imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Mimi naamini vita vitakatifu vimeshaanza ndani ya CCM the begining of the end.Ila Chalamila naye siyo wa kuaminiwa!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi naamini vita vitakatifu vimeshaanza ndani ya CCM the begining of the end.Ila Chalamila naye siyo wa kuaminiwa!!
Ushamba mzigo.Muda wa Asali huu na Maendeleo binafsi ya watu.
Hayo ma umeme na maji ni maendeleo ya vitu, na maendeleo ya vitu aliondoka nayo mwendazake.
Tafta channel ya asali ununue jenereta lako, uchimbe kisima chako uache malalamiko.
We jamaa mpuuzi sana.Nini kifanyike ili Mama amtimue Waziri wa Maji? au ni mpaka Wananchi wafe kwa kiu?
Kwanini mkuu?We jamaa mpuuzi sana.
Hao kinachosababisha wabakie kama chama ni Dola tu. Siku watu wa dola wakiacha ule U-CCM hicho chama chini ya sekunde kitakuwa kimeshasambaratika.Mimi naamini vita vitakatifu vimeshaanza ndani ya CCM the begining of the end.
Sarcasim...only the brave can read btn the lines.Ushamba mzigo.
Nchi hii tumepata mzigo hatuna hata bwawa moja la Umeme. Kila jambo lazima mumpe sifa mwendazake. Mnachora picha kwenye maji, haitaonnekana kamwe.
Watanzania tutakuwa tumepata Uhuru kamili.Hao kinachosababisha wabakie kama chama ni Dola tu. Siku watu wa dola wakiacha ule U-CCM hicho chama chini ya sekunde kitakuwa kimeshasambaratika.
Kwani uongo?Ushamba mzigo.
Nchi hii tumepata mzigo hatuna hata bwawa moja la Umeme. Kila jambo lazima mumpe sifa mwendazake. Mnachora picha kwenye maji, haitaonnekana kamwe.
Ujinga huu.Wasaidizi ndio wanamhujumu mama...ila mama kama mama anaupiga mwingi
Hiki kinachoendelea kimyakimya ni mchakato wa kuturudisha kuleee miaka ilee ya 2005, 2006, 2007...... miaka ambayo Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla ilikua imepambwa na mikokoteni ilishosheheni madumu ya korie yaliyobeba maji na magari yenye matank ya maji kila kona.
Kwa kasi ya ajabu tunarudi miaka Ile ambayo mazingira yalikua yamepambwa kwa sauti za majenereta usiku na mchana
Au ndio ule mkakati wa kuutaka urais umeanza!? Acheni mambo yenu buana. Mama Samia yupo sana bado, ndio kwanza kumekucha
Hali ni mbaya sana na hatari kwa afya kwa jiji lenye wakazi wengi zaidi nchini, Dar Es Salaam. Watu tumepona kwenye corona lakini sasa mnataka kutulazimisha tufe kwa kipindupindu
Watendaji mnaohusika kwenye haya maeneo fanyeni kile kilichokua kinafanyika miaka mitano iliyopita hadi tukasahau kabisa kero ya umeme na maji. Kupewa nafasi ya kuhudumia wananchi kwa huduma muhimu kama umeme na maji halafu hao wananchi wakakosa hizo huduma ni wazi kabisa kwamba kufanya imeshindikana. Bora kuiacha office kuliko kukaa kwenye office halafu huduma asipatikane
Tanesco na idara za maji sisi wananchi tunamuamini rais wetu na yeye amewaamini nyie. Mnapopewa dhamana ya kutuhudumia halafu mnaamua kutuhujumu tutapaza sauti kwamba kazi imewashinda. Heri kuteua na kutumbua kuliko wananchi kuteseka kwa kukosa huduma za msingi tena ambazo wanazichangia kwa kodi zao wenyewe
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hasan
Kazi iendelee
Cc Wizara ya Afya Tanzania
waziri huyu ndo yule yule aliekua ana upiga mwingi awamu iliyopita...the question is what changed?Huyu Waziri wa Maji atumbuliwe.
Nadhani anamchukulia Maza poa.waziri huyu ndo yule yule aliekua ana upigw mwingi awamu iliyopita...the questions what changed?
Uongo mtupu.
Wewe kama hapo Dar es Salaam ulisahau shida ya maji na umeme miaka mitano iliyopita hauwakilishi Watanzania wengi wasio na uwezo wa kutoa ushuhuda wao hapa.
Nchi hii kuna mamilioni ya watu ambao maisha yao yote maji ya bomba ni anasa, wanayatumia kunywa na kupikia tu na yanapatikana kwa manati, hata chini ya kipenzi chenu jiwe hali hiyo haijwahi kubadilika kwao.
Aisee imenibidi nicheke sana.😂Waziri wa maji na nishati ni akina nani?!
Maan vitu vimepanda bei hadi napoteza kumbukumbu