Mgogoro wa Ethiopia unadhihirisha umadhubuti wa mfumo wetu wa mikoa dhidi ya ule mfumo wa majimbo

Kwako wewe ujanja ni vita ya kupigana wenyewe kwa wenyewe? Huo sio ujanja, ni ubinafsi tu. Duniani kote hakuna nchi wanaojielewa, na wenye maendeleo ya kweli, wakaanza kupigana wao kwa wao.

Yaani ushindwe kupata maendeleo kwa hali ya amani, uje uyapate kwa kupigana nyie kwa nyie?
 
Unaona sasa?

Nyie ndio mna tatizo

Wenyeji lazima wafaidike na mali zao

Nyie hamtaki mnataka muweze kuvamia na kula mali bila wenyeji kupata chochote.

Thats unacceptable
Kwa hiyo mchaga akianzisha duka la jumla Mwanjelwa huyo ni mvamizi?
Na huyo mwenyeji kwanini hakuanzisha hilo duka na hiyo ardhi alinunua au kukodisha kutoka kwa nani?
 
Hongera umeeleza kitu cha kweli na cha maana sana. Shukran
 
Sisi mikoa yetu itakayounganishwa na kuwa ni majimbo haina ukabila. . Tofautisha Ethiopia na Tanzania
 
Vifo vyote ni expected. Kila mtu ana expect kufa wakati wo wote ambao haujui. Kila mtu ni marehemu mtarajiwa.
Hesabu za probability (chances) zina kanuni zake. Zinafanana na mchezo wa kubahatisha. Kila mchezaji ana expect kushinda bingo. Na kweli yupo anaweza kucheza mara moja tu na akapata bingo lakini yupo na ambaye atacheza zaidi ya mara million moja asiambulie kitu.

Haya kwa majirani zetu, hiko kipindi cha miezi 3 cha kusubiri na kuandaa uchaguzi mkuu unafikiri nchi itakuwaje? Unafikiri huyo makamu aliyeshika nchi kwenye kipindi hicho ataachia nchi kirahisi rahisi? Yaani ahisi kwamba kushinda uchaguzi kwake inaweza kuwa ngumu, unadhani hawezi kufanya figisufigisu ili kuchelewesha uchaguzi au uchaguzi huo kufanyika in his favour kwani mamlaka kaishayashika? Tuache kudanganyana. Katiba yetu ndiyo best. Rais wetu ndiyo mkuu wa nchi, mkuu wa watendaji na majeshi yote. Anapatikana kwa kuchaguliwa na watu wote ikimaanisha mamlaka hayo anayakabidhiwa kwa niaba yao na ni wao pekee wanaoweza kumunyang'anya mamlaka hayo kupitia uchaguzi. Wakuu wa mihimili mingine hawachaguliwi na wananchi wote na hivyo hawawezi kuwa above ya mkuu wa nchi. Huyu ndiye kakabidhiwa nchi na umma. Anapaswa kuwaangalia wote kwa niaba ya umma ambao umempa nyezo za kufanya hivyo kupitia katiba na sheria. Inashangaza mtu kama CAG kusema hawezi kuondolewa madarakani na mkuu wa nchi. Yaani CAG naye anajiona kapata madaraka hayo moja kwa moja kupitia umma (the people) kwa uchaguzi.
 
Mkoa pendekezwa wa Chato Tanzania chini ya awamu ya 5 na awamu ya 6 ni aina ya mikoa ya kikabila iliyopo huko Ethiopia ya Tigray, Oromoia n.k ipo kikabila zaidi ,inaanzishwa na madictator inapendelewa na serikali kwa kupelekewa uwanja wa ndege, hospitali, uwanja wa mpira n.k

Hivyo nchi yetu na raia wote tupinge vikali mikoa au majimbo ya kabila moja. Tujenge majimbo ya kanda yaliyo na mkakati wa kuunganisha makabila badala ya kujenga mikoa / majimbo ya kabila moja.

https://www.bbc.com › swahili › ha...
Je eneo la Chato nchini Tanzania linapaswa kuwa Mkoa au halifai


7 Jun 2021 — Hata kabla mwili wa hayati Rais John Magufuli haujaingia kaburini nyumbani kwao alikozaliwa, wazee wa Chato walimpa mtego Rais ...






https://www.mwananchi.co.tz › kitaifa
Mapendekezo Mkoa wa Chato kuwa na wilaya tano - Mwananchi


29 May 2021 — Kikao maalumu cha ushauri cha Mkoa wa Geita, kimeridhia kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Chato na kupendekeza mkoa huo mpya kuwa ...
 

..tatizo la ethiopia ni utawala wa kikandamizaji na ukabila.

..ukishakuwa na utawala wa aina hiyo haijalishi nchi ina mfumo wa majimbo au mikoa lazima kutatokea machafuko.
 
Mfumo wa majimbo kwa waafrica bado Sana...changamoto zake bado waafrika hawana uwezo wa kutatua

..mbona kuna nchi nyingi za afrika zina majimbo?

..kwa uchache ghana, nigeria, zimbabwe, angola, msumbiji, zambia...kote huko wana majimbo.

..kuna baadhi wamefanikiwa na baadhi hawajafanikiwa kuwa wamoja.
 
Kwa sababu Mimi naamini katika usawa wa binadamu. Mimi siamini kuwa eneo fulani ni la watu wa aina fulani.
Mimi naamini kwenye mfumo kama wa European Union (Tweaked a Lil bit) na siyo Jimbo lenye mikoa ambayo hata maji ya kuoga Hamna.

Naamini kwenye muunganiko wa SADC kuwa nchi moja.

I'm thinking big ... Not a petty a$$ negro.
We need to think like white people.
 
Wewe jamaa nilikuwa nakuona uko vizuri upstairs kumbe kichwa chako kimebeba maji ya nazi KATIBA ILIYOPO INATOSHA??
 
..mbona kuna nchi nyingi za afrika zina majimbo?

..kwa uchache ghana, nigeria, zimbabwe, angola, msumbiji, zambia...kote huko wana majimbo.

..kuna baadhi wamefanikiwa na baadhi hawajafanikiwa kuwa wamoja.
Cape Delgado- Msumbiji
Nigeria- Kano/Katsina


Tunachomaanisha uwezo wa kumudu mgawanyo wa majimbo na utatuzi wa changamoto zake. Haina maana kwamba haiwezekani.
 
Hapo jirani tu Zambia Rais amewahi kufariki akiwa madarakani, wapinzani wamewahi kushinda urais mara TATU na madaraka yakabadilishwana kwa amani mara zote. Usijione keki sana.
 
Malawi Rais amewahi kufariki madarakani, Rais amewahi kuondolewa urais na mahakama, upinzani umewahi kushinda urais na mambo yote hayo yamefanyika kwa amani.
 
Wewe jamaa nilikuwa nakuona uko vizuri upstairs kumbe kichwa chako kimebeba maji ya nazi KATIBA ILIYOPO INATOSHA??
Maelezo yake kuhusu majimbo yanaweza kuwa sahihi. Sema hapo alipomalizia ngoja tumuache mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…