Uchaguzi 2020 Mfumo wa Majimbo wa Lissu na CHADEMA unatumika katika Mataifa na Taasisi kubwa duniani kuleta ufanisi wa kimaendeleo

Uchaguzi 2020 Mfumo wa Majimbo wa Lissu na CHADEMA unatumika katika Mataifa na Taasisi kubwa duniani kuleta ufanisi wa kimaendeleo

Hakuna kitu kama hicho tena utakuta wana matatizo makubwa tu , angalia Nigeria, Kenya , USA ya Trump n.k
USA ni matatizo ya Trump mwenyewe sio majimbo UBAGUZI,Nigeria udini/kabila Kenya sio majimbo kimsingi ila tunafanana nao ila wao huwachagua wakuu wa mikoa husika lakini mapato yako centralised KRA, kila nchi ina matatizo yake isipokuwa uoga wa CCM sio majimbo bali wanamhitaji sana Rais mfalme ili ailinde CCM isife, iko wazi kuwa ili CCM iishi ni lazima ikae kwenye koti la serikali.
 
Ila unaelewa kuwa Dar ndio kunatoa kodi kubwa kwa serikali - si ndio? Maana Viwanda vikubwa viko Dar (Pwani itafuatia soon), Bandari kubwa iko Dar, Airport kubwa iko Dar, na watu wengi kutoka mikoa mingine mingi wanaishi Dar. Hivyo sera za Majimbo zikianza; pesa zilizokuwa zikipatikana Dar na kugawawiwa ili kuleta maendeleo ya kile kijiji chako cha Lumonge; hazitopatikana tena. Dar itaneemeka zaidi; maana mapato yote yatabaki hapo. Itabidi jimbo lako liangalie jinsi ya kupata pesa za maendeleo kivyakevyake. Labda kama jimbo lako litakuwa maeneo yenye dhahabu (hapo mtaula); utalii (mtaula pia) ikiwa jimbo lako litakuwa kwenye kilimo (haswa Mihogo; Ufuta; Mbogamboga siju) - mtaisoma namba. Labda kama mtauza hayo mazao mara 300% ya bei ya sasa.
Hapo penye rangi si sawa. Siyo mapato yote yatakayobaki Dar. Serikali kuu itakuwa pia inakusanya kiasi fulani cha pesa kutoka majimboni na hizi fedha zitaendesha serikali kuu na pia kupelekwa kule ambapo kipato cha serikali ni kidogo. Kumbuka pia Japan hawana rasilimali za kuzungumzia lakini wanavuna akili zao. Ushindani kati ya jimbo na jimbo utakuwepo na upuuzi wa kusema hamkunipigia kura hivyo hamtapata maendeleo utakufa.
 
Huu mfumo, in practice ndio anaoutumia magufuli. Pale anaposema msipochagua upinzani, sileti maenddleo. Kuna kanda/majimbo yana upinzani mkubwa na yameshatengwa
 
Hapo penye rangi si sawa. Siyo mapato yote yatakayobaki Dar. Serikali kuu itakuwa pia inakusanya kiasi fulani cha pesa kutoka majimboni na hizi fedha zitaendesha serikali kuu na pia kupelekwa kule ambapo kipato cha serikali ni kidogo. Kumbuka pia Japan hawana rasilimali za kuzungumzia lakini wanavuna akili zao. Ushindani kati ya jimbo na jimbo utakuwepo na upuuzi wa kusema hamkunipigia kura hivyo hamtapata maendeleo utakufa.
Hiyo ni kitu chako tofauti - sio kitu ambacho ana-advocate mmoja wa Wagombea. Mgombea yuko very clear - kila jimbo litakusanya mapato yake - na kuamua nini cha kufanya. Na kila jimbo wanachozalisha; watamua wao wakauze wapi. Sasa kama pesa zitapelekwa wenye majimbo mengine - kuna tofauti gani na mfumo wa sasa?
 
Ukifika maeneo inakotoka dhahabu ya nchi hii ndipo utakubaliana na sera hii ya majimbo. Barabara na mashimo na vumbi la kutisha lakini maeneo yasiyo na kitu mfano TACHO ni lami na uwanja wa nanihii
 
Majimbo ni sawa kama mikoa hii hii itageuka majimbo. Sio kufanya majimbo Tisa kama ya ukoloni..
Mikoa ipo ila haina nguvu kama majimbo.

Hata viongozi wa majimbo watapigiwa kura na wananchi sio sawa na wakuu wa mikoa, wakurugenzi, DAS, RAS wanaoteuliwa na rais.
 
Mikoa ipo ila haina nguvu kama majimbo.

Hata viongozi wa majimbo watapigiwa kura na wananchi sio sawa na wakuu wa mikoa, wakurugenzi, DAS, RAS wanaoteuliwa na rais.

Point yangu tusirudishe majimbo tisa
Kama majimbo hii hii mikoa iwe majimbo
 
Hiyo ni kitu chako tofauti - sio kitu ambacho ana-advocate mmoja wa Wagombea. Mgombea yuko very clear - kila jimbo litakusanya mapato yake - na kuamua nini cha kufanya. Na kila jimbo wanachozalisha; watamua wao wakauze wapi. Sasa kama pesa zitapelekwa wenye majimbo mengine - kuna tofauti gani na mfumo wa sasa?
Issue ni kiasi gani kinapelekwa wapi na maamuzi ya kutumia yanahusu nini. Pia accountability chini ya majimbo ni kwa wapiga kura na sio kwa raisi. Msikilize Lissu kwa umakini utaelewa anasema nini.
 
Nimekuwa nakufatilia namna unavowakilisha Sera zako kwa ufasaha kwamba kama ukifanikiwa kuwa rais utaifanyia mini Tanzania.
Kiukweli kuna mengi nakubaliana nayo ili hili LA kuigeuza nchi yetu kuwa katika mfumo wa serikali za majimbo sikubaliani nalo hata kidogo.

Nina sababu chache kama ifuatavyo:
1.Mfumo juu unaweza kuwa chanzo cha kuondoa umoja wa kitaifa tulionao

2.:Unaweza kuleta ukabila na hata udini

3. Utaondoa kabisa rationale katika rasilimali za nchi ambazo ni kwa faida ya watanzania wote

4. Kunaweza tokea hatari kwa baadhi ya majimbo huko baadae kutaka kujitoa na kujitangazia Uhuru/utaifa wao

Conclusion.
Kama kweli ikatokea miujuza umekuwa rais hii Sera si ya kushikamana nayo.
Mfumo wa sasa wa serikali za mitaa bado unafaa sana ila unahitaji maboresho makubwa ili use more responsive
 
Majimbo kujitoa ondoa shaka, ni uhaini. Nyerere aliunga mkono Biafra kujitoa Nigeria lakini ilishindikana, Gowon aliwatuiza. Majimbo saba ya marekani kusini yalijaribu kujitoa USA ilishindikana, Lincoln aliwatuliza.

Leo hii tizama Nigeria inaongoza kwa uchumi Africa, Marekani inaongoza kwa uchumi duniani. Sisi miaka 55 ya mikoa maadui bado ni walewale watatu.
 
Majimbo kujitoa ondoa shaka, ni uhaini. Nyerere aliunga mkono Biafra kujitoa Nigeria lakini ilishindikana, Gowon aliwatuiza.
Majimbo saba ya marekani kusini yalijaribu kujitoa USA ilishindikana, Lincoln aliwatuliza.
Leo hii tizama Nigeria inaongoza kwa uchumi Africa, Marekani inaongoza kwa uchumi duniani.
Sisi miaka 55 ya mikoa maadui bado ni walewale watatu.
Nigeria is one of rich and developed country because of oil , iliyo wawezesha kuwa na vyuo vingi na kuwaelimisha watu was, na waliokwenda nje waka more exposed etc na sio suala majimbo
 
Ile siku inatangazwa kuwa Tanzania tutakuwa na majimbo ndio tuhesabu kupoteza jina Tanzania katika orodha ya nchi Duniani.

Hii sera haitufai.
 
Kama ungekuwa niLutelo wa Kweli ama Roman Catholic tuna mfumo unaofanana na majimbo tukiziita Dayosisi.
Mfano. Dayosisis ya mashariki na pwani.
Dayosisi ya kusini magharibi.
Dayosisi ya konde.
Dayosisi ya kasikazini kati nk nk.

Huu ni mfumo ulioanzishwa na wazungu hata selikalini ulikuwepo kabla CCM haijaleta upumbavu wake.
 
Majimbo au mikoa si lolote kama huna taasisi imara. Kwenye hiyo clip Lissu katolea nchi zenye majimbo zingine zina hali mbaya kuliko TZ yenye mikoa. Nchi kama Congo, Zambia, Msumbiji zina majimbo ila zinapumulia mpira.
 
Hizo nchi ndio zakutolea mfano? Wapumbavu nyie
 
Majimbo ni sawa kama mikoa hii hii itageuka majimbo. Sio kufanya majimbo Tisa kama ya ukoloni..
majimbo anayosema Lissu ni sawa kabisa na yale ya Mkoloni kukiwa na tofauti ndogo sana. Kwenye majimbo ya Mkoloni kulikuwa na temi nyingi sana kila temi ikiwa inaongoza kabila fulani, ila mkuu wa jimbo alikuwa na mteule wa Gavana. Lissu anasema kuwa kila jimbo litatajitawala lenyewe kutafuta mkuu wa jimbo, ukuu wa kata na kadhalika. Weakness kubwa ya proposal ya Lissu kuhusu mfumo huo (sina uhakika kama anataka kuwa rais wa nchi ya aina hiyo) ni kuwa ukishafanya hivyo unarudishia ukabila na utemi kama mwanzo kabisa kule tulikotoka; inawezekana bsi mara moja, ile destination itakuwa hiyo.
 
Issue ni kiasi gani kinapelekwa wapi na maamuzi ya kutumia yanahusu nini. Pia accountability chini ya majimbo ni kwa wapiga kura na sio kwa raisi. Msikilize Lissu kwa umakini utaelewa anasema nini.
Hakuna nchi ambayo accountability iko kwa wananchi moja kwa moja. Accountability ni lazima iwe kwa watu wachache waliochaguliwa kwa niaba ya wananchi. Hapo Mkuu tusidanganyane. Maneno anayotoa Mgombea ni tofauti na unayotoa wewe - unaya-modify. Ndio maana tunataka mambo yawe kwenye ilani . Weka ukurasa wa hiyo ilani inayoelekeza hapa JF.
 
Kama tunamchagua gavana kwa kura na tunauwezo wa kumtoa akifurunda-hiyo siyo accountability kwa wananchi? Ilani hauwezi kuwa na details za jinsi majimbo yatakavyo operate, lakini yote niliyosema kwa mfano ndio yale Lissu anaongelea.
 
Back
Top Bottom