Uchaguzi 2020 Mfumo wa Majimbo wa Lissu na CHADEMA unatumika katika Mataifa na Taasisi kubwa duniani kuleta ufanisi wa kimaendeleo

Uchaguzi 2020 Mfumo wa Majimbo wa Lissu na CHADEMA unatumika katika Mataifa na Taasisi kubwa duniani kuleta ufanisi wa kimaendeleo

FAIDA YA SERIKALI ZA MAJIMBO NI IPI?

Hivi unajua kuwa Serikali ya majimbo huwa na Serikali inayojitegemea kwa kila Jimbo? Inakuwa na Waziri mkuu na mawaziri wengine wote.

Hebu tuambieni faida za Serikali ya majimbo Ni zipi? Hivi Mkoa Kama wa Arusha, Kilimanjaro, na Manyara mapato yake kulingana na Rasilimali zinaweza kuwa sawa na Mkoa wa singida, Dodoma na Kigoma?

Hebu tujadili kisomi faida za Serikali ya majimbo ni zipi kiuchumi, na Kisiasa. Au tumeamua tu kuiga? Je hatuwezi kuboresha zaidi muundo wetu wa Serikali za mitaa ambazo zinabeba lengo Hilo Hilo zikawa Bora zaidi?
Hatujalenga hizi semi autonomous states. Kimsingi tumelenga kufanya devolution ya kawaida bila kuathiri geographical demarcation iliyopo.

Hautathiri mfumo wa mahakama uliopo na hautathiri mfumo wa bunge uliopo isipokuwa utaarhiri mfumo wa uendeshaji serikali.

Kikubwa kitakachofanyika ni kufanya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuwa watu wa kuchaguliwa na wananchi huko mikoani ili wawajibike moja kwa moja kwa wananchi.

Hatulengi kutengeneza semi autonomous states zenye mahakama zinazojitegemea, bunge linalojitegemea na serikali yanayojitegemea hapana.

Tunachotaka ni kufanya ugatuzi tu ili serikali za mikoa na serikali za mitaa wawajibike moja kwa moja kwa wananchi.
 
Kwahiyo kuna Mkoa wa Mbulu, Same, Meru, Arusha kati na mashariki? shame on you
Wewe utaamua hivyo "shame on you" lakini ukweli wa mambo utabaki hivyo hivyo utatengeneza ma king pin kwa kila sehemu na division within people even of the same sect.
E.g. Hanang Nagu awe CCM na kundi lake, then Sumaye awe Chama Kingine na watu wake, si watapigana wenyewe kwa wenyewe kwa kundi moja kuwaona wengine no betrayers etc.
Lakini ukiwa ni hamnazo hutaona the big picture
 
Chukueni mtazamo mpana zaidi wa suala la ulinzi na usalama kwa taifa. Tusijilinganishe na Kenya ambayo bajeti yao uchumi wake pia hauwezi kuulinganisha na wakwetu. Mentality ya watz na uvivu na wizi je vitaondoka kwa kuweka majimbo?

Mkuu - wasikudanganye hao wanaopigia debe majimbo na kuitumia Kenya kama reference. Lissu anasema Majimbo yatakusanya pesa yake na kufanya maendeleo kutokana na pesa za Majimbo. Kenya haifanyi hivyo - utaratibu wa Kenya ni kama wetu tu hapo TZ - wao wanaita tu County - lakini ndio kama mikoa. County inapokea pesa kutoka serikali kuu - na ndio maana kuna Kenya Revenue Authority (KRA); ambayo inakusanya kodi kama tu TRA inavyofanya, na kuikabidhi tu kwa serikali ya Kenya. Hivyo hizo "porojo" zinazopigwa na hawa "Ma-Great Thinker Poyoyo" wasiofanya utafiti wa kweli usisikilize. Wengi wao hawajui wanaloliongea. Maana hata hajiulizi - kuna Majimbo ambayo resource kubwa zao zitakuwa ni kulima Mihogo tu - sasa hao watapata vipi pesa za kuongoza jimbo? Kwa kulima Mihogo utaweka lami ambayo gharama yake ni Tshs 1.2 bilioni kwa kilomita?
 
Hiki ndicho Lissu cha ChademaDM wanamaanisha, na tangu jana nimekuwa muumini mkubwa wa Serikali ya majimbo.
Jana nimemsikia mgombea uraisi wa UMD (The Union for Multiparty Democracy) nae bila kumung'unya maneno akisema sera ya majimbo nao wakipata ridhaa wataitekeleza. Mimi si mchadema lakini sera hii nimekua niki iunga mkono kwa muda mrefu. Haiwezi tukatetegemea Dar na sasa Dodoma kutuamulia kila kitu.
 
Bibi yangu wa kule kijiji cha epanko- wilaya ya ulanga ,sijui ataelewa kweli haya mambo ya majimbo wakati toka azaliwe hajawahi kutoka nje ya kile kijiji ,mmmh sijui ila ngoja tuone itaishia wapi
 
Chukueni mtazamo mpana zaidi wa suala la ulinzi na usalama kwa taifa. Tusijilinganishe na Kenya ambayo bajeti yao uchumi wake pia hauwezi kuulinganisha na wakwetu. Mentality ya watz na uvivu na wizi je vitaondoka kwa kuweka majimbo?
Kenya,Marekani,Nigeria,Uingereza hawana majeshi? hawana maamiri jeshi wakuu wanao. serikali kuu itakuwepo kama kawaida ila ikiwa na wizara chache sana Ulinza,Mambo ya ndani kwa baadhi ya maeneo,fedha,nchi za nje.

majimbo yatakuwa yanapeleka serikari kuu sehemu ya mapato yao serikali kuu kwa ajili ya kuwezesha uendeshaji wa serikari kuu na kwa nchi za aina hii unakuta viongozi wanawatii wapiga kura sio viongozi wanawatisha wapiga kura, muhumu ni kuwa viongozi wa kuteuliwa huwa ni watendaji wa serikali na hawana madaraka ya moja kwa moja kwa wananchi kama wakuu wa mikoa,wilaya nk.
 
Tungeangazia NCHI ZA KIAFRIKA zinazotumia mfumo huu,tuone ufanisi wake badala ya kuangazia vitaasis tu.

KKKT yenyewe unayoipigia chepuo ina migogoro kibao isiyoisha juu ya matumizi mabaya ya fedha.
Kesi ya Munga imeishia wapi?

Na sidhani kama CDM yenyewe (wapiga filimbi ya majimbo) kama wanatumia mfumo huo kugawa ruzuku ili kila kanda/jimbo lijisimamie lenyewe!
Niambie mgogoro uliopo wa Kkkt unaohusu labda mapato
 
Tusijilinganishe na uingereza au marekani. Chukulia kenya na nigeria na angalia historia yao. Je rushwa na wizi vimekomeshwa? Umasikini umekomeshwa? SGR ya kenya mbona bomu na wananchi inawauma kabisa hata ukizungumza nao unaona kabisa walivyo na uchungu kuwa "wameliwa" pale. Tuache ulimbukeni na kukosa shukrani. Majuto ni mjukuu na maji yakimwagika hayazoleki.Waulize walibya.
 
Mfumo wao wa viongozi wa kanda umeleta tija yoyote kwenye performance ya chama?
Ndio maana cama kimebaki imara hata baada ya kufungiwa miaka mitano kisifanye siasa,na ndio maana mnateseka sana sasa hivi majukwaani baada ya kutangaziwa kuwa kimekufa na sasa ki hai na kinanguvu mara dufu.
 
Tusijilinganishe na uingereza au marekani. Chukulia kenya na nigeria na angalia historia yao. Je rushwa na wizi vimekomeshwa? Umasikini umekomeshwa? SGR ya kenya mbona bomu na wananchi inawauma kabisa hata ukizungumza nao unaona kabisa walivyo na uchungu kuwa "wameliwa" pale. Tuache ulimbukeni na kukosa shukrani. Majuto ni mjukuu na maji yakimwagika hayazoleki.Waulize walibya.
Waribya walikuwa na sera ya majimbo ndio iliwaletea hayo yote?
 
Tungeangazia NCHI ZA KIAFRIKA zinazotumia mfumo huu,tuone ufanisi wake badala ya kuangazia vitaasis tu.

KKKT yenyewe unayoipigia chepuo ina migogoro kibao isiyoisha juu ya matumizi mabaya ya fedha.
Kesi ya Munga imeishia wapi?

Na sidhani kama CDM yenyewe (wapiga filimbi ya majimbo) kama wanatumia mfumo huo kugawa ruzuku ili kila kanda/jimbo lijisimamie lenyewe!
Hesabu ya matumizi ya ruzuku kwa chadema ni SIRI eti
 
Kenya ufisadi, rushwa, ukabila, na uhalifu uko kila mahali. Nigeria rushwa, wizi, uhalifu,ukanda, udini na ugaidi vipo sana. Sioni kama majimbo yao yanasaidia vipi kuondoa kasoro hizi zote.
 
Kenya,Marekani,Nigeria,Uingereza hawana majeshi? hawana maamiri jeshi wakuu wanao. serikali kuu itakuwepo kama kawaida ila ikiwa na wizara chache sana Ulinza,Mambo ya ndani kwa baadhi ya maeneo,fedha,nchi za nje.

majimbo yatakuwa yanapeleka serikari kuu sehemu ya mapato yao serikali kuu kwa ajili ya kuwezesha uendeshaji wa serikari kuu na kwa nchi za aina hii unakuta viongozi wanawatii wapiga kura sio viongozi wanawatisha wapiga kura, muhumu ni kuwa viongozi wa kuteuliwa huwa ni watendaji wa serikali na hawana madaraka ya moja kwa moja kwa wananchi kama wakuu wa mikoa,wilaya nk.
Hakuna kitu kama hicho tena utakuta wana matatizo makubwa tu , angalia Nigeria, Kenya , USA ya Trump n.k
 
Jana nimemsikia mgombea uraisi wa UMD (The Union for Multiparty Democracy) nae bila kumung'unya maneno akisema sera ya majimbo nao wakipata ridhaa wataitekeleza. Mimi si mchadema lakini sera hii nimekua niki iunga mkono kwa muda mrefu. Haiwezi tukatetegemea Dar na sasa Dodoma kutuamulia kila kitu.
Ila unaelewa kuwa Dar ndio kunatoa kodi kubwa kwa serikali - si ndio? Maana Viwanda vikubwa viko Dar (Pwani itafuatia soon), Bandari kubwa iko Dar, Airport kubwa iko Dar, na watu wengi kutoka mikoa mingine mingi wanaishi Dar. Hivyo sera za Majimbo zikianza; pesa zilizokuwa zikipatikana Dar na kugawawiwa ili kuleta maendeleo ya kile kijiji chako cha Lumonge; hazitopatikana tena. Dar itaneemeka zaidi; maana mapato yote yatabaki hapo. Itabidi jimbo lako liangalie jinsi ya kupata pesa za maendeleo kivyakevyake. Labda kama jimbo lako litakuwa maeneo yenye dhahabu (hapo mtaula); utalii (mtaula pia) ikiwa jimbo lako litakuwa kwenye kilimo (haswa Mihogo; Ufuta; Mbogamboga siju) - mtaisoma namba. Labda kama mtauza hayo mazao mara 300% ya bei ya sasa.
 
Back
Top Bottom