Tetesi: Mgeja na wenzake watano kurudi CCM

Mgeja alikuwa ndio Mweka hazina wa Genge la Lowassa ilikuwa ukitaka Fungu lazima umuone huyu. 2010 ndie alitumwa na Lowasa amchukulie form ya Urais Jk ili wazidi kujipendekeza kwake
 
Mkuu falcon mombasa hata wakirudi wote maana hiyo itakuwa ni nguvu ya mungu anaisaidia cdm kuwaondoa hao wasaliti,cdm itabakia salama
 
Hivi kwa hii kasi ya.magufuli inawezekanaje CDM kubaki salama?
Sio kina mgeja tu,jiandaeni kwa makubwa zaidi!
Hakuna makubwa zaidi kama ile mlivyo mrubuni slaa akabwaga manyanga katikati ya uchaguzi mkuu mwaka jana,maccm hamna akili
 
Hatuwatakiiiiiiiiiiiiiiiiii.....


Hao ni mamluki......bora wasipokelewe kabisa !

Muasi ni muasi tuuuu!
 
Hii taarifa sio kweli kwa kila kitu. Mgeja ni LOWASSA damu, hawezi kuachana naye HATA SIKU MOJA. Kuna waliojiunga CHADEMA bila kujua kuwa Lowassa naye angekwenda huko. Hao ni kama Lembeni. Ukiniambia yeye ataomba msamaha arudi CCM naweza kuamini kwa sababu sidhani kama Mzee Lowassa angefurahi kama Lembeni angepata Ubunge. Sio Mgeja bwana, huyu hatenganishwi na Lowassa.
 
Kwa Tanzania haya sio mapya.
Vyama havina itikadi na wanachama wanafuata watu.
Mgeja hakuja upinzani, alimfuata Lowassa bahati mbaya matarajio hayajafikiwa.
 
Kuna kitu hamkijui humu
ndani Ccm ni wepesi kuliko unavyojua !!!

Wanajihami kuanzisha madam Na kuchangia wenyewe
Wanajua ni swala LA Muda tuu !!!
MTU ansema kasi ya Magufuli ;muulize IPI?

anakujibu Lowassa angeweza ???

Ni mbwembwe tu jibu kasi IPI ??

Hakuna jibu!
 
Dr. Slaa aliondoka CHADEMA kwa sababu yeye sio mnafiki. Asingeweza kukaa meza moja na mtu ambaye chama chake kilizunguka nchi nzima kuueleza umma kisahihi kabisa kuwa ndiye kiongozi wa mafisadi nchini. Kujifanya amesahau hayo na kuanza kumwona kama ni shujaa ambaye angeleta mabadiliko TZ roho yake ilikataa kwa sababu haina unafiki. Wenzake walipewa mapesa "wakabadilisha gear" na kuanza kumwita Lowassa kiongozi wa mabadiliko. Dr Slaa ilimshinda hiyo. Hapo ni nani aliyesaliti? Ni hao waliokwenda nje ya misingi ya CHADEMA au waliosimamia misingi na kujiondoa? Kwa kiasi fulani Tindu Lissu alikuwa mkweli aliposema kuwa kwa sasa adui mkubwa wa CHADEMA ni CCM hivyo hata angepatikana shetani wa kuisaidia CHADEMA kuiondoa CCM wangemkaribisha. Hivyo Lowassa alikaribishwa kama shetani ambaye angeweza kuisaidia CHADEMA kuiondoa CCM madarakani. Sasa kwa hilo Dr. Slaa "hakuwa tayari kushirikiana na shetani".
 
Nimesikia kuwa rowasa naye anarudi home....
Sijui ni kweli??
 
Wanashughulikiwa Vipi? Si Demokrasia Hii? Ccm Waache Ujinga
 
Na umesahau slaa alikuwa ccm damu,akasaliti upadre,akasaliti famelia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…