DOKEZO Mfumo wa SIS unatumiwa na Wakuu wa Shule kujaza wanafunzi hewa ili wapate hela

DOKEZO Mfumo wa SIS unatumiwa na Wakuu wa Shule kujaza wanafunzi hewa ili wapate hela

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mfumo wa SIS (School Information System) unatumika na Wakuu wa shule kujaza wanafunzi hewa (walioacha shule/kufukuzwa/wasioripoti) wote wanawekwa na hawaondolewi kwenye mfumo ili wapate hela nyingi kupitia mfumo wa FARRS.

Wengine wanaenda mbali zaidi, wanawachangisha wazazi michango ya walimu wa muda, wakuu wa shule wanatumia kwa mambo yasiyohusiana na walimu wa muda (binafsi) halafu wanaandaa mihutasari ya uongo na kutoa hela kupitia FARRS ili kuwalipa walimu wa muda.

Takwimu sahihi ni zinazotumwa NECTA, TAMISEMI zinatumwa takwimu za uongo(kubwa) ili hela iletwe nyingi.

Kuna shule inaitwa MIGEZI SECONDARY, ipo Wilaya ya Kibondo, kwa vidato viwili vya mtihani, tofauti kati ya Takwimu za SIS na NECTA ni wanafunzi hewa 303. Yawezekana hali Iko hivi hivi nchi nzima!
 
Huo mfumo unajazwa na mkuu wa shule unathibitishwa na WEO NA DEO na taarifa ukikosea zikashindwa kuoana unaleta query sio rahisi utengeneze
 
Huo mfumo unajazwa na mkuu wa shule unathibitishwa na WEO NA DEO na taarifa ukikosea zikashindwa kuoana unaleta query sio rahisi utengeneze
Alichoandika hapo mleta uzi ni kweli mkuu,...
Japo ni kama anawachongea wakuu wa shule, ila ukweli upo....

Takwimu Halisia za wanafunzi ni zile zinazoenda NECTA pekee...

Halafu kwa sasa, DEO na wakuu wa shule lao moja...labda hujui tu
 
Sawa
 
Back
Top Bottom