Nyagawakelvin
Member
- Apr 8, 2021
- 8
- 34
MFANYAKAZI ili Afukuzwe Kazi Kwa Sababu ya UTORO/KUTOKWEPO KAZINI, Inatakiwa Asiwepo Kazini Kwa Zaidi ya Siku Tano (5) za Kazi Bila Ruhusu au Sababu ya Msingi.
Inaletwa kwako na Nyagawa, J (Mwanasheria)
Wazee wa Mahakama ya Rufani Wamekubali Kupitia (Review) Upya Maamuzi Yao, Watoto wa Mjini Wanakwambia: Wazee Wamekubali Kuyarudia Matapishi Yao.
Iko Hivi, tarehe 25/9/2009 COSTANTINE Alifutwa Kazi na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Sababu ya Kutokwepo Kazini. Akafungua Kesi Kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Akashinda, CMA Iliamuru Arudishwe Kazini na Alipwe Mishahara Yote Ambayo Hakulipwa Tangu Kufutwa Kazi. Muhimbili Wakaenda Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Wakashindwa, Wakaenda Mahakama ya Rufani (Revision), Wakashinda Hiyo ilikuwa tarehe 29/01/2016, Mahakama ya Rufani Ilitengua Maamuzi ya Mahakama za Chini, ilisema Alifutwa Kazi Kihalali, Ilionekana HAKWEPO KAZINI KWA SIKU SABA (7).
Sasa CONSTANTINE Akawarudia Tena Wazee wa Mahakama ya Rufani ili Wayapitie (Review) Upya Maamuzi Yao, Imekuja Kuonekana Katika Zile Siku Saba (7) Ambazo ilionekana Hakwepo Kazini, Siku Zingine Zilikuwa Weekend na Sikukuu ya Idi, Hazikuwa Siku za Kazi, Kwahiyo Baada ya Kuziweka Pembeni Hizo Siku, Imegundulika HAKWEPO KAZINI KWA SIKU NNE (4) TU na Sio Siku Saba(7). Kanuni za Kazi Zinasema Ili Afutwe Kazi Inatakiwa Asiwepo Kazini Kwa Zaidi ya Siku Tano (5).
Hivyo tarehe 24/10/2022 Wazee Wameunga Mkono Maamuzi ya CMA na Mahakama Kuu, Alifutwa Kazi Kimakosa. Sasa Tupo 2022, Alifutwa Kazi 2009, Kwahiyo Atarudishwa Kazini na Kulipwa Mishara Yote Kuanzia 2009 Mpaka 2022!
Hii ni Moja ya Kesi Adimu Sana, Wazee wa Rufani Wanakubali Kureview Maamuzi Yao. Ikae Kabatini.