Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

kweli kabisa wasiwe watanzania ...maana sioni kwa nini serikali inakataza mgombeea binafsi...
 
Tatizo na mahakama zetu kwa kiasi bado zinaingiliwa na wanasiasa. sioni ni kwa nini hili suala limechukuwa muda mrefu hivi kuanza kusikilizwa. Anyway, ndio Tanzania yetu hiyo!
 
na hata hao majaji wakiamua wawepo wagombea binafsi, utaambiwa hilo haliwezekani kabla ya uchaguzi wa mwaka huu, maana mpaka kupenge likae libadili hivyo vipengele , then raisi aridhie hiyo sheria, halafu mawasiliano n ya wepo kwa tume ya uchaguzi.
 
na hata hao majaji wakiamua wawepo wagombea binafsi, utaambiwa hilo haliwezekani kabla ya uchaguzi wa mwaka huu, maana mpaka kupenge likae libadili hivyo vipengele , then raisi aridhie hiyo sheria, halafu mawasiliano n ya wepo kwa tume ya uchaguzi.

Katika nchi inayofuata sheria mgombea binafsi ikipitishwa halafu hizi biashara nyingine zikawa bado uchaguzi unasubiri a speedy process ya kukamilisha hilo. Kwa sababu ukifanya uchaguzi bila kuruhusu wagombea binafsi wakati sheria inawakubalia unatafuta matatizo mahakamani baada ya uchaguzi.
 
It is impossible and unconstitutional!

Nafikiri hiyo ni hyperbole ya kuonyesha watu walivyokosa imani na mahakama za Tanzania.

Mahakama za juu zinajitahidi sana, na sintoshangaa nikisikia mahakama imeipitisha hii na ku declare kuzuia private candidate kuwa unconstitutional.Mtikila ana kesi nzuri sana, pamoja na matata yake yote anafanya bonge la service kwa demokrasia Tanzania, he is individually doing much more than many opposition parties.
 
kama kuna uwezekano hao majaji wasiwe watanzania!!!

Ujinga wa kutojiamini kama Taifa. Kwani hao kina Manento ambao mwanzo walikubaliana na Mtikila walikuwa Wakenya?

Jengeni imani na taasisi zenu. Ndio maana wakenya wanawashughulikia kila siku kwa kutojiamini kwenu. Watanzania bana!
 
Ujinga wa kutojiamini kama Taifa. Kwani hao kina Manento ambao mwanzo walikubaliana na Mtikila walikuwa Wakenya?

Jengeni imani na taasisi zenu. Ndio maana wakenya wanawashughulikia kila siku kwa kutojiamini kwenu. Watanzania bana!
bila shaka utakuwa wakala wa mafisadi,! kwa taasisi zipi za kuwa na imani nazo? na serikali gani? unajaribu kulazimisha ng'ombe awe mbuzi....utadumaa na mawazo hata ya mafikirio yako tumejaribu uwazavyo, kwa ujumla taasisi za taifa la tanzania nimezipa talaka
 
Ujinga wa kutojiamini kama Taifa. Kwani hao kina Manento ambao mwanzo walikubaliana na Mtikila walikuwa Wakenya?

Jengeni imani na taasisi zenu. Ndio maana wakenya wanawashughulikia kila siku kwa kutojiamini kwenu. Watanzania bana!

Nafikiri wewe ndiye mjinga wa kutoelewa wenzako wanamaanisha nini wanaposema heri waje majaji wa nje si kwamba hawajui kuwa haiwezekani bali ni kuonyesha kiasi gani serikali yetu na majaji wake wanavyofanya kazi kwa matakwa ya watawala sometimes you should read between the lines si kila kitu lazima kiandikwe direct hiyo ni lugha ya picha tu.
 
Mahakama zetu za juu ziko huru sana kuliko mahakama nyingi za Afrika. Hii ni tangu enzi za Nyerere. Tatizo letu kubwa liko kwenye mahakama za chini ambako watu wengi zaidi ndio hukutana nazo katika kutafuta haki.

Ukija kwenye Mahakama Kuu na ile ya Rufaa.. sina mashaka nazo kabisa.

Tatizo letu ni kuwa bado hatujafikia mahali pa serikali kuheshimu Mahakama kama vile isivyoheshimu Bunge. Matokeo yake maamuzi ya Bunge na Mahakama kwa serikali yamebakia kuwa ni mapendekezo tu!
 
Binafsi bado ni muumini mzuri wa dhana ya uhuru wa mahakama pamoja na madudu yanayotokea huko sometimes.,nadhani Jaji mkuu amelipa uzito unaostahili ndio maana katika usikilizwaji wa rufaa hii Bench litakuwa na majaji 7.

Naheshimu sana busara za majaji hawa wa mahakama yetu ya juu kabisa ambayo ndiyo "fountain of Justice", naomba tu haki itendeke, kama rufaa haina merits basi ishindwe na kama ina merits basi uamuzi utolewe accordingly.
 
Mzee Mwanakijiji,

Right on,

Haya mambo ya mgombea huru alishayasema Jaji Nyalali (namsifu mzee yule kwa uthabiti) prior to 1992, though yalikuwa katika tume.Serikali ika pick and choose kipi cha ku implement.

Mahakama Kuu na ya rufaa zina ahueni, nakumbuka kuna majaji kama kina Lugakingira (thabiti mwingine huyu) walikuwa na misimamo bila kujali sana maoni ya serikali kuu.
 
- Hili swali niliwahi kmuuliza Waziri wetu wa sasa wa sheria, akaniambia tena bila hata ya kufikiri sana kwamba sheria ya jamhuri iko wazi kwamba wale majaji wa Mrema walikosea, kwamba mahakama haina nguvu kisheria ya kutunga sheria ya independent candidates, isipokuwa ni wabunge tu bungeni tena kwa 2/3 sasa kama alivyosema ni kweli hapa hakuna kesi wala hope, ni waste of time!

Respect.

FMEs!
 
Field Marshall ES,

Kuna sheria nyingine si lazima ziainishwe kwa kutungwa na bunge. Kuna sheria nyingine zinatoka moja kwa moja kwenye katiba.

Ndiyo maana nikasema Mtikila ana bonge la kesi, kwa sababu katiba imetoa sifa za mtu kupiga au kupigiwa kura, awe Mtanzania aliyefikisha umri fulani na asiye na matatizo ya akili etc etc. Katiba haikusema kwamba lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa.

Kwa hiyo utaona sheria ya kuruhusu wagombea binafsi Tanzania ipo katika katiba, na hili la kuzuia wagombea binafsi linakwenda against the spirit if not the letter of the constitution.

Sasa kukataza wagombea binafsi either kunakuwa unconstitutional, au kunaleta a constitutional crisis.
 
Ujinga wa kutojiamini kama Taifa. Kwani hao kina Manento ambao mwanzo walikubaliana na Mtikila walikuwa Wakenya?

Jengeni imani na taasisi zenu. Ndio maana wakenya wanawashughulikia kila siku kwa kutojiamini kwenu. Watanzania bana!

Wewe ndiyo unajichangana mkuu Bigilankana na labda nikueleze historia ya kesi ya wagombea huru toka mwanzoni mwa miaka ya 90!

Mwaka 1992 huko mahakama kuu kanda ya Dodoma,Mchungaji Christopher Mtikila alifungua kesi ya katiba kutaka wawepo wagombea binafsi;Jaji Kahwa Lugangira(sasa marehemu)alikubaliana na hoja ya Mtikila hasa kwenye kipengele cha katiba kisemacho"kila mtu ana haki ya kupiga na kupigiwa kura";kwenye kipengele hicho hamna hata sehemu moja inayosema kupiga au kupigiwa kura lzm usimamishwe na chama cha siasa;hivyo serikali ikabwagwa kwenye mahakama ya kisheria!

Serikali badala ya kukata rufaa ikakimbilia Bungeni na kumbuka kipinidi hicho Bunge lilkuwa la CCM tu,na kufuta kinyume cha katiba hukumu ya mahakama halali;uamuzi huu wa kutokata rufaa na badala yake kukimbilia bungeni ni udhalilishaji mkubwa mno wa mojawapo wa mihimili 3 ya dola,na uamuzi huu uliofanywa na akina Mrema na akina Warioba kipindi hicho unawasuta hadi leo na labda hadi wakiingia kaburini!

Mwaka juzi tena Mtikila alifungua kesi kudai tena wagombea binafsi na akashinda kesi hiyo kama alivyoshinda mwaka 1992!Na kwa vile sasa serikali ya CCM inajua watz wameelimika kwenye mambo ya katiba safari hii wakafuata mlolongo mnaokubaliwa-wakakata rufaa kupinga hukumu hiyo na ndiyo itaanza kusikiliza hivi karibuni!

Bagilankana;mm nawaunga mkono wale wasio amini taasisi zetu kwenye kesi hii hasa baada ya uamuzi wa Jaji mkuu alipoteau majaji 7 badala ya 3 kupitia rufaa hii.Wasi wasi wangu ni huu "kwa vile katiba inasema wazi kupiga na kupigwa kura ni haki ya msingi tena ya kikatiba ya kila mtz;iweje ateue majaji 7 kwa kesi rahisi kama hii?Kumbuka mwaka 92 na mwaka 2007 majaji waliokuwa wanasikiliza kesi hii walitumia muda mfupi sana kuimaliza maana kila kitu na ushahidi upo ndani ya katiba!

Yetu macho,lkn suala la kuwa na mgombea binafsi ni haki ya kila mtz na ipo ndani ya katiba na wala sio suala la kuomba toka kwa akina Mathias Chikawe!Maana haiingii akilini hata kidogo kuwa "kupiga kura upo huru hata kama hauna" chama lkn "kupigiwa kura lzm uwe na chama cha siasa kilichokuteua"!
 
Tuangalie katiba inasemaje kuhusu mgombea urais na ubunge

Ibara ya

39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-

(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipakodi yoyote ya Serikali.

Ibara ya 67
.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-

(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote

ya Serikali

 
Luteni,
- Thank you great thinker, hivi ndivyo tunavyopaswa kujadili hoja, kama hii ndio katiba kumbe hakuna kesi ni waste of time maana hapa umekatwa mzizi wa fitina!

Respect.


FMEs!
 
Mimi si mtaalam wa sheria naombeni msaada nimeangalia toleo hili la katiba sijaona sehemu yeyote inayompa mtu haki ya kuchaguliwa lakini inampa haki ya kupiga kura tu hapa ndipo najiuliza kama katiba imetoa haki ya msingi au kuna sheria nyingine iliyotungwa kumpa haki hiyo hivi kupiga kura ndiyo kuchagua? naomba msaada

(Toleo hili la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977,
limezingatia na kuweka pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Katiba
ya Muungano tangu ilipotungwa mwaka 1977 hadi tarehe 30 Aprili, 2000)

Ibara ya 5.-
(1)Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.
(2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo-​

(a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;​

(b) kuwa na ugonjwa wa akili;​

(c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;​

(d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama mpiga kura, mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyoteinayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura​

 
Hivi naomba kuuliza kwa washabiki wa hii proposal ya mgombea binafsi. In general mgombea binafsi atasaidia vipi katika jamii au hata fanya kitu gani ambao especially wabunge wa sasa hawafanyi? Na vile vile ni kitu gani kinachomfanya asigombee kupitia chama?.
 
Back
Top Bottom