Mgogoro wa Ethiopia unadhihirisha umadhubuti wa mfumo wetu wa mikoa dhidi ya ule mfumo wa majimbo

Mgogoro wa Ethiopia unadhihirisha umadhubuti wa mfumo wetu wa mikoa dhidi ya ule mfumo wa majimbo

Sasa hiyo sio amani, huo ni ujuha. Watu wanalalamika mioyoni. Sijajua wewe upo class gani, lakini sisi tunaotoka poor class tunajua namna nchi ilikotoka na inavyozama baharini. Waulize wafanyabiashara na wakulima namna mambo yalivyo magumu. Anyway labda kama tunaishi ilimradi tuneamka salama basi sawa. Lakini tukitaka maendeleo ya kweli, lazima tuwe na watu wanaohoji na sio kukaa. Na maumivu moyoni.
Kwako wewe ujanja ni vita ya kupigana wenyewe kwa wenyewe? Huo sio ujanja, ni ubinafsi tu. Duniani kote hakuna nchi wanaojielewa, na wenye maendeleo ya kweli, wakaanza kupigana wao kwa wao.

Yaani ushindwe kupata maendeleo kwa hali ya amani, uje uyapate kwa kupigana nyie kwa nyie?
 
Unaona sasa?

Nyie ndio mna tatizo

Wenyeji lazima wafaidike na mali zao

Nyie hamtaki mnataka muweze kuvamia na kula mali bila wenyeji kupata chochote.

Thats unacceptable
Kwa hiyo mchaga akianzisha duka la jumla Mwanjelwa huyo ni mvamizi?
Na huyo mwenyeji kwanini hakuanzisha hilo duka na hiyo ardhi alinunua au kukodisha kutoka kwa nani?
 
Habari wanajamvi,

Kama ilivyo kawaida, kufanya tafakuri ya mambo yale mtu anayoyasikia maredioni na magazetini kuhusu yanayoendelea kwenye siasa za nchi mbalimbali.

basi nami nimejikuta nikiyatafakari sana yale yanayoendelea huko Ethiopia na vita vyao vya serikali ya kitaifa na wanamgambo wa jimbo lao la tigrinya, ambapo sasa vita hivyo vimeonekana kuvuta na makundi mengine ya makabila toka majimbo tofauti na tigrinya, tena mbaya zaidi makundi hayo yameanza na kutaka kudai uhuru.

Sasa, nikakumbuka mfumo wao wa uongozi wa Ethiopia wa kutumia majimbo, na kukumbuka jinsi baadhi ya watanzania huwa wanausema mfumo wetu wa mikoa ambao mkuu wa mkoa anateuliwa na rais hivyo kufanya serikali kuu kuwa na mkono wa moja kwa moja kwenye kuongoza mkoa, ambapo ni tofauti na mfumo wa majimbo ambapo kiongozi wa mkoa anapigiwa kura

Ubaya wa majimbo ni kuwa viongozi hao wa majimbo wana kuwa na mamlaka makubwa hata yanawajaa vichwani mara nyingine na kuwa fanya kutaka kuwa juu ya serikali ya kitaifa

Mfano serikali ya jimbo la tigrinya ambalo viongozi wake ndio vinara wa kisapoti waasi wapiganao dhidi ya serikali kuu. Mbaya zaidi mfumo huo wa majimbo unatoa mamlaka ya majimbo kuunda majeshi yao, ndio yanaibuka hayo ya makundi ya kiti gray, ambayo kiukweli ni jeshi la ndani la jimbo la Tigrinya

Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti, hivi, hata siuoni mwanya wa mkoa fulani kutuletea vurugu za kujitenga ama kuanzisha mapigano ndivyo ninazidi kuu appreciate mfumo wetu wa mikoa tulio nao

Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake.

Viongozi waasisi wa taifa letu walikuwa na ujiniasi wa kipekee kabisa maana taifa hili walilolisuka baada ya kulipokea toka kwa wakoloni wamelisuka vizuri sana, ulimbukeni wa kukaa na kuona mifumo ya siasa ya wezetu ni bora zaidi ya kwetu tukiuendekeza utafanya siku moja tufumuefumue taifa hili lililosukwa vyema.
Hongera umeeleza kitu cha kweli na cha maana sana. Shukran
 
Sisi mikoa yetu itakayounganishwa na kuwa ni majimbo haina ukabila. . Tofautisha Ethiopia na Tanzania
 
Kwani vifo vitatu ni expected occurence? Unasahau 2016 tulifanya chaguzi ya marudio zenji? Kila kitu ni mipango na chaguzi zinaachana siku 90 tokea makamu ashike nadhani so within that time frame serikali inakua imejipanga.

Tuige mazuri na yale mabaya tuyaache kuliko kupinga mfumo mzima kisa tu "Ethiopia mfumo umefeli"
Vifo vyote ni expected. Kila mtu ana expect kufa wakati wo wote ambao haujui. Kila mtu ni marehemu mtarajiwa.
Hesabu za probability (chances) zina kanuni zake. Zinafanana na mchezo wa kubahatisha. Kila mchezaji ana expect kushinda bingo. Na kweli yupo anaweza kucheza mara moja tu na akapata bingo lakini yupo na ambaye atacheza zaidi ya mara million moja asiambulie kitu.

Haya kwa majirani zetu, hiko kipindi cha miezi 3 cha kusubiri na kuandaa uchaguzi mkuu unafikiri nchi itakuwaje? Unafikiri huyo makamu aliyeshika nchi kwenye kipindi hicho ataachia nchi kirahisi rahisi? Yaani ahisi kwamba kushinda uchaguzi kwake inaweza kuwa ngumu, unadhani hawezi kufanya figisufigisu ili kuchelewesha uchaguzi au uchaguzi huo kufanyika in his favour kwani mamlaka kaishayashika? Tuache kudanganyana. Katiba yetu ndiyo best. Rais wetu ndiyo mkuu wa nchi, mkuu wa watendaji na majeshi yote. Anapatikana kwa kuchaguliwa na watu wote ikimaanisha mamlaka hayo anayakabidhiwa kwa niaba yao na ni wao pekee wanaoweza kumunyang'anya mamlaka hayo kupitia uchaguzi. Wakuu wa mihimili mingine hawachaguliwi na wananchi wote na hivyo hawawezi kuwa above ya mkuu wa nchi. Huyu ndiye kakabidhiwa nchi na umma. Anapaswa kuwaangalia wote kwa niaba ya umma ambao umempa nyezo za kufanya hivyo kupitia katiba na sheria. Inashangaza mtu kama CAG kusema hawezi kuondolewa madarakani na mkuu wa nchi. Yaani CAG naye anajiona kapata madaraka hayo moja kwa moja kupitia umma (the people) kwa uchaguzi.
 
Mkoa pendekezwa wa Chato Tanzania chini ya awamu ya 5 na awamu ya 6 ni aina ya mikoa ya kikabila iliyopo huko Ethiopia ya Tigray, Oromoia n.k ipo kikabila zaidi ,inaanzishwa na madictator inapendelewa na serikali kwa kupelekewa uwanja wa ndege, hospitali, uwanja wa mpira n.k

Hivyo nchi yetu na raia wote tupinge vikali mikoa au majimbo ya kabila moja. Tujenge majimbo ya kanda yaliyo na mkakati wa kuunganisha makabila badala ya kujenga mikoa / majimbo ya kabila moja.

https://www.bbc.com › swahili › ha...
Je eneo la Chato nchini Tanzania linapaswa kuwa Mkoa au halifai

7 Jun 2021 — Hata kabla mwili wa hayati Rais John Magufuli haujaingia kaburini nyumbani kwao alikozaliwa, wazee wa Chato walimpa mtego Rais ...
Mkoa wa Chato from www.bbc.com

1636811745516.pnghttps://www.mwananchi.co.tz › kitaifa
Mapendekezo Mkoa wa Chato kuwa na wilaya tano - Mwananchi

29 May 2021 — Kikao maalumu cha ushauri cha Mkoa wa Geita, kimeridhia kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Chato na kupendekeza mkoa huo mpya kuwa ...
 
Duuuh 😳😳😳

Hayati Meles Zenawi alitokea Tigray......aliitawala hiyo nchi kwa MKONO WA CHUMA......

Unajua ni kwanini alifanya hayo ?!!!

Kwa sababu Ethiopia ni nchi ya kikabila na matabaka....matabaka makubwa ni OROMO na AMHARA ambao huwa wanadai "share" kubwa kwa sababu ya WINGI wao .....Meles Zenawi aliiongoza nchi hiyo kwa MKONO WA CHUMA Kama afanyavyo ABIY AHMED.....na la kushangaza ABIY AHMED ni mchanganyiko wa kutoka OROMO na AMHARA....ndugu zake hao wanamuona kama mtu msaliti aliyewageuka....wao walitegemea ANGEWABEBA KIKANDA......

Ikumbukwe alipoondoka Meles Zenawi Watigrinya walikuwa ni KABILA hodhi ya kila eneo la kimkakati nchini Ethiopia ijapokuwa ni kabila DOGO.........

Leo wameungana(ajabu kabisa) wanamshambulia ndugu yao Abiy Ahmed wakiwa bega kwa bega na kundi lililofaidika kipindi cha hayati Zenawi(TPLF)....

Hapa ndipo tunapopinga Sera za MAJIMBO kwani hutokea siku isiyo na jina WANASIASA kwa tamaa na ULAFI WAO huiingiza nchi matatizoni....wanaoumia ni wazee ,wanawake na watoto!!!!

SIEMPRE JMT

..tatizo la ethiopia ni utawala wa kikandamizaji na ukabila.

..ukishakuwa na utawala wa aina hiyo haijalishi nchi ina mfumo wa majimbo au mikoa lazima kutatokea machafuko.
 
Mfumo wa majimbo kwa waafrica bado Sana...changamoto zake bado waafrika hawana uwezo wa kutatua

..mbona kuna nchi nyingi za afrika zina majimbo?

..kwa uchache ghana, nigeria, zimbabwe, angola, msumbiji, zambia...kote huko wana majimbo.

..kuna baadhi wamefanikiwa na baadhi hawajafanikiwa kuwa wamoja.
 
Kuna jimbo lolote linalokataza yeyote kufungua duka kokote?

Au unajenga artificial problem kutoka kwenye ubongo wako binafsi?

Wewe una tatizo gani na jimbo likiwa na viongozi wake wa kuchaguliwa ,waendeshe eneo lao kwa sera zao wanazoona wao,na kulinda maliasili zao kwa staili wanayopenda wao,na wapange jinsi ya kufaidika na maliasili zao kwanza kabla wageni hawazila,na pia kujenga sheria zao za kuwasaidia kwenye eneo lao wao,na kua na bunge lao la kudiscuss mambo yanayowahusu wao,etc

Wewe una tatizo na hilo kwa sababu gani?
Kwa sababu Mimi naamini katika usawa wa binadamu. Mimi siamini kuwa eneo fulani ni la watu wa aina fulani.
Mimi naamini kwenye mfumo kama wa European Union (Tweaked a Lil bit) na siyo Jimbo lenye mikoa ambayo hata maji ya kuoga Hamna.

Naamini kwenye muunganiko wa SADC kuwa nchi moja.

I'm thinking big ... Not a petty a$$ negro.
We need to think like white people.
 
Yaani baada ya kukupa mifano yote hiyo bado unang'ang'ana tu ?!! [emoji1787][emoji1787]

Ok.....

Sababu zinazosababisha baadhi ya majimbo kutaka kujitenga zinashahabiana duniani kote....."mgawanyo wa resources" ukiwa unaongoza.......

✓Majimbo ambayo yana raslimali kubwa huona yanatumika kubeba majimbo mengine na kwa kuwa wanaona hawawahitaji wengine basi hutaka kujitenga(Tigray ,Katanga ).

Kuna la WINGI wa watu (population demographic) mathalani Jimbo la OROMIA na AMHARA nchini Ethiopia.......

Kwa hiyo ndani ya Sera za MAJIMBO inaweza kupita miaka mingi ya UTULIVU ila iko siku tu historia inaweza kubadililishwa kwa sababu hizo nilizoziorodhesha hapo juu......

SIEMPRE JMT
KATIBA ILIYOPO INATOSHA
Wewe jamaa nilikuwa nakuona uko vizuri upstairs kumbe kichwa chako kimebeba maji ya nazi KATIBA ILIYOPO INATOSHA??
 
..mbona kuna nchi nyingi za afrika zina majimbo?

..kwa uchache ghana, nigeria, zimbabwe, angola, msumbiji, zambia...kote huko wana majimbo.

..kuna baadhi wamefanikiwa na baadhi hawajafanikiwa kuwa wamoja.
Cape Delgado- Msumbiji
Nigeria- Kano/Katsina

Tunachomaanisha uwezo wa kumudu mgawanyo wa majimbo na utatuzi wa changamoto zake. Haina maana kwamba haiwezekani.
 
Hapo jirani tu Zambia Rais amewahi kufariki akiwa madarakani, wapinzani wamewahi kushinda urais mara TATU na madaraka yakabadilishwana kwa amani mara zote. Usijione keki sana.
Nasirimgambo uko sahihi kabisa. Katiba yetu ni bora na madhubuti kuliko barani Afrika. Ushahidi mwingine ni kile kilichotupata mwezi March cha kupotelewa ghafla kwa rais aliyekuwa madarakani. Jambo kama hili lingalitokea kwa majirani zetu ambao CDM huwa inawasifia kuwa na katiba mpya bora, sijui hali ya huko ingalikuwaje. Kwani huko rais wa nchi na makamu wake hawako chungu kimoja na hawatoki chama kimoja cha siasa. Katiba yetu ilituvusha salama salimini.

Katiba yetu kwa miaka yote imekuwa ikituvusha salama salimini kwenye chaguzi kuu zote. Imekuwa ikifanyiwa updates (marekebisho) ili kwenda na wakati kama ambavyo katiba za nchi zilizoendelea zimekuwa zikifanyika hususani ya USA ni ya mwaka 1780 yenye updates lukuki. UK hawana katiba, wao wanaongozwa na sheria tu.
 
Malawi Rais amewahi kufariki madarakani, Rais amewahi kuondolewa urais na mahakama, upinzani umewahi kushinda urais na mambo yote hayo yamefanyika kwa amani.

Back
Top Bottom