Mfanyakazi wa TRA akutwa amehifadhi pesa taslimu Tsh. Bilioni 7 nyumbani

Chura kiziwi alishasemaga kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake....Ila TRA siku nikiingia huko Aloo aloo lazima nimuhamishe mtu pale Masaki.
 
Na hawa watu ni kama Raisi anawaogopa sana.
Ni lazima awaogope, kwani wao ndio maboss wake, raia wengine ni mateka wao, ambao rais huyo huyo anawadharau na kuwapuuza hadi kuwaambia hadharani ameamua kuwa 'Chura Kiziwi' ili asisikie kelele toka kwao. Rais anafanya hivyo akijuwa hawa raia hawawezi kumfanya chochote; kwa sababu ngao yake ni hao wenye kamba ndefu.

Lakini nirudi nyuma kidogo. Habari za namna hii kwenye kipeperushi kama hicho mara nyingi kazi yake ni kama kutafuta kuumiza akili za wananchi tu. Hata kutaja tu, hao watu ni akina nani gazeti linashindwa?

Hii ni biashara mbovu sana.
 
Yaani mimi mtoto wangu ashindie mlenda huku analipa kodi haya majangili yanazipiga? sifanyi huo upumbavu nikipata chance nitaiba haswa, n ujinga mimi
Ni upambavu wa hali ya Juu sana, Mimi ninaviji biashara zangu kama nne, sijawahi kulipa Kodi, siwezi kuwalipia kodi watu wahuni. Hii Nchi ya Ajabu sana.
 
 
Mpaka siku tutakapokuwa na uwezo wa kubadilisha vyama katika uongozi wa nchi tusitegemee mwanasiasa yeyote wa chama tawala kuheshimu wananchi. Never.
 
Halafu wanamdanganya Raisi naye anadanganyika kwamba wafanyabiashara wanakwepa kodi, sasa huyo ni mmoja tu B7, ke hao wengine? Mungu yupo iko siku haya yatakwisha....
 
Kwa Sasa nchi imeoza kabisa.wafanya kazi wa Tra wengi wao ni Wala rushwa sana na wahujumu wa biashara za watu.mfano wao kuagiza bidhaa nje Huwa hawajikati Kodi.mtu anaka diploma tu uchwara ka Kodi kasomea hapo mikocheni akiajiriwa Tra mwaka mmoja tu bilionea.
 
ccm na viongozi wake ni vipofu na janga la taifa
 
TAKUKURU imejaaa wahuni ile, yaani wale mpaka uwaambie sasa kamata huyu, ogopa taasisi unaongozwa na askari Police
ogopa ni hatari kuna hawa askari wa fire kufuatilia fire-extinquishers maeneo ya biashara kazi kuwakamua watu elf20-50 kulingana na biashara yako kama hauna mtungi wa fire na wenyewe wanajipangia kila mwaka lazma wapite kila mlango kusanya hizo hela na kuzitia kwenye mifuko yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…