta kodi kwenye betting company. Mwigulu hafai kuwa waziri.
Usiku huuMama kama anataka kampeni zake ziwe smooth 2025 amtoe mwigulu na january