Uchaguzi 2020 Mfumo wa Majimbo wa Lissu na CHADEMA unatumika katika Mataifa na Taasisi kubwa duniani kuleta ufanisi wa kimaendeleo

Uchaguzi 2020 Mfumo wa Majimbo wa Lissu na CHADEMA unatumika katika Mataifa na Taasisi kubwa duniani kuleta ufanisi wa kimaendeleo

Tungeangazia NCHI ZA KIAFRIKA zinazotumia mfumo huu,tuone ufanisi wake badala ya kuangazia vitaasis tu.

KKKT yenyewe unayoipigia chepuo ina migogoro kibao isiyoisha juu ya matumizi mabaya ya fedha.
Kesi ya Munga imeishia wapi?

Na sidhani kama CDM yenyewe (wapiga filimbi ya majimbo) kama wanatumia mfumo huo kugawa ruzuku ili kila kanda/jimbo lijisimamie lenyewe!
Ili mtu apewe uongozi lazima kuwepo reference. Chadema ni taasisi kama wao wanavyodai. Hela yote inaishia makao makuu.

Wajaribu kwanza ndani ya Chama chao tuuone huo ufanisi wake kabla hatujawapa jukumu kubwa la nchi.
 
Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!
Very true. Bila kujipendekeza kwa mkuu mkoa wako utabaki nyuma. We must get rid of this shit
 
Wakati mbeba maono ya umoja wa kitaifa na maendeleo Rais John Magufuli akisema kuwa siasa za majimbo zitaleta mgawanyiko na mkanganyiko pro lisu walishupaza shingo na kumkumbatia lisu aliyetumwa na mabeberu kuvuruga umoja wa kitaifa kwa kuja na hoja ya siasa za majimbo .

Leo maelfu ya waethiopia wanakimbia nchi yao kisa jimbo moja tu la tu Tigray kuamua kukabilia na serkali ya kitaifa na mpaka sasa watu wengi wamesha uwawa ni sawa na kusema kuwa kama sera ya chadema ya majimbo ikitekelezwa hapa Tanzania yawezekana kuzuka mkoa mmoja kusema hautambui serkali ya shirikisho na kuligawa taiafa maana hakuna atakaye kubali kugawana nchi.

Sera mbovu kama hizi watanzania tuko macho kuzikataa tena kwa nguvu zote bila kujali itikadi na hapa tunawapa onyo chadema wasije kutamka tena eti zera ya majimbo hapa Tanzania

Ethiopia inawaka moto na waziri mkuu ameshasema hawataiacha Tigray ijitenge au ikaidi amri ya serkali kuu

Hapa Tanzania sera hii haitakuja kuwekwa kwa maslahi mapana ya utaifa na umoja ambayo ndio tunu za taifa hili , tumkemee lisu na sera yake tuangalia mfano Ethiopia ambayo wamama na watoto ndio wanakufa

USSR
 
Back
Top Bottom