Mgahawa maarufu hapo Tabora maarufu kwa 'chotara" wahudumu awajali wateja

Ni mara mia hapo chotara, kuna moja inaitwa chioma huko kanyenye, wahudumu huwaoni unaeza ukaita mpaka ukianza kuondoka unasikia we maku unasemaje? Sishauri mtu aende pale kabisa. Kiufupi tabora bado sana asilimia kubwa ya wahudumu wako kimkakati zaidi.
Wapo kimkakati kabisaa, hasa hapo chotara naona lengo lao kubwa ni kuwaibia wateja..wakikuona ni mjanja mjanja hawakuhudumii
 
Ni mara mia hapo chotara, kuna moja inaitwa chioma huko kanyenye, wahudumu huwaoni unaeza ukaita mpaka ukianza kuondoka unasikia we maku unasemaje? Sishauri mtu aende pale kabisa. Kiufupi tabora bado sana asilimia kubwa ya wahudumu wako kimkakati zaidi.
Du uitwe maku kweli usimzawadie mtu hata kakonde kamoja katakatifu
 
Katika majukumu yangu ya kila siku leo nilipita Tabora mjini nikielekea mpanda Katavi katika hali ya kupata chochote kitu ikanibidi niulizie mgahawa ambao ninaweza kupata chakula kizuri, kulingana na uchumi wangu.

Wenyeji wakanielekeza eneo lile Kuna mgahawa Al maarufu kwa "chotara" kwa nje ya mgahawa ule Kuna vijana wanaouza vitafunwa kama maandazi, chapati na sambusa, nikachukua chapati zangu tatu kwa vijana wale na nikaingia ndani ya mgahawa, nikatafuta meza yangu nikaketi ili nisubiri huduma nyingine kutoka kwa wahudumu, mgahawa huu umesheheni wahudumu wa kike wanaovaa ushungi..

Kitu Cha ajabu niliwaita wahudumu zaidi ya mara tatu lakini wote walikuwa wakiniangalia kama sanamu la posta😁. Muda uleule niliokuwa nimekaa akaja jamaa mwingine nae akaita wahudumu zaidi mara tatu lakini wahudumu hawakutokea hata mmoja.

Shime kama Kuna wamiliki wapo humu nawapeni taarifa kuwa wahudumu wanawaharibia biashara na wanawafukuzia wateja nimeambatanisha na picha za eneo hilo..View attachment 3279002View attachment 3279002
Sasa wewe uliamua kununua chapati nje ya mgahawa sasa ndani umeingia kufanya nini kama si msumbufu! Waambie waliikuuzia chapati wakuhudumie sisi tanahudumia wateja wa ndani tu.
 
Hawo wamefunga wanahisi wakikuudumia watakosa malijali 7 peponi hutambui Hilo ungeenda zako bar flani ungepata supu kwa chapati na mikas na nyagi mo zen safari shauri yako
 
Nasema umekurupuka kwa sababu hata mazingira ya pale huyafahamu...kawaida ya ule mgahawa huwa unawahudumu wengine wanaouza vitafunwa kwa nje kwa hiyo ukinunua vitafunwa vile ni sawa na mtu alienunua ndani ya mgahawa....
Sasa kwanini ununue nje wakati ndani vipo? Huwenda ikawa kosa ni wewe kununua vitafunwa nje then ukazamanavyo ndani
 
Tarizo jamaa unaita kwa dharau unamuitaje mtu kwa ishara ya kidole kimoja wakati wenzio wanatumia vidole vyote,mimi nilikuona toka unaingia mle,ulinunua chapati kwa yule dogo mwenye tshirt nyeusi kisha ukaja mle ndani,mimi ni jamaa fulani mweusi mfupi nilikuwa karibu yako nikukushangaa unavyoita kwa kufedhehesha

Zipo CHOTARA mbili, moja ipo mtaa wa shule mkabala na sikonge rodi, na nyingine ipo njia panda kwenye mataa karibu na stand ya bus.
Hiyohiyo ya njia panda ni sehemu ya hovyo lakini bado wahudumu Wana huduma za hovyo
 
Wanazarau hapo kuna kadada kanavaa ushungi ni balaaa.
Sijui kinachofanya wawe na dharau ni kipi, viushungi venyewe wanavyovaa ni vichafu. Ukimuita kama unashida ya kumuuliza kitu yeye anahisi unataka kumtongoza
 
IMG_20250321_200019.jpg
 
Katika majukumu yangu ya kila siku leo nilipita Tabora mjini nikielekea mpanda Katavi katika hali ya kupata chochote kitu ikanibidi niulizie mgahawa ambao ninaweza kupata chakula kizuri, kulingana na uchumi wangu.

Wenyeji wakanielekeza eneo lile Kuna mgahawa Al maarufu kwa "chotara" kwa nje ya mgahawa ule Kuna vijana wanaouza vitafunwa kama maandazi, chapati na sambusa, nikachukua chapati zangu tatu kwa vijana wale na nikaingia ndani ya mgahawa, nikatafuta meza yangu nikaketi ili nisubiri huduma nyingine kutoka kwa wahudumu, mgahawa huu umesheheni wahudumu wa kike wanaovaa ushungi..

Kitu Cha ajabu niliwaita wahudumu zaidi ya mara tatu lakini wote walikuwa wakiniangalia kama sanamu la posta😁. Muda uleule niliokuwa nimekaa akaja jamaa mwingine nae akaita wahudumu zaidi mara tatu lakini wahudumu hawakutokea hata mmoja.

Shime kama Kuna wamiliki wapo humu nawapeni taarifa kuwa wahudumu wanawaharibia biashara na wanawafukuzia wateja nimeambatanisha na picha za eneo hilo..View attachment 3279002View attachment 3279002
Mkuu ni kwa nia njema tu, nunua simu
 
Back
Top Bottom