Mgogoro wa Kariakoo unashinikizwa zaidi na wafanyabiashara wakubwa

Mgogoro wa Kariakoo unashinikizwa zaidi na wafanyabiashara wakubwa

Jbst

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2020
Posts
1,971
Reaction score
4,085
Nilichogundua kuhusu Kariakoo sio kila mfanyabiashara hapo anagoma.

Wafanyabiashara wakubwa wanaoshusha kontena bandarini ndo wanamiliki mastoo hapo Kariakoo na hawa ndo waasisi wa mgomo wenyewe kwasababu hawataki stoo zao zitambulike.

Ukiwasikiliza wengi wanaogopa kufungua kwasababu wanafanyiwa fujo, jana kuna watu walikua wanazunguka kuangalia aliyefungua na wakikuta umefungua wanakutisha kubeba hata mali yako kwahyo hawa wenye maduka wengi wanashinikizwa na wakubwa.

Nilikuwepo hapo nimeona, watu walianza kufungua maduka saa 4 asubui kuna watu wakawa wanakuja kuwatisha wafunge.

Maoni yangu sio kwamba nakubaliana na TRA wanachokifanya ila nimesema kile kinachoendelea hapo Kariakoo.
 
Migomo ya hivi,

Ukijifanya kichwa ngumu unapotezwa kwny game.

Maana bidhaa nyng hapa k'koo karibu kila sekta madon wake wakubwa hawazidi 5, hao wanaheshimika sana, Wana influence kubw kwny mzunguko, serikali na chama.

Hao wakiungana, wanaamua Jambo lao kwa mustakabali mzima wa k'koo yote na sisi wauzaji wadogo wa chini tuuzeje na tupate faida kias gani.

Ukikaza fuvu lako, ukajifanya mzalendo uchwara, Unatengwa na kufanyiwa figisu kibao ili upotee kbs kwny biashara.

Hebu Ni nambie,
Ni Nani mwny guts za kukaza fuvu ili wanae wasiende chooni? Jibu Ni HAYUPO.

TUNAKOMAA WOTE HADI KIELEWEKE[emoji106]
 
Na hao wafanyabiashara wakubwa miongoni mwao ndio wabunge, mawaziri, na vigogo wengine serikalini.

Ajabu zaidi, unakuta hao wabunge wafanyabiashara wa CCM ndio walipitisha hizo sheria kandamizi kule bungeni, wakidhani zingewaumiza wapinzani peke yao wasijue extent ya ujinga wao.

Halafu hizo sheria zikija kwenye utekelezaji, wao wanawashawishi wafanyabiashara wadogo wagome, wakati huo wao wapo bungeni wanamuuliza Spika nini kinaendelea kule Kariakoo, huku PM akiwa amezungukwa na kundi kubwa la wafanyabiashara wadogo akiongea nao.
 
We mwalimu lia lia tulia uusiingilie mambo yasio kuhusu kwahyo kama na mzigo store natakiwa kulipia mizigo ya store na pia mteja akija dukani alipie kodi na akitoka apo akamatwe aombwe rushwa si ndio unaona sawa .... ebu tuachie sigara subili laki sita zako mwisho wa mwezi ulale [emoji35][emoji35]
 
Ukiniuliza mimi nasema ni shinikizo la wanaharakati wanaotafuta mitaji ya Ajenda zao.

Ukifuatilia vizuri, utasikia na kuona ni jinsi gani Viongozi na hata Wanaharakati wa CHADEMA jinsi walivyoteka suala hili na kulifanya la Kisiasa.

Kwa maoni yangu, ni suala la Kisiasa zaidi kuliko Biashara.
 
Nilichogundua kuhusu kkoo sio kila mfanyabiashara hapo kkoo anagoma.

wafanya biashara wakubwa wanaoshusha kontena bandarini ndo wanamiliki mastoo hapo kkoo na hawa ndo waasisi wa mgomo wenyewe kwasababu hawataki stoo zao zitambulike...
Hatufungui bhnaa, hakuna cha nini wala nini, miaka yote tushawashauri TRA hawasikii
 
Nilichogundua kuhusu kkoo sio kila mfanyabiashara hapo kkoo anagoma.

wafanya biashara wakubwa wanaoshusha kontena bandarini ndo wanamiliki mastoo hapo kkoo na hawa ndo waasisi wa mgomo wenyewe kwasababu hawataki stoo zao zitambulike...
Sababu ya bandarini na stoo ndio vipi sababu yq wafanyabiashara wa nje na wengine kuwa harrased? Hio inamhusu mfanyabiashara mdogo kuliko mkubwa.
 
Migomo ya hivi,
Ukijifanya kichwa ngumu unapotezwa kwny game.

Maana bidhaa nyng hapa k'koo karibu kila sekta madon wake wakubwa hawazidi 5, hao wanaheshimika sana, Wana influence kubw kwny mzunguko, serikali na chama...
Yeap kuna mapapa hapo ukienda against unapotezwa kabisa na familia itakula msoto..
 
Asilimia zaidi ya 90 ya wafanyabiashara wa hapo Kariakoo hawafati mizigo yao China

Wengi wananunua hapo hapo kwenye maduka ya Jumla, sasa hao baadhi wakiamua kukaza hakuna atakayetoboa , maana changamoto ya kuagiza mzigo ambao unakuja baada ya miezi miwili or mitatu ni wafanyabiashara wakubwa wanaweza ku-mantain huo mzunguko na bado kuleta supply ya kutosha

Hivyo mmoja akiamua wengine wataumia tu, lakini pia pamoja na hayo hawa wafanyabiashara wadogo wamekuwa wakikumbwa na madhila ikiwemo kukamatwa na wanausalama na watu wa forodha na kupigwa faini jambo ambalo limekuwa likiwaumiza sana
 
Wewe endelea kupokea mshahara wako wa tgsb achana na wafanyabiashara, mimi nipo kkoo kwa zaidi ya 10yrs nishapitia mengi hata usiyowahi kuyafikiria kuwa yanatokea kkoo.

Wewe jifanye mjuaji watu wakufurahishe, kwa taarifa yako biashara zote duniani zinaongozwa na cartels na huwezi fanya lolote.
 
Wewe endelea kupokea mshahara wako wa tgsb achana na wafanyabiashara, mimi nipo kkoo kwa zaidi ya 10yrs nishapitia mengi hata usiyowahi kuyafikiria kuwa yanatokea kkoo, ww jifanye mjuaji watu wakufurahishe, kwa taarifa yako biashara zote duniani zinaongozwa na cartels na huwezi fanya lolote.
Wanaotetea udhalimu huu wa TRA nna uhakika hawajawahi fanya biashara nchi hii, Kama ndio Basi wanaleta siasa kwny biashara za watu
 
Nilichogundua kuhusu Kariakoo sio kila mfanyabiashara hapo anagoma.

Wafanyabiashara wakubwa wanaoshusha kontena bandarini ndo wanamiliki mastoo hapo Kariakoo na hawa ndo waasisi wa mgomo wenyewe kwasababu hawataki stoo zao zitambulike...
 
Naomba kujuzwa tu huu mgomo una faida Gani kwa wafanya biashara?

Maana Kodi washakadiriwa na Bei za pango wanalipa kama kawaida?
 
Nilichogundua kuhusu Kariakoo sio kila mfanyabiashara hapo anagoma.

Wafanyabiashara wakubwa wanaoshusha kontena bandarini ndo wanamiliki mastoo hapo Kariakoo na hawa ndo waasisi wa mgomo wenyewe kwasababu hawataki stoo zao zitambulike...
Kwanini wafungue saa 4 si wangefungua mapema kama kawaida
 
Back
Top Bottom