Mgogoro wa Ukraine na Urusi unapima akili za Waafrika


Kavulata:

Umenifungua macho kuhusu Mwafrica..... " Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinachochewa na nchi zenye viwanda vya silaha" Sasa huyu mwafrica yeye ni zezeta kukubali kuchochewa na mzungu! Miaka 60 toka ajipatie uhuru wake ameshindwa kabisa kujitambua na kuwa na fikra zake....! Kushindwa kutatua matatizo yake ya ndani na kuruhusu mtu toka nje kuja na kuzidi kuwagonganisha vichwa!

" Silaha zinaingizwa kwa njia mbali mbali " Kweli akili ya Mwafica ina matatizo! Ina maana nchi za Kiafrica hazina Immigration unit (Idara za Uhamiaji) Hazina watu wa Customs! Miaka mingi toka tujipatie Uhuru tunashindwa kulinda mipaka yetu! Ni nani wa kumlaumu hasa! Maana hata kuendesha bandari tu inaonekana shida hapa kwetu Tanzania! Yaani kupokea mizigo na kusafirisha tunahitaji usaidizi! Kweli tutafika! Ni nani wa kumlaumu!

Asante kwa kunifungua macho kuhusu akili ya Mwafrica, uko sawa kabisa, na Mzungu hata kututupia ndizi kama ulivyosema ametuhurumia sana! Maana kisha jua akili zetu!
 
Chanzo kikuu Cha matatizo yetu ni ukosefu wa nguvu dhidi ya Wazungu. Hatuna nguvu za kiuchumi, nguvu za kijeshi, nguvu za kujilisha na nguvu za kujivisha wenyewe. Mtu au hata taifa lolote duniani litakalokosa mojawapo kati ya nguvu hizi atalazimika ku conform/kubaliana na upande wenye nguvu hizi. Ujeruman hii Vita ya Ukraine Haina maslahi nayo lakini analazimika ku conform kwakuwa Hana nguvu kubwa za kijeshi dhidi ya Urusi, North Korea na uchina (eastern), hivyo analazimika kuandamana na Marekani hata kama haipendi.

Umaskini wa Afrika umepangwa, sio wa bahati mbaya. Westerns wanaendelea na uhusiano wa kikoloni na makoloni yake kwaajili ya kuendelea kupata rasilimali, cheap Labor and markets. Mbinu wanazozitumia ni kuwatupia ndizi( misaada na mikopo hafifu sana) waafrika, kuchochea vita, mikataba mibovu kama ileile ya akina Karl Peters, kuwa na vyombo vya habari vya propaganda kama BBC, Dw, France internal kwa lugha zetu, na hata kuua mbegu zeu za asili.
 
Kuilazimisha nchi iliyoko huru na kuichagulia iwe upande gani katika huu mgogoro pia ni zaidi ya ukoloni mambo leo.
Wazungu wa magharibi n marekani ni watu hatari sana, mtu mwenye akili kamili hawezi kufurahia mawazo na vitendo vyao hata kidogo labda kwa mtu mwenye uhafifu kidogo. Nchi za Western zinahakikisha kuwa nchi nyingine zinakuwa tegemezi kwao milele. Wanafanya hivyo kwa kuhakikisha kuwa nchi za kiafrika na nyinginezo haziwi na viwanda mama na technologia na uwezo wa kuzitawala rasilimali zao kama madini, mafuta na mazao ya mashambani. Watahakikisha kuwa madini, gesi na mafuta yanaangukia mikononi mwao kwa gharama yoyote ile. Hakuna nchi ya western hata moja itatoa msaada wa kujenga viwanda Afrika. Misaada yao kwa nchi za Afrika ni kama ile ya kutoa njia za uzazi wa mpango, kutunza misitu, na kuhifadhi wanyamapori tu. Nchi yoyote ambayo itagundua hifadhi kubwa ya madini, mafuta au gesi watahakikisha kuwa rasilimali hizo hazitumiki kupata fedha nyingi ya kujenga viwanda vikubwa, kununua technolojia na kuwapa elimu ya maana watoto wetu. Ukiona kiwanda kikubwa Afrika na Asia basi huo ni uwekezaji kutoka western. Sasa hivi wanahakikisha kuwa nguvukazi yetu inahamishwa kwenda nchi za western kuwatumikia wao na kuziancha nchi zinazoendelea na vibarua wa hovyohovyo tu kwa kigezo cha greener pastures.

Ni mwehu tu ndie ambae hajui jamaa wanatufanya na kutufanyia nini. Huu ni muda wanyonge kujikusanya nyuma ya Urusi na China angalau kurekebisha mizania itufae sote.
 

Kavulata:

Hivi kama umaskini wa Africa umepangwa na si bahati mbaya, kwa nini tunashindwa kuupangua? Miaka na miaka, tuna miaka mingi toka tupate uhuru! Huu udumavu wa akili utakwisha lini hasa?
 
Kavulata:

Hivi kama umaskini wa Africa umepangwa na si bahati mbaya, kwa nini tunashindwa kuupangua? Miaka na miaka, tuna miaka mingi toka tupate uhuru! Huu udumavu wa akili utakwisha lini hasa?
Hebu wape shule wangeweza kuupangua kwa njia gani? Maana viongozi wenye dhamira ya kuupangua umaskini wote ama wataondolewa kwa kura, vurugu za "wenyewe kwa wenyewe" au kuwaua. Nchi zote zenye mafuta na madini (Nigeria, Angola, Sudans, Lybia, Iraq, Iran, Syria, Saudia, DR Congo, Tanzania, Afrika ya kati, mali, Urusi, etc) ama kuna vita, ama viongozi wameuawa, ama kuna mikataba ya kinyonyaji, na Hakuna free markets at all. Sasa hivi wanakwenda mbali hata zile mbegu zetu za asili zinapotezwa ili watu walazimike kwenda kununua mbegu kwao utake usitake. Kule Uganda wamegundua mafuta Wazungu wamekasirika, kule rufiji Tanzania ilikatazwa na Wazungu isijenge bwawa kubwa la umeme litakalomaloza shida ya umeme, kule Ethiopia walikatazwa kujenga bwawa,nk. Kuna watanzania wenzetu ambao ni vibaraka wao ambao wananunuliwa na Wazungu kufanya kazi za Wazungu ndani ya mataifa yetu, tunafahamu hili.
 
Ngoja nikune mbupu nilale , na umeme wamekata sijui mbezi juu tu au kote[emoji1787][emoji1787]
 
Siyo kweli...
SoMo la kujitambua na kutafakari kwa kina lazima lifundishwe tangu elimu ya awali, hali yetu ni mbaya sana. Kule kwa wenzetu mtoto wa darasa la kwanza ukimpa pipi atakuuliza "why me?" kwanini unipe Mimi na kwanini unanipa? unataka nini kwangu?. Huku kwetu hata mtoto wa university ukimnunulia chips kuku atafakamia TU.

Tumechelewa sana, inatubidi tukimbie sana kufika tulikotakiwa kuwa. Tumecheleweshwa na kufikiria na kutenda kigoigoi, undugu, ukabila, ukanda, udini, na uccm na upinzani kwenye mipango yetu.
 
Shida hapa ni aina ya elimu uliyonayo

Kavula,

Hiyo System ya kuwa na hao Judges ni wenyewe! Sisi tulikuwa tunakaa chini ya mti, chini ya Chifu kuamua kesi zetu! S dini, elimu na mfumo wa maendeleo tuyayoyaita maendeleo umetoka kwao, hilo la kuvaa wigi halishangazi! Namshangaa sana Lumumba! Je lugha anayotumia kufikisha ujumbe wake anatumia lugha gani! Mbona hajavaa magome ya miti!

Nilikwambia huko nyuma, toka babu yako na babu yangu waliposhindwa kumzuia Mzungu/Mwarabu au mtu mweupe kwa ujumla asishuke pwani zetu miaka 1800, tayari mtu mweupe aliisha tuteka! Ndio maana mpaka leo wengine wanadhani matatizo yetu yataisha akija sijui Mrusi, Mchina hawajui ni kitu kile kile!
 
Sehemu ya ukweli ni hii hapa
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu lazima awe na upande anaouunga mkono kwasababu zake mwenyewe, kikundi chake au taasisi yake dhidi ya mtu mwingine, kikundi au taasisi nyingine kwenye jambo, tukio au tabia Fulani. Kila mtu lazima awe sehemu ya tatizo au suluhu kwenye changamoto za mtu, kikundi au taasisi. Hakuna kuwa kati (neutral) labda TU wenye mtindio wa ubungo, woga na wanafiki/ndumilakuwili.
 
Kuwa na akili timamu ni kuwa upande wowote ! Uko Right...Kuwa Upande wa Hitler...Pol Pot... Iddi Amin.....Mobutu Sesseko..Jean Bedel Bokassa....Charles Taylor....Paul Biya....General Sani Abacha.....Macias Nguema....Bennito Mussolini...Wote Hao walikua upande wa kutatua Matatizo kwa mitazamo yao!

Hata Taasisi kama Al quaeda, Al Shabab...Boko Haram....Baader Menhof...Red Brigade...Na vingine vingi....Vikundi hivi vyote vinajiona ni suluhisho la kutatua tatizo fulani!

Unaposema kila mtu awe ni sehemu ya kutatua tatizo naona unajichanganya sana Kavulata! Njia yako ya kutatua tatizo si lazima iwe njia yangu au ya mwingine!

Wengine wanaona kutatua matatizo ya jamii ni kufuata Itikadi ya Uislamu....Wengine Ukristo...Wengine ni Ujamaa...Wengine Ubepari....Wengine Social Democracy....Wengine African Socialism....the list is endless......
 
Kuwa upande mmojawapo wa changamoto ni akili kubwa. Ndio maana Kuna watu wanaiywa ma pro.... na ma anti-..... lazima uwe ama unaunga mkono hoja au huungi mkono hoja, nothing more nothing less,
 
akili ni bora kuliko mali
 
Akili za kuambiwa changanya na zako

 
Hawa ni raia wenye akili nyingi kama za binadamu kamili. If you don't do it yourself who will do it?
 
Mwenyewe unaona umewaza kwelikweli kumbe ni mikamasi tupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…