Mfumo wa LATRA haufanyi kazi, wasafirishaji washindwa kupata huduma kwa siku kadhaa

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,901
Mfumo wa Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini (The Land Transport Regulatory Authority- LATRA). Huafanyi kazi sasa kwa takribani wiki nzima.

Watoa huduma za usafiri wa Ardhini ambao wanapaswa kupata leseni toka mamlaka hiyo kupitia mfumo wao wa njia ya mtandao (Online Application) wamekwama.

Kila wakipiga simu wanaambiwa mfumo utatengamaa ndani ya saa moja lakini hadi sasa huduma hakuna.

Ni ajabu sana mamlaka hii inayokusanya mamilioni ya shilingi kila siku inashindwa kusimamia njia waliyojiwekea huku wateja wakienda ofisini kupata huduma wanaambiwa hawana namna ya kuwasaidia hadi mfumo utengamae.

Na shida ni kwamba ukifanya huduma za usafirishaji bila leseni yao unapigwa fine ya 250,000.

Mifumo hii ilitengenezwa kudhibiti mapato ya serikali kupitia Control number. Lakini kwa siku za hivi karibuni mifumo mingi imekuwa ikisumbua. Je watendaji wa mifumo hii wanataka turudi katika mifumo ya zamani ili waweze kuhujumu mapato ya serikali?

Tunaomba Wizara ya Uchukuzi na Fedha iliangalie hili kwa kina.
 
Mifumo mingi ilitengenezwa haraka haraka bila kufuata misingi ya usanifu wa mifumo ya Software.

Pia mifumo mingi imetengenezwa na vijana walio toka vyuoni ambao walikuwa hawana uzoefu, wa kutengeneza mifumo mikubwa.

Mingi ya mifumo hii inahitaji kufanyiwa usanifu upya na kutengenezwa, upya ili kuendana na growth ya data na users.
 
Sio kweli. Mifumo mingi imenunuliwa nje na kuwa customized. Hii failure sio ya bahati mbaya kuna mkakati ili watu warudi Analogy.
 
E0NhMwdXIAAW0HL.jpeg
 
Pia mfumo wa TASAC haufanyi kazi wiki ya Pili Sasa.
 
Mifumo mingi ilitengenezwa haraka haraka bila kufuata misingi ya usanifu wa mifumo ya Software.

Pia mifumo mingi imetengenezwa na vijana walio toka vyuoni ambao walikuwa hawana uzoefu, wa kutengeneza mifumo mikubwa.

Mingi ya mifumo hii inahitaji kufanyiwa usanifu upya na kutengenezwa, upya ili kuendana na growth ya data na users.
pointless!
 
Kodi nyingi sana zinapotea, mifumo mingi sana yakifedha nwadays Aisha haifanyi kazi au ipo down.
 
Mifumo mingi ilitengenezwa haraka haraka bila kufuata misingi ya usanifu wa mifumo ya Software.

Pia mifumo mingi imetengenezwa na vijana walio toka vyuoni ambao walikuwa hawana uzoefu, wa kutengeneza mifumo mikubwa.

Mingi ya mifumo hii inahitaji kufanyiwa usanifu upya na kutengenezwa, upya ili kuendana na growth ya data na users.
Kwahiyo hio mifumo ilipewa muda baada ya 26/03/2021 ianze kusumbua?
 
Haya madudu ndiyo yanayowafanya waandike kwamba sasa hivi wana furaha zamani hawakuwa na furaha.

Lakini sauti ya Majaliwa ina mamlaka ndani yake ndiyo maana wako bize kumfundisha rais Samia kuwa amtoe kwenye uwaziri mkuu kwa sababu eti ni masalia ya JPM!

Kwani SAMIA ni masalia ya nani?
 
Mifumo mingi ilitengenezwa haraka haraka bila kufuata misingi ya usanifu wa mifumo ya Software.

Pia mifumo mingi imetengenezwa na vijana walio toka vyuoni ambao walikuwa hawana uzoefu, wa kutengeneza mifumo mikubwa.

Mingi ya mifumo hii inahitaji kufanyiwa usanifu upya na kutengenezwa, upya ili kuendana na growth ya data na users.
Kwanini ilikuwa haifeli hapo mwanzo??
 
Acha kudanganyaa. Mifumo mingi haikuwa wazi. Aliijua mtu mmoja tuu na wasaidizi wake ambao wengi walikuwa ndugu zake.
Acha uongo wewe kama hujui kitu nyamaza siyo kila mada uchangie waache wanaojua mada husika wachangie wewe baki kujifunza.
 
Nachangia pale ninapo kuwa na uelewa wa jambo husika. Nachosema ni hivi' hakuna mfumo unaosumbua pale TASAC. Nimeuliza ni mfumo gani unasumbua ili usaidiwe?. Otherwise utakuwa basi unadanganya umma kupitia JF.

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
magufuli alikuwa dikteta kama madikteta Wengine, alikuwa na roho mbayaa na ya chuki,

Mungu siku zote hamuinui mtu kibri, na watu vibri siku zote mwisho wao huwa mbaya,
Mwisho mbaya wa Magufuli ni upi ?

Kama kama kufa kila mtu atakufa
 
Back
Top Bottom