Chambusiso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 2,592
- 4,640
Sijui kama ilishawahi kujadiliwa humu lakini nimekuwa najiuliza sana na kukosa majibu, kwanini mfumo wa masaa wa Afrika Mashariki upo tofauti na sehemu zingine duniani? Sehemu zote siku inaanza saa 6 (0000) usiku lakini kwetu inaanza saa 1 (0700) asubuhi. Kuna sababu ya hii tofauti mahali?
Na tulipatia wapi huu mfumo na kwa nini? Tujiulize wanabodi na tunafaidika nini au tunapata hasara gani kwa hii? Karibuni kwa tafakuri.
Na tulipatia wapi huu mfumo na kwa nini? Tujiulize wanabodi na tunafaidika nini au tunapata hasara gani kwa hii? Karibuni kwa tafakuri.