Mfumo wa NHIF kila wakati tunaambiwa uko chini, Wagonjwa wamekaa kwenye foleni

pandagichiza

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2013
Posts
5,248
Reaction score
3,663
Kila tunaambiwa mtandao uko chini tuwe na subira. Wagonjwa wamekaa kwenye foleni tangu saa mbili asubuhi.

Haya mambo ya mitandao mngeachana nayo tu naona hamkuwa tayari.

Kuanzia mapokezi, kwa daktari, pharmacy ni tabu tupu.
 
Pole .Kama mtandao uko vibaya sio kosa la NHIF. Kuwa mvumilivu kwani rekodi zako lazima ziingie humo, ndizo changamoto za teknolojia.
 
Sijui lini tutapata bima ya afya bure kama walivyotuamisha kwenye uchaguzi, maana sasa hivi hiyo kadi kwa mwaka ni balaa. Bora wewe unayo kadi vumilia hapo notiweki itarudi tu.
 
Wenye bima ndio tunaopata tabu
 
Sijui lini tutapata bima ya afya bure kama walivyotuamisha kwenye uchaguzi, maana sasa hivi hiyo kadi kwa mwaka ni balaa. Bora wewe unayo kadi vumilia hapo notiweki itarudi tu.
Ni lini walisema wanatoa bima za afya bure.

Ninachojua hata wazee na watoto ambao sera ilitaka wapewe matibabu bure sasa hivi wanahamasishqa kukata bima za iCHF ambazo ni Tsh 30,000 kqa mwaka.
 
Kila tunaambiwa mtandao uko chini muwe na subira. Wagonjwa wamekaa kwenye foleni tangu saa mbili asubuhi.

Haya mambo ya mitandao mngeachana nayo tu naona hamkuwa tayari.

Kuanzia mapokezi, kwa daktari, pharmacy ni tabu tupu
Aise
 
Pole .Kama mtandao uko vibaya sio kosa la NHIF. Kuwa mvumilivu kwani rekodi zako lazima ziingie humo, ndizo changamoto za teknolojia.
Ni kosa lao NHIF walitakiwa wawe na mfumo usiotegemea mtandao, ukiugua mikoani ambako mtandao uko kwenye nguzo ya umeme mkubwa utafanyaje!
 
iCHF ni bima za kijamii. Wanapata watu wasio kwenye mfumo rasmi. Hii mara nyingu utapata matibabu ndani ya mkoa uliokatiwa tu.

Na NHIF ni kwaajili ya watu walio kwenye mfumo rasmi.
Mkuu hii bima hata wazee wanakubaliwa?
Na je wanapata vipimo vyote na madawa?au iko selective?
 
Ni lini walisema wanatoa bima za afya bure.

Ninachojua hata wazee na watoto ambao sera ilitaka wapewe matibabu bure sasa hivi wanahamasishqa kukata bima za iCHF ambazo ni Tsh 30,000 kqa mwaka.
Hio bima ya 30,000 ubaya ni kwamba haitafanya lolote zaidi ya kutibu malaria
 
Back
Top Bottom