Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE

Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE

Naomba nitoe mfano kidogo tu ,nilikuwa na duka sikulipa kodi kwa miez sita baada ya mda wa mwanzo kifika ,nikawa na bajaji ikakamatwa nilipokwenda Sumatra walinitaka nifike tra kulipoa leseni .kuingiza tin yangu ilionekana na biashara nyingine ya duka nadaaiwa hivyo ilibd nilipie kodi ya duka na bajaj ndo niruhusiwe kuondoka nayo.

Kiufupi tin ni nzuri lakn wafanyakaz mjipange kulipa kodi kiufasaha kabsa kwa kila mnachofanya kuongeza kipato.pia biashara yako .na mda wa kufanya biashara bila kuzingatia mda wa serikal unaolipwa mshahara pia nao utafuatiliwa vizur

Nendeni kachukueni tin mtimize malenho ya serikal lakn mjue kuishi kiujanja ujanja na kukwepa kwedi itakuwa mwisho

Kwa pamoja tuijenge nchi

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Nimekuelewa japo sjaupenda huu mfumo

Maana mm n mswahili haswa.
 
Halafu ukija kuandaa hesabu zako za mwaka unafanyaje mkuu ili ubaki na faida kubwa??

Nikuibie siri ilivyokua inafanyika. Unalipa mishahara watumishi wako 50 tsh 300,000@ halafu kwenye mahesabu yako unaenda kuandaa kwa muhasibu/tax consultant unaandika umelipa watu 70 tsh 350,000@ kwa kuonesha labda daftari tu la mishahara na saini. Inapigwa hesabu mapato-matumizi(inflated) kinachobaki kinapigiwa hesabu Kofi

Sasa hivi itakua na TIN ya biashara na ya wafanyakazi 50 kwa mfano kilichoingia na kilichotoka tayari kinaonekana

Ila ofkoz njia nyingine za kukwepa zitapatikana tu(sitaziandika hapa) hahahaaa
Mimi nishazipata.
 
Ni kuboresha taarifa za walipa kodi tu. Nchi itakuwa kama islaer yaani ukiingiza namba ya nida papo hapo ikupe namba ya nssf/psssf na tin number.

Wahusika watajua kama upo kazini au ni mfanya biashara.
Na kama upo kazini basi taarifa za ukomo kazini ziwe zinawiana yaani ukisimamisha kodi ya PAYE na PSSSF/NSSF/ZSSF nazo zikome.

Na faida ya pili tutaokoa wafanyakazi hewa kwenye taasisi za watu binafsi kwani ma hr wanabandika majina tu huku wahusika hawapo na matajiri hawajui kama wanaibiwa.

Tutafika mahali ambapo taarifa za vizazi na vifo nao watakuwa wanahitaji namba ya NIDA yaani ukiweka namba tu itasema huyu ni marehemu.

Sio ni maandalizi ya tukinyimwa misaada wapi pa kuwabania
 
Huu utaratibu ulianza toka mwanzoni mwa mwaka huu nadhani kama sio February/March huko

Na kodi hapa inayotafutwa ni ya wale walioajiriwa sekta binafsi

Wafanyakazi was maduka,madereva,walinzi no

Yaani Yale maswala ya kulipana mshahara kwenye bahasha laki 2 na nusu halafu sie waajiri tunaingiza mshahara kwenye matumizi tunapigiwa hesabu ya kodi tunalipa ndio mwisho

Inatakiwa na mshahara wa muajiriwa ukatwe PAYE kama wanavyofanyiwa watumishi wa umma halafu Kofi ipelekwe TRA ikiainisha na TIN ya muajiriwa wako

Patamu sana hapa

Nchi zingine upo utaratibu huu au tumekopi rwanda
 
Aaah safi Sana jiwe kamatia hapo hapo anza na mapolisi na wafanyakazi wa tume waanze kusabmit TIN namba ukifika December awajatuma sisitisha mishahara Hadi walete TIN ndo fungua.
Mitano tena kwa jina la Yesu na Muhammad
 
Hilo tangazo limetolewa tokea mwezi wa 7, kwahiyo halijaanzia ulivyoona hiyo clip
Kuna taarifa inasambazwa kwa video clip na magazetini ikiwa imetolewa na TRA kuwataka waajiliwa wote kuwa na TIN. Ni taarifa ambayo naona kama inatokana na uongozi wa TRA wenye mapungufu ya hekima. Kwanza imeletwa ikiwa na kikomo (ultimatum) wakiamini wanayo nguvu hiyo ya kuwapa ultimatum waajiliwa wote. Pili imetolewa utadhani ni jambo la dharula. Tatu imetolewa kwa lugha ya hovyo, isiyo na uungwana pamoja na tishio la kuzuia mshahara wa mwajiliwa.

Naomba TRA wasijitwishe madaraka yasiyo yao. Mwajiliwa yeyote hajawahi kuwa na mkataba wa aina hiyo na TRA. Kama TRA wanaleta utaratibu mpya, wanatakiwa wawe waungwana (reasonable). Walete taarifa ya kiungwana na siyo kutishia wakati hakuna mwenye makosa. Labda wanaiga lugha za viongozi wanaomiliki vyombo vya dola. TRA hana nguvu ya aina hiyo na ni makosa kutishia watu wasio na mkataba wa aina hiyo.
ne
 
Kodi ambayo mfanyakazi analipa kama mfanyakazi, ni PAYE. Hii wala haina shida na haikwepeki. Serikali inaikata mapema kabisa.

Mimi nadhani wanataka kutrack mali za wafanyakazi . Kama mfanyakazi ana TIN ya gari alimiliki halafu akauza, mfano, itaonekana. Hasa kama aliuza bila TRA kujua, na kupata mgao wake.

Kwa vyovyote, ni ishara tosha kuwa honeymoon ya uchaguzi imekwisha sasa, ni muda wa kamatakamata. Tutaisoma Namba haswa.
Kuuza gari bila TRA kujua manake unayemuuzia habadili jina lako, na asipobadili manake TRA hawatojua kama uliuza hilo gari. Point yako kama haieleweki
 
YULE BWANA MKUBWA AMEPIGA MAHESABU YAKE NA KUONA HII NCHI NI TAJIRI 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom