KERO Mfumo wa kulipia maji Iringa uwe automatic Mtu ukilipa tu maji yaanze kutoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
289
Reaction score
415
Mimi ni Mwananchi kutoka Iringa, kero yangu kubwa ni kwa IRUWA (Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Iringa (IRUWASA) kuna wakati tunanunua maji token hazirudi siku moja mpaka mbili.

Hii ni kero kubwa sana kwangu na kwa wengine, nashauri mfumo wa kulipia maji uwe automatic mtu ukilipa tu maji yaanze kutoka.

Kuhusu hilo pia kusubiri tokeni ni kero sana.

Pia, ununuaji wa maji saizi bila kuwa na Shilingi 3,000 inagoma tunaomba warudishe mfumo wa kununua maji kuanzia Shilingi 500 kwa kuwa kuna muda mtu unaweza kuwa hauna fedha na unahitaji maji kidogo tu lakini kwa kiwango hicho unalazimishwa kununua maji mengi.
 
Hivi huko mnatumia mita unalipia kadri unavyotumia sio kusoma bill kama za kwetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…