Mgawo mkali wa umeme na maji unaoendelea nchini ni wazi kabisa watendaji wa Serikali mnaihujumu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan

Wananchi Wana wazoom tu ngoja walete hizo hoja nyepesi 2025 watajua wanapendwa wao au hayati [emoji23]
Unategemea kura uwaangushe
Upige usipige wanapita tuunafikiri
Hawajui

Ova
 
Sisi tunaotengeneza ice cream na kuzigandisha mambo hayaendi [emoji1]

Ova

Maji ya kuziandaa hakuna na umeme wa kuzigandisha hakuna pia
Sa tutaponea wapi mrangi😎😎😎
 
1. Unaamini kwamba kuna tishio la ukame, na kwamba mito imepungua sana maji?!

2. Kama HUAMINI, well and good, lakini kama unaamini, unaweza kunitajia alternative ya kupata maji safi na salama kwa mahali kama Dar es salaam ni ipi inapotokea mito kupungua maji?!
 
Kama viongozi waliowekwa/waliochaguliwa na wananchi hawawezi kuja na alternatives sioni sababu ya wao kuwepo madarakani au kutuongoza.

Mito kukauka maji na ukame isiwe sababu ya ukosefu wa maji, zipo alternatives, bahati mbaya watu wapo tu, wamekaa tu maofisini wakisubiri paychecks zao. Creativity kwa mtu mweusi limekuwa tatizo kubwa.
 

Mito kupungua maji wakati wa kiangazi na mito kufurika maji wakati wa mvua sio kitu kipya, sio tukio la kushtukizwa

Ipi mipango iliyowekwa kukabiliana na wakati wa kupungua kwa maji ili kuhakikisha haiathiri maisha ya mtanzania? Kama mipango haipo au haitekelezeki basi kazi imewashinda wenye dhamana
 
Wenzetu huko kazi ikiwashinda wanaachia wengine waongoze, hawa wa kwetu wakikaa kwenye viti vyao wanakuwa miungu, hawasikilizi la mtu, wakisemwa wanatuambia tuhamie nchi jirani, hakuna uwajibikaji hata kidogo.
 
Mito kupungua maji wakati wa kiangazi na mito kufurika maji wakati wa mvua sio kitu kipya, sio tukio la kushtukizwa
TOO Defensive, Darling!
Ipi mipango iliyowekwa kukabiliana na wakati wa kupungua kwa maji ili kuhakikisha haiathiri maisha ya mtanzania? Kama mipango haipo au haitekelezeki basi kazi imewashinda wenye dhamana
This's a defensive version of saying "No alternative plan at all"!

No alternative kwa sababu tunaishi kwa kutegemea kudra za Mwenyezi Mungu...

Pawapo na mvua za kutosha za kujaza mito, maji yatapatikana kwa kiwango cha kuridhisha kule maeneo lalamishi!!

Pasipokuwa na mvua za kutosha, ndo haya yaliyopo sasa!!

Sasa kutakuwa na watu wanaomhujumu Samia if, and only if, hao watu wana uwezo wa kuleta mvua! Kinyume na hayo, wanaomhujumu SSH ni yeye mwenyewe na Serikali yake ya CCM ambayo haina njia mbadala kwa maeneo yanayotegemea maji ya kwenye mito!!

So, kwa miji kama Dar es salaam permanent solution ni moja TU: Ama serikali ivute maji kutoka Lake Victoria, au ifanye desalination, au itafute chanzo kikubwa cha maji ya ardhini. Moja kati ya hizo ndo solution na sio Wami, Ruvu, wala Mto Rufiji!!
 
Maneno mengi kuliko umeme mtaani

[emoji706]

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Yaani wewe akili zako sijui unakopaga wapi
Unaongeaongeaga na kuandikaandika vitu vya aina yako. Yaani dah, huruma
Hujaona point kati hayo alio andika? Je umejipa mda kidogo kumuelewa ?
 
"wanasema maji kwenye mabwaya yote matatu ya mepungua"

Je ni Kweli? Au wewe waonaje Khali mito inayo pereka maji huko? Hapo Ipogoro mto Ruahaha unamaji Ya kutosha
 
Hivi wale waganga wa kutengeneza mvua aliowatafuta Lowasa wamekufa au bado wako hai? Muombeni Mzee Lowasa akawatafute tena
 
Nini kifanyike ili Mama amtimue Waziri wa Maji? au ni mpaka Wananchi wafe kwa kiu?
Kwanini waziri wa maji na siyo hao wengine ambao wizara zao ndizo zimeanza kuharibu? Mnawanga mchana nyie!
 
Kwanini waziri wa maji na siyo hao wengine ambao wizara zao ndizo zimeanza kuharibu? Mnawanga mchana nyie!
Labda kama hunisomagi, kila Waziri akiboronga huwa tunashauri apumzishwe.

Hakuna Conspiracy yoyote mzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…