Mgogoro wa Ethiopia unadhihirisha umadhubuti wa mfumo wetu wa mikoa dhidi ya ule mfumo wa majimbo

Mgogoro wa Ethiopia unadhihirisha umadhubuti wa mfumo wetu wa mikoa dhidi ya ule mfumo wa majimbo

Malawi Rais amewahi kufariki madarakani, Rais amewahi kuondolewa urais na mahakama, upinzani umewahi kushinda urais na mambo yote hayo yamefanyika kwa amani.
Nilikuuliza swali kama hili wakati Fulani. Why Zambia inaweza kupita ktk hali ya kisiasa kama hiyo? Nikafatilia kidogo nikagundua kwao ni kawaida hata Keneth Kaunda aliondoka madarakani akaenda jela. So walipitia kipindi cha kuwafanya waone aliyepo na atakayekuja kuna utifauti fulani. Hivyo siyo kwa sababu ya uwepo au kutokuwepo kwa majimbo.
 
Kitu gani kilikufanya umuone yuko vizuri upstairs huyu sycophant siempre siempre?!
Wewe jamaa nilikuwa nakuona uko vizuri upstairs kumbe kichwa chako kimebeba maji ya nazi KATIBA ILIYOPO INATOSHA??
 
Kwa nini kwetu sio kawaida?
Nilikuuliza swali kama hili wakati Fulani. Why Zambia inaweza kupita ktk hali ya kisiasa kama hiyo? Nikafatilia kidogo nikagundua kwao ni kawaida hata Keneth Kaunda aliondoka madarakani akaenda jela. So walipitia kipindi cha kuwafanya waone aliyepo na atakayekuja kuna utifauti fulani. Hivyo siyo kwa sababu ya uwepo au kutokuwepo kwa majimbo.
 
Habari wanajamvi,

Kama ilivyo kawaida, kufanya tafakuri ya mambo yale mtu anayoyasikia maredioni na magazetini kuhusu yanayoendelea kwenye siasa za nchi mbalimbali.

basi nami nimejikuta nikiyatafakari sana yale yanayoendelea huko Ethiopia na vita vyao vya serikali ya kitaifa na wanamgambo wa jimbo lao la tigrinya, ambapo sasa vita hivyo vimeonekana kuvuta na makundi mengine ya makabila toka majimbo tofauti na tigrinya, tena mbaya zaidi makundi hayo yameanza na kutaka kudai uhuru.

Sasa, nikakumbuka mfumo wao wa uongozi wa Ethiopia wa kutumia majimbo, na kukumbuka jinsi baadhi ya watanzania huwa wanausema mfumo wetu wa mikoa ambao mkuu wa mkoa anateuliwa na rais hivyo kufanya serikali kuu kuwa na mkono wa moja kwa moja kwenye kuongoza mkoa, ambapo ni tofauti na mfumo wa majimbo ambapo kiongozi wa mkoa anapigiwa kura

Ubaya wa majimbo ni kuwa viongozi hao wa majimbo wana kuwa na mamlaka makubwa hata yanawajaa vichwani mara nyingine na kuwa fanya kutaka kuwa juu ya serikali ya kitaifa

Mfano serikali ya jimbo la tigrinya ambalo viongozi wake ndio vinara wa kisapoti waasi wapiganao dhidi ya serikali kuu. Mbaya zaidi mfumo huo wa majimbo unatoa mamlaka ya majimbo kuunda majeshi yao, ndio yanaibuka hayo ya makundi ya kiti gray, ambayo kiukweli ni jeshi la ndani la jimbo la Tigrinya

Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti, hivi, hata siuoni mwanya wa mkoa fulani kutuletea vurugu za kujitenga ama kuanzisha mapigano ndivyo ninazidi kuu appreciate mfumo wetu wa mikoa tulio nao

Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake.

Viongozi waasisi wa taifa letu walikuwa na ujiniasi wa kipekee kabisa maana taifa hili walilolisuka baada ya kulipokea toka kwa wakoloni wamelisuka vizuri sana, ulimbukeni wa kukaa na kuona mifumo ya siasa ya wezetu ni bora zaidi ya kwetu tukiuendekeza utafanya siku moja tufumuefumue taifa hili lililosukwa vyema.
Mkuu, nimekusoma nikiwa ninaielewa mada yako hadi nilipofika kwenye mistari hii:
"Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti..."

Hilo nadhani hukuliwaza kwa kina, kwa sababu utulivu unaousema wewe, kiuhakika siyo utulivyo hasa! Sitalielezea hili, lakini nina hakika hata wewe unaweza ukawa unajiuliza kama tulichonacho sasa ni utulivu kweli au la! Kukosekana kwa vurugu, huku wanaochochea pawepo na vurugu ni watu walewale wanaotakiwa kulinda hali ya usalama wa nchi yetu, sioni kwamba hilo ni jambo la kujivunia hasa.

Hata hivyo, ninakubaliana nawe kwenye jambo la mikoa na/au shirikisho. Mfumo wetu kama ulivyoanzishwa ulitusaidia sana kuanza kuondokana na matatizo yanayowakabili nchi mbalimbali, hasa Afrika, kama hiyo Ethiopia, Nigeria..., Kenya wao wanadhani kuwa na mikoa ya kikabila kunawasaidia, lakini sidhani kuwa ni hivyo.

Nikiachana na kuandika gazeti humu, jambo ninaloliona juu ya mfano wa Ethiopia, na ambalo pengine linaweza kuwa fundisho kwetu ni hili ambalo sikulitegemea kabisa, la jeshi la nchi hiyo kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na waasi hawa. Tigray ni kasehemu kadogo sana ka nchi hiyo, pamoja na kwamba ndiko kalikuwa kanashikilia utawala wa nchi hiyo kwa miaka kadhaa iliyopita. Haka kasehemu pamoja na udogo wake kameweza kuwayumbisha sana Ethiopia kama nchi.

Je, na sisi tuwe tayari, KiZanzibar ketu kakicharuka? Au mbaya zaidi: Kanchi kadogo jirani nasi (sitaki kukataja) katakapokuwa tayari kututoa kamasi hatutakuwa na njia ya kujitetea?
Najua sifa zetu mara nyingi tunazo midomoni. Ethiopia pia walidhani wapo imara sana.

Sibezi chochote, lakini hii ni tahadhari tu!
 
Unajua kwa Nini kabla ya Abby migogoro hii haikuwa na Nguvu au haikuwepo? Ni kwa sababu wenzao Watigray walibalance uongozi bila ubaguzii.
Si kweli mkuu. Ethiopia kabila lenye watu wengi l ni waolomi. Lkn kwa miaka mingi hawa watu wamekuwa wakibaguliwa kwenye nyadhifa mbalimbali serikalini (sababu za kihistoria ni kwamba walichelewa kuchangamkia elimu kulliko wenzao watigrei)

Sasa watigrei wakawa wanabebana ktk kila sekta wakawa wao. Jeshini ndiyo usiseme.

Miaka imepita mingi. Mungu jalia Abby muOlomia akaingia madarakani watigrei (wachache) hawakupnda. Wakati waolomia (wengi wakafurahia na wakawa na matumaini makubwa kwamba sasa muOlomia mwenzao atawabeba.

Watigrei wakaliqnzisha Abby akatumia nguvu akawatuliza. Sasa Abby akaona atafanyaje ili cheo chake kiwe salama. Akawapuuza waolomia na kuwapavhika watigrei kwenye nyadhifa. Waolomia wamechukia ndiyo maana wameungana na watigrei wasiopenda muOlomia kuwa kiongozi wa nchi hata kama anagawa vyeo kwenye kabila lao. Vita ya sasa Abby hachomoki.
 
Hakuna

Civil wars hazijengwi na MAJIMBO

Vita ya Burundi sababu sio majimbo
Vita DRC sababu sio majimbo
Vita Angola sababu sio majimbo
etc

Nipe nchi sababu ni "majimbo"!

Na nchi zenye vita unazodai zipo ngapi?

Wapumbavu nyie...acheni fear mongering!
Majimbo yanaweza kuwa ni kichocheo, hata kama siyo sababu.

Mstari wa mwisho hauongezi uzito wowote katika uliyoandika hapo.
 
Si kweli mkuu. Ethiopia kabila lenye watu wengi l ni waolomi. Lkn kwa miaka mingi hawa watu wamekuwa wakibaguliwa kwenye nyadhifa mbalimbali serikalini (sababu za kihistoria ni kwamba walichelewa kuchangamkia elimu kulliko wenzao watigrei)

Sasa watigrei wakawa wanabebana ktk kila sekta wakawa wao. Jeshini ndiyo usiseme.

Miaka imepita mingi. Mungu jalia Abby muOlomia akaingia madarakani watigrei (wachache) hawakupnda. Wakati waolomia (wengi wakafurahia na wakawa na matumaini makubwa kwamba sasa muOlomia mwenzao atawabeba.

Watigrei wakaliqnzisha Abby akatumia nguvu akawatuliza. Sasa Abby akaona atafanyaje ili cheo chake kiwe salama. Akawapuuza waolomia na kuwapavhika watigrei kwenye nyadhifa. Waolomia wamechukia ndiyo maana wameungana na watigrei wasiopenda muOlomia kuwa kiongozi wa nchi hata kama anagawa vyeo kwenye kabila lao. Vita ya sasa Abby hachomoki.
Umempa darasa zuri huyo jamaa ambaye hakuwa na ufahamu wowote juu ya Ethiopia, lakini kama ilivyo kawaida yetu waTz, kaeleza kama yeye anaijua vyema sana Ethiopia, kumbe hajui kitu!
 
Nidhamu ya woga ndo inafanya CCM kuogopa mfumo wa majimbo.
Faida za mfumo wa majimbo ni lukuki kuliko hasara zake.
Imagine jimbo la victoria (MWANZA, SHINYANGA,MARA,KAGERA) wasimamie rasilimali zao kwa ajili ya wananchi wao.
Bulyanhulu,almasi,ziwa Victoria, serengeti.
Jimbo la kaskazini (Arusha,Kilimanjaro,Tanga)
Wasimamie rasilimali zao mlima,mbuga,bandari,tanzanite.
JIMBO LA KUSINI (Mtwara,lindi,Ruvuma)
Wasimamie Korosho,Gesi,Mawese,Tumbaku.
Jimbo la Nyanda za juu kusini (Iringa,Mbeya,Songwe)
Wasimamie wenyewe rasilimali zao Kilimo cha mazao ya chakula, kilimo cha miti.
Jimbo la Pwani (Dar es Salaam, Pwani)
Wasimamie rasilimali zao Pwani ni eneo la Viwanda, Bandari ya Dar.
ETC.
na majimbo mengine yoote.
DODOMA IBAKI KUWA JIMBO HURU. FREE STATE SHUGHULI ZOTE ZA SERIKALI KUU ZIWE ZINAFANYIKA DODOMA BILA KUATHIRIWA NA SERIKALI ZA MAJIMBO.
Serikali kuu iwe msimamizi wa shughuli za serikali za majimbo...
Serikali za majimbo ziwe na maamuzi juu ya shughuli kwayo.
CCM wanafaidika sana na huu mfumo wa mikoa kwa sababu unaendeleza umaskini wa kupindukia mtaji wa CCM ni masikini the so called Wanyonge... Uwepo wa wanyonge wengi ndo uhai wa CCM.
FAIDA YA MAJIMBO NI FREE AND FAIR COMPETITION MAJIMBO YATAPAMBANA KUVUTIA WAWEKEZAJI MFANO JIMBO LA KASKAZINI LITAPAMBANA KUVUTIA WATALII... shughuli za kuvutia watalii hazitasimamiwa na TANAPA BALI NA TOURISM DEPARTMENT YA JIMBO HUSIKA.
JIMBO LA KASKAZINI LITAPAMBANA KUHAKIKISHA WANAKUWA NA KILIMANJARO AIRWAYS.

HUU MFUMO WA MAJIMBO NI HATARI SANA KWA UHAI WA CCM KWANI LITAWAFUMBUA MACHO HADI MAJIMBO YENYE RASILIMALI CHACHE KUPAMBANA.
CCM hawahitaji nchi hii iwe na raia wengi matajiri ndo maana wamachinga,bodaboda,wanaobadilisha fedha za kigeni walisumbuliwa sana kipindi cha mwendazake.
Mfumo wa sasa wa mikoa umewekwa kuhakikisha unaipa pumzi CCM.
Mtaji wa CCM ni umaskini,ujinga na maradhi. Hivi vikitoweka na CCM itatoweka.

#KATIBAMPYANISASA
We we no Jenerali Ulimwengu was kesho. Umedadavua vema.

Hawa ndugu zetu wansalalamika hawatoweza kupata majibu ya chanzo cha mgogoro was sasa was Ethiopia na kwengineko hadi pale watakapouliza chanzo cha machafuko Ethiopia ni nini; in serikali ya majimbo au chanzonini.

Kwa ufupi historia ya machafuko ethiopia ilianza kabla ya serikali za majimbo. Na chanzo cha serikali ya majimbo ni pale serikali zilizopita kutokuwa na uwiano sawa wa madaraka kati ya jamii zinazounda taifa LA Ethiopia. Ni kama hapa tz uone labda wakatoliki au waasia ndio wameshika 90% ya nafasi zote za kufanya maamuzi na teuzi. Ktk hali kama hiyo ndipo serikali mpya ikaamua kuundwa kwa serikali ya majimbo. Mgogo uliopo sasa unatokana na kabila hili lililoshika 90% ya madaraka kuona kuwa wao ndio wanaostahili kuendelea kushika madaraka na hivyo wanataka kurejeshwa ktk nafasi hizo au jimbo lao lijitenge.

Hali kama hii yaweza kutokea nchi yyt kwani wenye kuanzisha machafuko ni wale wanaonyamg'anywa tonge (ccm) na kuhiona hawastahili kunyang'anywa
 
Sentensi yako ya mwisho inalihukumu bara la Afrika kuwa nyonge daima. Kuwa bara la wajinga (ignorants) wasiokuwa na weledi wa kisiasa (lacking political savvy). Kihivyo, hakuna namna Waafrika wanaweza kuwa na jeuri ya kutembea kifua mbele, kujitegemea na kushindana kwenye soko la kimataifa.

Halafu ni kupotosha kufikiri viongozi wa majimbo wanakuwa na madaraka yote juu ya taasisi na vyombo vyote vya dola. Mfano hapa Tanzania. Rais wa Zanzibar SI amiri mkuu wa majeshi na si mkuu wa Mambo ya Nje wala ya Ndani. Mamlaka hayo ni ya Rais wa JMT pekee.

Utawala wa Ethiopia ya leo unaundwa na vikundi vya wapigania uhuru wa majimbo ya kikabila yaliyokuwa mwanzoni chini ya utawala wa kifalme na baadaye chini ya utawala wa kidikteta/kikomunisti na mwishowe Federation.

Tatizo lao kuu si majimbo bali ni kuendelea kuwepo kwa vikundi vya kijeshi chini ya miamvuli ya vyama vya siasa vya kikabila vinavyotawala majimbo. Ethiopia huwezi kuwa na chama cha siasa ambacho sio cha kikabila. Na wako tayari kwa mapambano hata kumwaga damu wakihisi wanaonewa.

Tanzania hatuna vikundi vya kijeshi vya kikabila. Vyama vya siasa si vya kikabila. Rais wa JMT ndiye mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama. Watanzania wameshachanganyika sana kijamii, kisiasa na kijiografia. Hakuna namna mgawanyiko kama wa Ethiopia unaweza kutokea.
siokweli kua hakuna vikundi viovu isipokua vinadhibitiwa na mfumo bora uliopo.
kuna system ambayo inajidhibit na kupata taarifa kwa urahisi kutoka ngazi ya mwenyekit wa kitongoji,kijiji,kata, wilaya,mkoa hadi taifa.
kwenye mifumo ya majimbo ni ngumu sana kudhibiti hivi vikundi.
lakin pia wakitokea viongozi wenye tamaa ni lahisi huyumbishwa.

labda nikupe mfano mdogo tu..!

chadema mlisema mkishika madalaka mtaanza na majimbo ma 5 hadib10 tu kwa tanzania nzima.

unafikili uaweza kudhibiti baadhi ya hali za kiusala?

kwa ufupi jalibu kuchunguza.afrilika nzima nchi zote zenye migogoro ya aina hii ipo kwenye mifumo ya majimbo. wewe bado hutaki kujifunza tu?

kabla ya kuingia kwenye mifumo hii kwa africa .kwanza wajifunze,wakubali kuelewa,kuijua democlasia ,na viongozi wajue haki za wanaowaongoza.

kama leo mboe anahamasisha kudai katiba mpya ,viongozi waliopo madalakani wanamziba mdomo kwa kupewa kesi kubwa bila ya aibu. unafikilia nini juu ya afrika na tanzania yako mkuu.

waafrika bado wana usokwe ndani yetu. capacit brain bado ipo chini sana.
kunavitu hatutakiwi kuvikulupukia.
 
Nimekuwekea takwimu....

Kati ya nchi 48 za Asia ni 5 tu zenye Sera za MAJIMBO.....

Kwa maneno yako hizo nchi 43 zisizo na mfumo huo "uupendao" zinasambaratika ama zingeshasambaratika.......

Kati ya nchi huru 54 za Afrika ni nchi 5 tu zenye Sera za majimbo.....

Kwa maneno yako nchi 49 zisizo na mfumo wa majimbo zinasambaratika ama zingeshasambaratika......

Kati ya nchi 12 za Amerika ya kusini ni 4 tu zenye Sera ya majimbo(Brazil ,Venezuela,Mexico na Argentina)....kote huko Kuna vikundi vya silaha vinavyotaka kujitenga(Ven-Zulia) (Arg-Patagonia) Brazil- Sao Paulo....Mexico imebaki "ngada"🤣🤣🤣

Hiyo mifano ya ubora wa Sera ya majimbo mnaitoa ULAYA NA MAREKANI?!!!!!

Marekani na Ulaya hatufanani nao kwa mengi tu na sidhani ni rejea yenye mantiki....

Huko juu nimeandika kwa kirefu kumjibu compatriot wako......

✓Ethiopia hali ni tete....ni marudio tu......
✓DRC ndio kabisaaa.....nchi imejikita tu kule Kinshasa na majimbo ya karibu....huko Mashariki serikali ya shirikisho haina udhibiti makini.......Katanga ilitaka kujichomoa mapema kabisa......

✓Nigeria ni sugu.....majimbo ya kaskazini yanajulikana kwa kukosa utulivu.......
Kule BIAFRA toka enzi ni fukuto tu hadi leo hii....nia Yao iko palepale ya kuiondoka NIGERIA

Nimekupa mifano ya nchi 3 tu za barani Afrika zenye "nakama" ya majimbo halafu bado unashupaza shingo tu 🤣🤣

SIEMPRE JMT
Wa
Yaani ikitokea marais 3 wanakufa ndani ya kipindi kimoja cha utawala basi nchi iingie gharama za uchaguzi mara 3 Khaaa 😳🤣🤣
Wazo la kijinga. Katiba mbovu ndiyo imepelekea mtu ambaye hakuwahi hata kuwaza kuwa rais sasa ndiye Rais. Yaani hata hajawahi kuwa hata waziri wa serikali ya muungano leo anaendesha nchi. Anajua nini zaidi ya kushikwa akili.!?
 
It's not nonsense, you are just too delusional.
Uta-argue vipi kuhusu majimbo bila kuhusisha geographic location?
Na uta-argue vipi kuhusu wars bila kuhusisha resources?
Resources ndiyo zina-create boundaries between a group of people especially when they don't want to share.
Majimbo yanawapa nguvu makundi ya watu waliogawanyika kutokana na resources (resources are a function of a geographic location).
Wenyeji??? What the f#ck is wenyeji?? At what part of the human timeline utasema hawa ni wenyeji???

Unabisha vitu obvious just because you wana be affiliated with a bogus policy that failed miserably at the ballot box. Stop affilliating your facts with a group of failed politicians.
You must be a fool to believe that policy failed at the ballot box.
 
Nilikuuliza swali kama hili wakati Fulani. Why Zambia inaweza kupita ktk hali ya kisiasa kama hiyo? Nikafatilia kidogo nikagundua kwao ni kawaida hata Keneth Kaunda aliondoka madarakani akaenda jela. So walipitia kipindi cha kuwafanya waone aliyepo na atakayekuja kuna utifauti fulani. Hivyo siyo kwa sababu ya uwepo au kutokuwepo kwa majimbo.
Hayati Kaunda aliweka precedent kama ambavyo hayati Jerry Rawlings wa Ghana na yule wa Malawi Kamuzu, kitu ambacho hayati Nyerere alikataa kufanya kule Zanzibar. Kaunda angekataa kuachia madaraka angeweza , Jerry pia angeweza kule Ghana kuhakikisha mgombea wa chama chake anatangazwa. Nyerere alikataa hilo lisitokee Zanzibar 1995, kwa hiyo kinachotokea Zanzibar leo ni zao la dhambi ile. Je, kama kipande kile kidogo cha Zanzibar wako tayari kuua watu ili wasikiachie, watakuwa tayari kuliachia pande kubwa la Bara!? Jibu ni hapana.
Huko kwingine wazee wa TaifA walishaonesha mfano kuwa kuachia madaraka ni jambo sahihi unaposhindwa uchaguzi.
 
Jifunze Kiswahili sahihi

Una tatizo la "r" unaweka "l"

Rekebisha hilo tatizo ni very annoying na litakunyima usipewe seriousness kwenye maandiko yako ya kazini na ya ki-professional

Huwezi andika report ya design au analysis kwa wateja au employer au wakubwa zako kwa lugha ya hovyo hivi hujui wapi inakaa R na L

Very poor na inaonesha una ubongo na umakini mbovu sana wa matumizi ya lugha...

Hovyo kabisa..fanyia kazi na usije hapa na utetezi wa kipumbavu...rekebisha that stupidity
hahahahahahahahahahahahahahahahah.............

nasikitika tu kua sina wakubwa. mimi mwenyewe mkulingwa mkuu.

lakini pia mimi sio mwandishi ,siku zote nasema.

ila sawa nitajitahidi kutafuta mwalimu wa uandishi mkuu.
 
Tigray ni kasehemu kadogo ila chenye watu wenye ushirikianao mkubwa sana na wanaojivunia historia yao. TPLF ya Tigray ndio iliyopinga utawala wa Derg wa dikteta Mengistu Haile Mariam tangu mwanzo na Watigrinya ndio waliokuwa Kiongozi wa kuwaunganisha na kuyaongoza makabila mengine makubwa kumuondoa Mengistu mwaka 1991.

Ukienda Rwanda utakuta Watusi ndio wachache ila ndio wamehodhi madaraka yote makubwa ya nchi hiyo kabla na baada ya ukoloni.

Makaburu walikuwa chini ya asilimia 10 ya watu wote wa Africa Kusini ila waliweza kulitawala taifa la watu weusi kwa zaidi ya nusu karne.

China wanachama wa Chama cha kikomonisti ni milioni 95 tu ila wameweza kuwatiisha raia bilioni 1.4

Power juu watu wengine ni suala la "organization na cooperation" na wala sio suala la wingi.

Abiy Ahmed alikuwa "naive" kufikiri angeweza kuwapoka Watigrinya kirahisi na kwa muda mfupi nguvu na fursa walizokuwa nazo muda mrefu bila kuleta mtafaruku mkubwa. Ilihitajika mkakati smart na wa muda mrefu wa kisiasa kufanya hivyo, bahati mbaya Abiy Ahmed ni mtu "smart" sana ila sio katika uwanja wa siasa na historia "complicated" ya Ethiopia, kwa kifupi alifanya mambo mengi kwa kukurupuka bila kujipanga.
Mkuu, nimekusoma nikiwa ninaielewa mada yako hadi nilipofika kwenye mistari hii:
"Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti..."

Hilo nadhani hukuliwaza kwa kina, kwa sababu utulivu unaousema wewe, kiuhakika siyo utulivyo hasa! Sitalielezea hili, lakini nina hakika hata wewe unaweza ukawa unajiuliza kama tulichonacho sasa ni utulivu kweli au la! Kukosekana kwa vurugu, huku wanaochochea pawepo na vurugu ni watu walewale wanaotakiwa kulinda hali ya usalama wa nchi yetu, sioni kwamba hilo ni jambo la kujivunia hasa.

Hata hivyo, ninakubaliana nawe kwenye jambo la mikoa na/au shirikisho. Mfumo wetu kama ulivyoanzishwa ulitusaidia sana kuanza kuondokana na matatizo yanayowakabili nchi mbalimbali, hasa Afrika, kama hiyo Ethiopia, Nigeria..., Kenya wao wanadhani kuwa na mikoa ya kikabila kunawasaidia, lakini sidhani kuwa ni hivyo.

Nikiachana na kuandika gazeti humu, jambo ninaloliona juu ya mfano wa Ethiopia, na ambalo pengine linaweza kuwa fundisho kwetu ni hili ambalo sikulitegemea kabisa, la jeshi la nchi hiyo kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na waasi hawa. Tigray ni kasehemu kadogo sana ka nchi hiyo, pamoja na kwamba ndiko kalikuwa kanashikilia utawala wa nchi hiyo kwa miaka kadhaa iliyopita. Haka kasehemu pamoja na udogo wake kameweza kuwayumbisha sana Ethiopia kama nchi.

Je, na sisi tuwe tayari, KiZanzibar ketu kakicharuka? Au mbaya zaidi: Kanchi kadogo jirani nasi (sitaki kukataja) katakapokuwa tayari kututoa kamasi hatutakuwa na njia ya kujitetea?
Najua sifa zetu mara nyingi tunazo midomoni. Ethiopia pia walidhani wapo imara sana.

Sibezi chochote, lakini hii ni tahadhari tu!
 
Haya kwa majirani zetu, hiko kipindi cha miezi 3 cha kusubiri na kuandaa uchaguzi mkuu unafikiri nchi itakuwaje? Unafikiri huyo makamu aliyeshika nchi kwenye kipindi hicho ataachia nchi kirahisi rahisi
Unaijua mahakama ya Kenya?? Wamezuia hadi BBI ambayo ndio ilikua succession management ya Kenyatta na Odinga most powerful men in Kenya ila wameangushwa.

Chaguzi ya 2017 Ilifutwa na Rais alikua madarakani ndio sembuse makamu??

Hapa Afrika mashariki lazma tukubali kwenye suala la katiba na uhuru wa mihimili, Kenya haina mfano!!
Inashangaza mtu kama CAG kusema hawezi kuondolewa madarakani na mkuu wa nchi. Yaani CAG naye anajiona kapata madaraka hayo moja kwa moja kupitia umma (the people) kwa uchaguzi
Yes kama unafahamu utawala bora the uwajibikaji na uhuru wa vyombo vya umma ni muhimu. Mfano Rais akiwa na uwezo wa kumtumbua anayemkagua kuna uhuru hapo? Hvi bajeti ya CAG ikipangwa na wizara kuna uhuru hapo? Lakini kenya kuanzia DPP,CAG,Korti,Bunge,DCI,ni independent entities na hawaingiliwi na yeyote. Bongo DPP amewahi pingana na Rais? Au Bunge limewahi pinga bajeti ya serikali au teuzi ya Rais??

Nitajie kitu kimoja tu ambacho katiba ya TZ is better than Kenya kwenye uwajibikaji na uhuru wa vyombo?
 
Tigray ni kasehemu kadogo ila chenye watu wenye ushirikianao mkubwa sana na wanaojivunia historia yao. TPLF ya Tigray ndio iliyopinga utawala wa Derg wa dikteta Mengistu Haile Mariam tangu mwanzo na Watigrinya ndio waliokuwa Kiongozi wa kuwaunganisha na kuyaongoza makabila mengine makubwa kumuondoa Mengistu mwaka 1991.

Ukienda Rwanda utakuta Watusi ndio wachache ila ndio wamehodhi madaraka yote makubwa ya nchi hiyo kabla na baada ya ukoloni.

Makaburu walikuwa chini ya asilimia 10 ya watu wote wa Africa Kusini ila waliweza kulitawala taifa la watu weusi kwa zaidi ya nusu karne.

China wanachama wa Chama cha kikomonisti ni milioni 95 tu ila wameweza kuwatiisha raia bilioni 1.4

Power juu watu wengine ni suala la "organization na cooperation" na wala sio suala la wingi.

Abiy Ahmed alikuwa "naive" kufikiri angeweza kuwapoka Watigrinya kirahisi na kwa muda mfupi nguvu na fursa walizokuwa nazo muda mrefu bila kuleta mtafaruku mkubwa. Ilihitajika mkakati smart na wa muda mrefu wa kisiasa kufanya hivyo, bahati mbaya Abiy Ahmed ni mtu "smart" sana ila sio katika uwanja wa siasa na historia "complicated" ya Ethiopia, kwa kifupi alifanya mambo mengi kwa kukurupuka bila kujipanga.
Sehemu kubwa ya andiko lako; hasa hiyo ya "organization and cooperation" ninakubaliana na wewe; ila unapokuja kwenye hiyo mifano mbalimbali uliyotoa kunakuwa na tofauti, yote haiwezi kushabihiana; hasa inapokuja kwenye kuwakandamiza watu wengine, utility ya umoja na mshikamano huo unakuwa na walakini, kwani una ukomo wake.
Kumbuka, umoja na mshikamano siyo 'exclusive', wengine pia wanaweza kuukwaa na kuutumia dhidi ya hao wanaowakandamiza, kama hiyo issue ya Makaburu.

Katika swala la Ethiopia yenyewe, hata hao Tigray wakati wao ulikuwa umepita kama ilivyokuwa tayari imejionyesha kwa matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea hasa sehemu za Oromo. Kwa hiyo huwezi kumlaum Abiy katika hilo, ilikuwa tayari muda wake umewadia.

Ninakubaliana nawe Abiy ni 'smart', na ninamatumaini hili ni swala la muda, litarekebishika. Watu waliozoea kutawala wengine sio rahisi kukubali kujishusha kuwa sawa na wengine waliokuwa wanatawaliwa.
 
Habari wanajamvi,

Kama ilivyo kawaida, kufanya tafakuri ya mambo yale mtu anayoyasikia maredioni na magazetini kuhusu yanayoendelea kwenye siasa za nchi mbalimbali.

basi nami nimejikuta nikiyatafakari sana yale yanayoendelea huko Ethiopia na vita vyao vya serikali ya kitaifa na wanamgambo wa jimbo lao la tigrinya, ambapo sasa vita hivyo vimeonekana kuvuta na makundi mengine ya makabila toka majimbo tofauti na tigrinya, tena mbaya zaidi makundi hayo yameanza na kutaka kudai uhuru.

Sasa, nikakumbuka mfumo wao wa uongozi wa Ethiopia wa kutumia majimbo, na kukumbuka jinsi baadhi ya watanzania huwa wanausema mfumo wetu wa mikoa ambao mkuu wa mkoa anateuliwa na rais hivyo kufanya serikali kuu kuwa na mkono wa moja kwa moja kwenye kuongoza mkoa, ambapo ni tofauti na mfumo wa majimbo ambapo kiongozi wa mkoa anapigiwa kura

Ubaya wa majimbo ni kuwa viongozi hao wa majimbo wana kuwa na mamlaka makubwa hata yanawajaa vichwani mara nyingine na kuwa fanya kutaka kuwa juu ya serikali ya kitaifa

Mfano serikali ya jimbo la tigrinya ambalo viongozi wake ndio vinara wa kisapoti waasi wapiganao dhidi ya serikali kuu. Mbaya zaidi mfumo huo wa majimbo unatoa mamlaka ya majimbo kuunda majeshi yao, ndio yanaibuka hayo ya makundi ya kiti gray, ambayo kiukweli ni jeshi la ndani la jimbo la Tigrinya

Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti, hivi, hata siuoni mwanya wa mkoa fulani kutuletea vurugu za kujitenga ama kuanzisha mapigano ndivyo ninazidi kuu appreciate mfumo wetu wa mikoa tulio nao

Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake.

Viongozi waasisi wa taifa letu walikuwa na ujiniasi wa kipekee kabisa maana taifa hili walilolisuka baada ya kulipokea toka kwa wakoloni wamelisuka vizuri sana, ulimbukeni wa kukaa na kuona mifumo ya siasa ya wezetu ni bora zaidi ya kwetu tukiuendekeza utafanya siku moja tufumuefumue taifa hili lililosukwa vyema.
Get to know a history of a country before getting into such a cacophonous writing

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
kichocheo kiaje?

Elezea hiyo process jimbo linaanza mgogoro na mtu

Shida ni pale local people are abused by the federal government bila haki ndio shida
Sikusikii ukizungumzia "shida ya local people used to abuse other communities when power was on their side"!

"Kichocheo kiaje"? - wakati kundi la watu katika eneo moja wanapojitambua kuwa wao wanahaki zaidi ya wengine, au sifa ya kipekee wanayojiona kuwa nayo wanayodhani inawafanya wawe zaidi ya wengine wasiokuwa eneo lao, hicho kinaweza kuwa kichocheo muhimu ya kuleta vurugu ndani ya nchi.
 
Back
Top Bottom