Mfanyakazi TRA: Toka nianze kazi TRA miaka 8, haupo wakati ukusanyaji kodi ulikubalika kama wa Hayati Magufuli

Aliyemtaja Samia na mambo ya 2030 hapa nani?

Jikite kwenye mada acha kuhemka!
Kama SSH kafeli inaonyesha JPM hakuandaa mifumo mizuri ili hta akistaafu nchi isitetereke!! Kma kiongozi alifeli kwenye sustainability na succession management basi hakufaa kuwa Rais.

Hta mkimsifia JPM is better than SSH then what?? Yaani inatusaidiaje sasa? Kwamba tumtoe SSH alafu awekwe nani ndani ya CCM ambaye ni msafi?? Solution ni kuwatoa CCM hyo 2025 coz mmeishiwa ideas mnabaki kuishi kwenye kivuli cha JPM
 
Kwa mujibu wa yule jamaa sasa hivi maafisa wa TRA wanajipigia tu rushwa kwa sababu hata wakikomaa mdau anapiga simu juu na wao wanaishia kufokewa tu
Acha wale Bata maana rais alisema hawezi kukaa anafokea watu wazima.
Ngoja wamuonyeshe utu uzima wao.
 
CCM ipishe 2025 impishe nani sasa?Chadema,ambacho kimeshindwa japo kuhimili kinapotikiswa kwa mbinu za kuvurugwa?!

Kwa sasa hakipo chama mbadala kwa CCM nahofia utaendelea kusubiri sana!
 
Hayo matrl aliyokusanya alifanyia nini? Au ndiyo walikula yeye, Bashite, Sabaya na Polepole huku wakituringishia mav8?? Maana hii hapa chini ni aibu aliyoiacha ndani ya miaka 5 yake ya kukusanya mifweza.....

 
Kama SSH kafeli inaonyesha JPM hakuandaa mifumo mizuri ili hta akistaafu nchi isitetereke!! Kma kiongozi alifeli kwenye sustainability na succession management basi hakufaa kuwa Rais..
Kuna watu katika hii nchi ni wapumbavu na hawana akili.

Sijaona la maana lolote lililofanywa na JPM, na hata hao maraisi wengine.

Wamebadilisha kila aina ya raisi, lakini wapi ndio kwanza wanazodoana tu kila leo
 
CCM ipishe 2025 impishe nani sasa?Chadema,ambacho kimeshindwa japo kuhimili kinapotikiswa kwa mbinu za kuvurugwa?!

Kwa sasa hakipo chama mbadala kwa CCM nahofia utaendelea kusubiri sana!
Sasa kama CHADEMA sio mbadala si mchukue mwana CCM unayemuona ndio ana sifa za Urais aanzishe chama amuondoe SSH??

Maana naona malalamiko mengi ila mmekalia unafiki tu mpo CCM kulinda maslahi. Hta hao kina polepole na Bashiru si waanzishe chama wamuangushe SSH? au kinachowabakiza CCM ni kipi?

CHADEMA kimehimili imagine wizi wote ule kime consolidate kura zaidi ya million 2 majimboni for 3 consecutive elections hakuna mpinzani mwingine ameweza na kama hakikufa wakati wa JPM then hakitokufa milele

Ironically kuna mawaziri na manaibu wa waziri wametoka CHADEMA almost 10 najiuliza kma CHADEMA sio mbadala mbona mmeazima mawaziri kutoka kwao ilihali kuna wana CCM kama Nape mmewaacha?? Unachekesha sana
 
Sukama gang mmetumwa kwa wingi kumchafua SSH wewe ndio umefungua account juzi kuja kupost upumbavu
 
USINIKUMBUSHE.

Yaani umepeleta hesabu za 2015 kwa wakati, TRA umekaa nazo mpaka 2020 hujazigusa, 2020 anafanya examination unakuta kuna kodi ya m1 iliyotokana na makosa ya kibinadamu kukosea kutoa risiti bila kuleta taarifa, anachukua hiyo m1 anaipiga interest ya mwezi kwa miezi 60, anapiga na penalty, Halafu anafanya hivyo kwa hesabu za 2016,17,18, 19 na 20? Kisha anafungia account yenye fedha za wateja AISEEEEEEE.

AFISA UNAMUELEKEZA NILIKOSEA BADALA YA KUTOA M1 NIKATOA M10 ILA MAKOSA YALIFANYIKA NI KWELI HATUKUTOA TAARIFA KWA WAKATI PENGINE UNGEFANYA UKAGUZI WAKO NILIPOKULETEA HESABU MWAKA 2015 RISITI ILIYOKOSEWA INGEKUWEPO NA HATA ISINGEKUWEPO HIYO RIBA YA MIEZI 60 ISINGEKUWEPO KUWA NA UBINADAMU USIUE BIASHARA YANGU NAOMBA UNIFUNGULIE ACCOUNT NILIPE MISHAHARA NA NIMALIZIE KAZI ZA WATU.

LIMTU HALIKUELEWI NDO KWANZA LINAAGIZA VITUMBUA VYA CHAI😡😡😡 HALAFU LINATOA MAELEKEZO UPEWE CONTROL NAMBA UKALIPE KIASI NDO URUDI. HAPO LIMESHIKILIA ACCOUNT YAKO NA GARI LAKO LENYE MZIGO. UNACHUKUKUA MKOPO UNALIPA UNAACHIWA GARI LIKIWA BIDHAA ZIPO KWENYE HALI MBAYA UNAINGIA GHARAMA YA RIBA, AKAUNTI INAFUNGULIWA KWA POZI, IKIFUNGULIWA PESA YOTE INALIPA MKOPO NA RIBA, MISHAHARA UNADAIWA, PESA ZA WATEJA UNADAIWA, PRESHA.

HALAFU UNASEMA WATU WALIGOMBANIA KULIPA KODI??????? SERIOUS????????
 
Kama SSH kafeli inaonyesha JPM hakuandaa mifumo mizuri ili hta akistaafu nchi isitetereke!! Kma kiongozi alifeli kwenye sustainability na succession management basi hakufaa kuwa Rais...
Una hoja hasa kwenye suala la kuandaa mifumo mizuri lakini ni nani wakuaminiwa ku-push hiyo agenda maana hao tudhanio ndiwo ajabu kesho wake zao wakihongwa Ubunge wa viti maalum nao wanahamia huku kwetu na kuwa wapambe wetu kuzidi hata wapambe wenyeji!

Tambua,hata ndani ya CCM wapo watu wasiopendezeshwa na baadhi ya mambo hasa yahusuyo ufisadi, rushwa,upendeleo na mengine mengi kwayo.Lakini,watakimbilia wapi ilhali hata huko kuna watu wasio weza kusimamia imani zao!

Mfano,unauaminije upinzani wa mtu kama Zitto?
 
Walikuwa wanagombea kulipa kodi au walikuwa wanagombea kufunga biashara?
Lakufunga biashara ilikuwa ni biashara za wapiga dili! Nambie kampuni gani hata ya usafirishaji ilifunga biashara? Maana shop rite walifunga wakati wa kikwete!
 
Tambua,hata ndani ya CCM wapo watu wasiopendezeshwa na baadhi ya mambo hasa yahusuyo ufisadi, rushwa,upendeleo na mengine mengi kwayo.Lakini,watakimbilia wapi ilhali hata huko kuna watu wasio weza kusimamia imani zao!
Hamna kitu ka hiko mtu asiyependa rushwa CCM lazima ajiuzuru aanzishe chama sio anabaki ndani afu analalamika? Mfano Polepole alipokua msemaji mbona hakukamata hao anaowaita wahuni ila leo kaachia madaraka ndio analialia wahuni mara anatishia kuwataja n.k then utasema huyo mtu anachukia rushwa??

Ripoti ya makinikia kuna aliyekamatwa? Ripoti ya Tanzanite kuna mwana CCM kawekwa ndani? Vp kashfa ya Passport na NIDA kuna wana CCM waliokula hela wamefungwa?? Sijaona hta kamati ya maadili CCM ikiwaita hao mafisadi tajwa kwenye ripoti then unasema eti kuan watu wanaochukia rushwa ndani ya CCM?

Acheni unafiki kma hamtaki SSH anzisheni chama chenu mumtoe sio mnalialia baada ya kunyang'anywa ulaji na timu mpya.
 
Lakufunga biashara ilikuwa ni biashara za wapiga dili! Nambie kampuni gani hata ya usafirishaji ilifunga biashara? Maana shop rite walifunga wakati wa kikwete!
Download NBS report za kuanzia 2019 to 2017 utaona biashara zilizofungwa na kufunguliwa then rudi hpa uandike hiki ulichoandika.
 
Sasa kama CHADEMA sio mbadala si mchukue mwana CCM unayemuona ndio ana sifa za Urais aanzishe chama amuondoe SSH?...
Chadema iwekeze kwenye Itikadi ili hata inapotikiswa kwa mbinu za kishamba km kuhongwa Viongozi wake wasikubali kukimbia chama.

Ile hali ya wanaoonekana vinara kwenye chama na wanapotikiswa kwa mbinu za kishamba za kijasusi na mwisho wa siku wanahamia huku hiyo ni sababu tosha ya kuwaonyesha hamjawekeza kwenye eneo la ujasusi wa kiitikadi.
 
Bado nasema una hoja.Lakini...

...kwanini chama kingine kipya na isiwe CHADEMA na vingine vilivyopo?

....kwa vinara wa kupambania mabadiriko wanakimbia risasi na kwenda kuishi ughaibuni ambapo mabadiriko hayapaswi kufanyikia huko?
 
Chadema iwekeze kwenye Itikadi ili hata inapotikiswa kwa mbinu za kishamba km kuhongwa Viongozi wake wasikubali kukimbia chama.
Tatizo unaangalia CHADEMA kwa wabunge na viongozi sio ile core ya chama nchi nzima. Hvi kuna mwenyekiti wa kanda au katibu wa kanda aliyehamia CCM hii miaka mitano bar Mathew suleiman? Walioahama ni hawa wa siasa za majimboni ila zile post za kichama tu bila interest za chaguzi za majimboni hakuna aliyehama CHADEMA na hiyo inaonyesha ukomavu wa chama kulinda core ya chama.

Strategy ya chama ilikua devolution so CHADEMA ni level ya kanda ndio operation zote zinafanyika no wonder viongozi wa kitaifa au mbunge akihama chama bado kina wafuasi hardcore eneo lile sababu coordination zote zinaanzia ofisi ya Kanda.

Ssa ijudge CHADEMA kwa mafanikio hayo Sio wanasiasa wa majimboni wanapohama eti ndio CHADEMA imekufa its funny. Chama kinakufa kma viongozi wa misingi, kanda na wilayani watahama maana hao ndio wanaamua hadi nani agombee na chama kijitanue vp n.k otherwise you r too bleek kuishauri CHADEMA maana hujui hta strategy zinazoendelea kma Chadema digital, Sera mbadala, chadema ni msingi, Bavicha queens n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…