Afadhali hilo jengo wamechukua CRDB kwa maana lilianza kuwa gofu,CRDB wamefanya ukarabati wa nguvu na anagalau sasa sisi tulio na vijisenti vyetu tuna sehemu salama ya kuweka na kuchulia hela kwa maana kale kanyumba ilimokuwa benki ya CRDB ilikuwa aibu utadhani sebule ya grocery na hata pa kupumulia palikuwa hakuna na bahati mbaya ndio iwe siku ya mgao wa wakulima wa chai inabidi mkae nje na kupanga foleni, pale yalipokuwa makao makuu ya kanisa ambapo wapo CRDB waumini walipageuza kama kijiwe cha majungu, ni kama palikuwa jobless corner.Askofu alifanya uamuzi mzuri kuhamishia makao makuu mjini Mbeya, waumini wa wilaya ya Rungwe wana nongwa sana hata mgogoro wa kanisa la Moravian uliofanya kule Kyela wajitenge ni sababu ya hawa hawa waumini wa Rungwe, Wanyaky wa Rungwe ni wabinafsi sana utadhani ni kama wale wa kutoka kwa mwenyekiti wa SACCOSS ya Kishmundu.