Sababu kuu ni kuwa upande wetu (ikweta), tuna takriban masaa 12 ya mwanga na 12 ya giza, bila kubadilika, kwa mwaka mzima. Hivyo kutumia kigezo cha mwanga, inatabirika kirahisi zaidi, siku huanza jua likichomoza (saa moja asubuhi) na huisha likizama (saa 12 jioni).
Wenzetu muda wa jua kuchwa na kucha hubadilika kutokana na majira. Wakati wa summer muda wa jua huwa mrefu (Kuna nchi jua huwaka hadi masaa 20 kwa siku) na giza huwa fupi sana, vivyo hivyo wakati wa winter tofauti yake hutokea. Kwa mantiki hiyo, kutumia mwanga na giza kuhesabu siku sehemu hizo, inakuwa haina mantiki.