Mgogoro wa Ethiopia unadhihirisha umadhubuti wa mfumo wetu wa mikoa dhidi ya ule mfumo wa majimbo

Malawi Rais amewahi kufariki madarakani, Rais amewahi kuondolewa urais na mahakama, upinzani umewahi kushinda urais na mambo yote hayo yamefanyika kwa amani.
Nilikuuliza swali kama hili wakati Fulani. Why Zambia inaweza kupita ktk hali ya kisiasa kama hiyo? Nikafatilia kidogo nikagundua kwao ni kawaida hata Keneth Kaunda aliondoka madarakani akaenda jela. So walipitia kipindi cha kuwafanya waone aliyepo na atakayekuja kuna utifauti fulani. Hivyo siyo kwa sababu ya uwepo au kutokuwepo kwa majimbo.
 
Kitu gani kilikufanya umuone yuko vizuri upstairs huyu sycophant siempre siempre?!
Wewe jamaa nilikuwa nakuona uko vizuri upstairs kumbe kichwa chako kimebeba maji ya nazi KATIBA ILIYOPO INATOSHA??
 
Kwa nini kwetu sio kawaida?
 
Mkuu, nimekusoma nikiwa ninaielewa mada yako hadi nilipofika kwenye mistari hii:
"Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti..."

Hilo nadhani hukuliwaza kwa kina, kwa sababu utulivu unaousema wewe, kiuhakika siyo utulivyo hasa! Sitalielezea hili, lakini nina hakika hata wewe unaweza ukawa unajiuliza kama tulichonacho sasa ni utulivu kweli au la! Kukosekana kwa vurugu, huku wanaochochea pawepo na vurugu ni watu walewale wanaotakiwa kulinda hali ya usalama wa nchi yetu, sioni kwamba hilo ni jambo la kujivunia hasa.

Hata hivyo, ninakubaliana nawe kwenye jambo la mikoa na/au shirikisho. Mfumo wetu kama ulivyoanzishwa ulitusaidia sana kuanza kuondokana na matatizo yanayowakabili nchi mbalimbali, hasa Afrika, kama hiyo Ethiopia, Nigeria..., Kenya wao wanadhani kuwa na mikoa ya kikabila kunawasaidia, lakini sidhani kuwa ni hivyo.

Nikiachana na kuandika gazeti humu, jambo ninaloliona juu ya mfano wa Ethiopia, na ambalo pengine linaweza kuwa fundisho kwetu ni hili ambalo sikulitegemea kabisa, la jeshi la nchi hiyo kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na waasi hawa. Tigray ni kasehemu kadogo sana ka nchi hiyo, pamoja na kwamba ndiko kalikuwa kanashikilia utawala wa nchi hiyo kwa miaka kadhaa iliyopita. Haka kasehemu pamoja na udogo wake kameweza kuwayumbisha sana Ethiopia kama nchi.

Je, na sisi tuwe tayari, KiZanzibar ketu kakicharuka? Au mbaya zaidi: Kanchi kadogo jirani nasi (sitaki kukataja) katakapokuwa tayari kututoa kamasi hatutakuwa na njia ya kujitetea?
Najua sifa zetu mara nyingi tunazo midomoni. Ethiopia pia walidhani wapo imara sana.

Sibezi chochote, lakini hii ni tahadhari tu!
 
Unajua kwa Nini kabla ya Abby migogoro hii haikuwa na Nguvu au haikuwepo? Ni kwa sababu wenzao Watigray walibalance uongozi bila ubaguzii.
Si kweli mkuu. Ethiopia kabila lenye watu wengi l ni waolomi. Lkn kwa miaka mingi hawa watu wamekuwa wakibaguliwa kwenye nyadhifa mbalimbali serikalini (sababu za kihistoria ni kwamba walichelewa kuchangamkia elimu kulliko wenzao watigrei)

Sasa watigrei wakawa wanabebana ktk kila sekta wakawa wao. Jeshini ndiyo usiseme.

Miaka imepita mingi. Mungu jalia Abby muOlomia akaingia madarakani watigrei (wachache) hawakupnda. Wakati waolomia (wengi wakafurahia na wakawa na matumaini makubwa kwamba sasa muOlomia mwenzao atawabeba.

Watigrei wakaliqnzisha Abby akatumia nguvu akawatuliza. Sasa Abby akaona atafanyaje ili cheo chake kiwe salama. Akawapuuza waolomia na kuwapavhika watigrei kwenye nyadhifa. Waolomia wamechukia ndiyo maana wameungana na watigrei wasiopenda muOlomia kuwa kiongozi wa nchi hata kama anagawa vyeo kwenye kabila lao. Vita ya sasa Abby hachomoki.
 
Majimbo yanaweza kuwa ni kichocheo, hata kama siyo sababu.

Mstari wa mwisho hauongezi uzito wowote katika uliyoandika hapo.
 
Umempa darasa zuri huyo jamaa ambaye hakuwa na ufahamu wowote juu ya Ethiopia, lakini kama ilivyo kawaida yetu waTz, kaeleza kama yeye anaijua vyema sana Ethiopia, kumbe hajui kitu!
 
We we no Jenerali Ulimwengu was kesho. Umedadavua vema.

Hawa ndugu zetu wansalalamika hawatoweza kupata majibu ya chanzo cha mgogoro was sasa was Ethiopia na kwengineko hadi pale watakapouliza chanzo cha machafuko Ethiopia ni nini; in serikali ya majimbo au chanzonini.

Kwa ufupi historia ya machafuko ethiopia ilianza kabla ya serikali za majimbo. Na chanzo cha serikali ya majimbo ni pale serikali zilizopita kutokuwa na uwiano sawa wa madaraka kati ya jamii zinazounda taifa LA Ethiopia. Ni kama hapa tz uone labda wakatoliki au waasia ndio wameshika 90% ya nafasi zote za kufanya maamuzi na teuzi. Ktk hali kama hiyo ndipo serikali mpya ikaamua kuundwa kwa serikali ya majimbo. Mgogo uliopo sasa unatokana na kabila hili lililoshika 90% ya madaraka kuona kuwa wao ndio wanaostahili kuendelea kushika madaraka na hivyo wanataka kurejeshwa ktk nafasi hizo au jimbo lao lijitenge.

Hali kama hii yaweza kutokea nchi yyt kwani wenye kuanzisha machafuko ni wale wanaonyamg'anywa tonge (ccm) na kuhiona hawastahili kunyang'anywa
 
siokweli kua hakuna vikundi viovu isipokua vinadhibitiwa na mfumo bora uliopo.
kuna system ambayo inajidhibit na kupata taarifa kwa urahisi kutoka ngazi ya mwenyekit wa kitongoji,kijiji,kata, wilaya,mkoa hadi taifa.
kwenye mifumo ya majimbo ni ngumu sana kudhibiti hivi vikundi.
lakin pia wakitokea viongozi wenye tamaa ni lahisi huyumbishwa.

labda nikupe mfano mdogo tu..!

chadema mlisema mkishika madalaka mtaanza na majimbo ma 5 hadib10 tu kwa tanzania nzima.

unafikili uaweza kudhibiti baadhi ya hali za kiusala?

kwa ufupi jalibu kuchunguza.afrilika nzima nchi zote zenye migogoro ya aina hii ipo kwenye mifumo ya majimbo. wewe bado hutaki kujifunza tu?

kabla ya kuingia kwenye mifumo hii kwa africa .kwanza wajifunze,wakubali kuelewa,kuijua democlasia ,na viongozi wajue haki za wanaowaongoza.

kama leo mboe anahamasisha kudai katiba mpya ,viongozi waliopo madalakani wanamziba mdomo kwa kupewa kesi kubwa bila ya aibu. unafikilia nini juu ya afrika na tanzania yako mkuu.

waafrika bado wana usokwe ndani yetu. capacit brain bado ipo chini sana.
kunavitu hatutakiwi kuvikulupukia.
 
Wa
Yaani ikitokea marais 3 wanakufa ndani ya kipindi kimoja cha utawala basi nchi iingie gharama za uchaguzi mara 3 Khaaa 😳🤣🤣
Wazo la kijinga. Katiba mbovu ndiyo imepelekea mtu ambaye hakuwahi hata kuwaza kuwa rais sasa ndiye Rais. Yaani hata hajawahi kuwa hata waziri wa serikali ya muungano leo anaendesha nchi. Anajua nini zaidi ya kushikwa akili.!?
 
You must be a fool to believe that policy failed at the ballot box.
 
Hayati Kaunda aliweka precedent kama ambavyo hayati Jerry Rawlings wa Ghana na yule wa Malawi Kamuzu, kitu ambacho hayati Nyerere alikataa kufanya kule Zanzibar. Kaunda angekataa kuachia madaraka angeweza , Jerry pia angeweza kule Ghana kuhakikisha mgombea wa chama chake anatangazwa. Nyerere alikataa hilo lisitokee Zanzibar 1995, kwa hiyo kinachotokea Zanzibar leo ni zao la dhambi ile. Je, kama kipande kile kidogo cha Zanzibar wako tayari kuua watu ili wasikiachie, watakuwa tayari kuliachia pande kubwa la Bara!? Jibu ni hapana.
Huko kwingine wazee wa TaifA walishaonesha mfano kuwa kuachia madaraka ni jambo sahihi unaposhindwa uchaguzi.
 
hahahahahahahahahahahahahahahahah.............

nasikitika tu kua sina wakubwa. mimi mwenyewe mkulingwa mkuu.

lakini pia mimi sio mwandishi ,siku zote nasema.

ila sawa nitajitahidi kutafuta mwalimu wa uandishi mkuu.
 
Tigray ni kasehemu kadogo ila chenye watu wenye ushirikianao mkubwa sana na wanaojivunia historia yao. TPLF ya Tigray ndio iliyopinga utawala wa Derg wa dikteta Mengistu Haile Mariam tangu mwanzo na Watigrinya ndio waliokuwa Kiongozi wa kuwaunganisha na kuyaongoza makabila mengine makubwa kumuondoa Mengistu mwaka 1991.

Ukienda Rwanda utakuta Watusi ndio wachache ila ndio wamehodhi madaraka yote makubwa ya nchi hiyo kabla na baada ya ukoloni.

Makaburu walikuwa chini ya asilimia 10 ya watu wote wa Africa Kusini ila waliweza kulitawala taifa la watu weusi kwa zaidi ya nusu karne.

China wanachama wa Chama cha kikomonisti ni milioni 95 tu ila wameweza kuwatiisha raia bilioni 1.4

Power juu watu wengine ni suala la "organization na cooperation" na wala sio suala la wingi.

Abiy Ahmed alikuwa "naive" kufikiri angeweza kuwapoka Watigrinya kirahisi na kwa muda mfupi nguvu na fursa walizokuwa nazo muda mrefu bila kuleta mtafaruku mkubwa. Ilihitajika mkakati smart na wa muda mrefu wa kisiasa kufanya hivyo, bahati mbaya Abiy Ahmed ni mtu "smart" sana ila sio katika uwanja wa siasa na historia "complicated" ya Ethiopia, kwa kifupi alifanya mambo mengi kwa kukurupuka bila kujipanga.
 
Haya kwa majirani zetu, hiko kipindi cha miezi 3 cha kusubiri na kuandaa uchaguzi mkuu unafikiri nchi itakuwaje? Unafikiri huyo makamu aliyeshika nchi kwenye kipindi hicho ataachia nchi kirahisi rahisi
Unaijua mahakama ya Kenya?? Wamezuia hadi BBI ambayo ndio ilikua succession management ya Kenyatta na Odinga most powerful men in Kenya ila wameangushwa.

Chaguzi ya 2017 Ilifutwa na Rais alikua madarakani ndio sembuse makamu??

Hapa Afrika mashariki lazma tukubali kwenye suala la katiba na uhuru wa mihimili, Kenya haina mfano!!
Inashangaza mtu kama CAG kusema hawezi kuondolewa madarakani na mkuu wa nchi. Yaani CAG naye anajiona kapata madaraka hayo moja kwa moja kupitia umma (the people) kwa uchaguzi
Yes kama unafahamu utawala bora the uwajibikaji na uhuru wa vyombo vya umma ni muhimu. Mfano Rais akiwa na uwezo wa kumtumbua anayemkagua kuna uhuru hapo? Hvi bajeti ya CAG ikipangwa na wizara kuna uhuru hapo? Lakini kenya kuanzia DPP,CAG,Korti,Bunge,DCI,ni independent entities na hawaingiliwi na yeyote. Bongo DPP amewahi pingana na Rais? Au Bunge limewahi pinga bajeti ya serikali au teuzi ya Rais??

Nitajie kitu kimoja tu ambacho katiba ya TZ is better than Kenya kwenye uwajibikaji na uhuru wa vyombo?
 
Sehemu kubwa ya andiko lako; hasa hiyo ya "organization and cooperation" ninakubaliana na wewe; ila unapokuja kwenye hiyo mifano mbalimbali uliyotoa kunakuwa na tofauti, yote haiwezi kushabihiana; hasa inapokuja kwenye kuwakandamiza watu wengine, utility ya umoja na mshikamano huo unakuwa na walakini, kwani una ukomo wake.
Kumbuka, umoja na mshikamano siyo 'exclusive', wengine pia wanaweza kuukwaa na kuutumia dhidi ya hao wanaowakandamiza, kama hiyo issue ya Makaburu.

Katika swala la Ethiopia yenyewe, hata hao Tigray wakati wao ulikuwa umepita kama ilivyokuwa tayari imejionyesha kwa matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea hasa sehemu za Oromo. Kwa hiyo huwezi kumlaum Abiy katika hilo, ilikuwa tayari muda wake umewadia.

Ninakubaliana nawe Abiy ni 'smart', na ninamatumaini hili ni swala la muda, litarekebishika. Watu waliozoea kutawala wengine sio rahisi kukubali kujishusha kuwa sawa na wengine waliokuwa wanatawaliwa.
 
Get to know a history of a country before getting into such a cacophonous writing

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
kichocheo kiaje?

Elezea hiyo process jimbo linaanza mgogoro na mtu

Shida ni pale local people are abused by the federal government bila haki ndio shida
Sikusikii ukizungumzia "shida ya local people used to abuse other communities when power was on their side"!

"Kichocheo kiaje"? - wakati kundi la watu katika eneo moja wanapojitambua kuwa wao wanahaki zaidi ya wengine, au sifa ya kipekee wanayojiona kuwa nayo wanayodhani inawafanya wawe zaidi ya wengine wasiokuwa eneo lao, hicho kinaweza kuwa kichocheo muhimu ya kuleta vurugu ndani ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…